Download Chereads APP
Chereads App StoreGoogle Play
Chereads

The crown's inheritance:Urithi wa taji

🇹🇿Bahati_Idd_Rigambo
--
chs / week
--
NOT RATINGS
21.1k
Views
Synopsis
Katika mchana wa baridi kali....Dragona anamsaidia mtu asiyemfahamu na kumficha ndani ya chumba chake.Balaa linakuja kutokea baada ya Annia,mke mtarajiwa na binamu wa kijana huyo shujaa Amarilla kuingia ndani ya kijiji cha Matix kumtafuta Amarilla ili warudi kukamilisha swala la ndoa ili mrithi wa taji apatikane Nani alidhani kama uzuri wa Dragona utakuwa chanzo chatmaumivu yake? Nani alidhani kwamba,huruma yake ndio chanzo cha matatizo yake? Na mwisho wa yote ni upi? Nani mrithi wa taji? Fuatilia....
VIEW MORE

Chapter 1 - Sura ya 1:pete

Matix village

Warembo wanne waliovalia nguo za asili ya kiafrika walikua wakizunguka zunguka ndani ya msitu.Zebrana,Yusra,Asteria na Emma ndio majina yao.

"Jamani mimi naona bora tukaogelee kidogo.Leo jua ni kali sana"

Akasema Zebrana kwa upole mno

"Yaani hiI laana imetushukiwa sisi sote na hatujui ni lini itaisha.Tangu muda mvua haijanyesha hata kidogo na wala hatujui mwisho wake."

Akasema Emma kwa masikitiko makubwa mno.

"Nina mashaka tusije tukafa kwa kiu na njaa."

Zebrana akasema na kuwafanya wote sasa wamtazame.

"Nina imani mungu atatutendea miujiza tu."

Asteria akasema kwa hisia kali mno.Ghafla wakasikia kishindo cha kitu kudumbukia majini.

"Nani?" akauliza Yusra kwa mashaka na wnte wakakaa kwa tahadhali.

"Tukimbie jamani." wakaamua kukimbia wote isipokuwa Asteria ambaye akaingia majini kwa ujasiri mkubwa.

"

Kuna ninï?" wenzake wakauliza wakiwa mbali mno.

"Ni salama,hamna tatizo." akasema na kutoka lakini mkononi Alikamata pete ya dhahabu yenye kichwa cha simba.

"Inamaana hii pete ndio yenye kishindo kikubwa namna hi?"

Akajiulïza na kuamua kutoka haraka.

Ndani ya mji mkuu~misri

Chumbani kwa firauni Hadas~

Firauni alikuwa amelala kitandani huku hali yake ikiwa sio nzuri kutokana na ugonjwa uliomtesa kwa muda mrefu mno na kwa wakati huo.....tayari ulimfikisha pabaya sana.Firauni alibarikiwa watoto wawili tu,wakike na wa kiume.Annia na Senet.

Utawala w@ke bado ulikuwa ukiogopwa sana sababu ya watoto hawa wawili hususani huyu Annia alirithi roho mbaya mno ya baba yake.Mbali na hivyo alikuwa mzuri na uzuri wake haukuwah kumpata mshindani kwa miaka yake yote 26.

Senet naye alikuwa na mvuto wa kipekee kiasi kuwapa ndoto wanawake wengi ya kuwa naye.

Firauni aliwaita kwa lengo la kuongea nao juu ya jambo fulani.

"Unaelewa ninavyokupenda Senet..hali yangu sio nzuri hata kidogo na naona sina maisha marefu kutoka sasa."

Akasema Firauni kwa masikitiko

"utapona baba ondoa shaka." akasema Annia akimpapasa kichwani baba yake.

1Bahati Ligambo1