Majira ya usiku tena wa mvua kali,anaonekana mdada mzuri kweli kweli akiingia kwenye lango la kuingilia kwenye kijiji cha Matix.
Alikuwa amevalia nguo za kitawala na macheni cheni mengi ya almasi.
,"Atakuwa wapi huyu mtu?"
Akajiuliza na kuingia langoni taratibu.Ile anaingia tu,mvua ikakata ghafla na kubakisha manyunyu na upepo mkali.Nani alitegemea wala kudhan kuwa huo ndio mwisho wa watu wa Matix?
Nani alitegemea kuwa siku hiyo ndio majanga na matatizo yataanza kwenye kijiji chao?
Hakuna anayejua.
"Afadhali hata mvua imeacha kunyesha kwa ukali ule."Dragona akajisemea na kuchungulia dirishani tu.Hata hivyo upepo ulikuwa mkali mno kiasi kupeperusha nyewe zake nzuri za kahawia.
"Jamani hizi nywele kha!" Akalalamika Dragona akijitahidi kuziweka vizuri lakini zikawa zinamshinda hivi.
Ghafla sana,akashtukia nywele zake zikikusanywa kurudishwa nyuma kwa utaratibu mno na ukarimu.
"Nani?" Dragona akageuka kwa fujo kutazama ni nani maana ni mtoto wa kike alafu kushikwa shikwa bila taarifa sio vizuri.
"Shhhh!!!" Akanyamazishwa asiendelee kupiga kelele.Ni Amarilla mwenyewe ndio alikuja pale.
"Mimi ni mlinzi wako hivyo lazima nikusaidie kwenye hali yoyote ile."
Amarilla akaanza kuzifunga funga nywele za Dragona tena.Ghafla kabisa nywele zote zikavuruguka tena na upepo.Jamani huu upepo huu mbona una mambo?
"Ah!!!"Dragona akajikuta akimkombatia Amarilla kwa uoga mno.
"Ni sawa usijali" Akasema Amarilla na ghafla Dragona akajitoa taratibu kumtazama Amarilla usoni taratibu.Akajikuta akitazamana naye kwa muda mrefu kidogo.
Mungu wangu!Saa ngapi Amarilla asianze kumsogelea Dragona? Amarilĺa akamsogelea na kumpiga busu moja hatari.Dragona akajikuta akipaa paa kwa raha.Akamkombatia na kumpa ushirikiano katika hilo.Raha juu ya raha,utamu zaidi ya utamu.