Chereads / The crown's inheritance:Urithi wa taji / Chapter 4 - Sura ya 4:inavutia?

Chapter 4 - Sura ya 4:inavutia?

Dragona akauliza "kwanini"kwa ishara tu ili ahakikishe.

"inasemekana ni laana,pete ya Amarilla imepotea."

Dragona akashtuka zaidi.Haraka akarudi ndani na kuitoa pete

"Umeitolea wapi hii pete?"

Emma akauliza kwa shauku kubwa mno na tamaa ndani yake.

"Inabidi tuirudishe" Akasema kwa ishara Dragona

"Sawa,naomba tu iwe siri maana wananchi wakijua tu jua umekufa wewe,"

Emma akasema lakini ghafla akaja Yusra eneo lilee na kuiona ile pete

"Ah!Kumbe nyie wezi ewh na ndio mnaotuletea laana sio?

Akauliza kwa hasira kali mno tena sana.

"Sasa naenda kusema kwa mkuu wa kijiji ili muuwawe nyote!"

Akasema na kutoka mbio eneo lile.Emma akamshika mkono Dragona na kumsimamisha juu.

"Cha kufanya ni tutoroke tu hapa haraka.sawa?"

akasema Emma.Dragona akabaki kulia tu asiwe na namna Sauti za wanakijiji kupiga kelele kuja nyumbani kwa kina Dragona zikatawala na hatimaye wakafika nyumbani kwa kina Dragona.

"Choma moto nyumba yote!"

Mkuu wa kijiji akaagiza baada ya kutomkuta mtu mule ndani.

"Aya tawanyikeni kuwatafuta ila muwalete wakiwa hai.Hawawezi kutusababishia matatizo na laana za bure sisi."

Kweli watu wakatawanyika haraka kuwatafuta kina Dragona.

Dragona na Emma tayari walishaondoka na kufika mbali kwa kutumia usafiri wa farasi wa kina Emma.Hata hivyo..hakumuacha nyuma mdogo wake Asteria.Aliogopa angelimuacha basi angeliuawa

siku kumi na tano mbele...

Tayari waliingia Misri wakiwa na ile pete mkononi.kwa wakati huo walikuwa wakikatiza maeneo ya msituni kabla ya kuingia mji mkuu.Ni lazma ukatize hapo.

Jambo wasilolijua ni kuwa huo msitu una wezi na majambazi wa kutosha.Dragona akalifungua lile boksi na kuitoa pete kisha wakaitazama.

"Inavutia?" akauliza Emma na kumfanya Dragona atabasamu .

"Tabasamu lako linaonyesha umeipenda mno hiyo pete"

akaongeza kusema Emma.Ghafla watu wasiofahamika wakawa wanateremka kutoka juu ya mti.

"Leteni hiyo pete haraka!!" wakasema kwa ukali lakini ukimya ukatawala.

"Mukitaka kuwa hai mulete pete hapa"

"sawa tutawapa pete lakini lazima tuikabidhi wote kwa muhusika.Niko pamoja nanyi.Si ndiyo Dragona?"

Akauliza Emma lakini alipogeuka ,Dragona hakuwepo tena.

"Dragona!!" akaita kwa mahangao mno.

"Kwahiyo wewe ulikuwa unatuzuga ili mwenzako aondoke na pete sio?"

Wakauliza kwa ukali mno