"Niache tafadhali." Akasema Dragona akijitahidi kujichomoa mikononi mwa yule mkaka.
"Nimesema niachie!!!!" Akafoka na kumsukuma kando yule mkaka.Ghafla mlango ukagongwa.!
"Fungua mlango Dragona mshenzi wewe!! Akafoka mzee Omnan kwa hasira kali sana.
"Mungu wangu baba amekuja....!" Dragona akachanganyikiwa sasa.Huruma imemponza au?
"Dragonna fungua mlango haraka lasivyo nikiingia humo ndani nitakumaliza.!!!"
Mzee akafoka na kuagiza mlango ufunguliwe kinguvu nguvu.Kabla hawajafungua,mlango ukafunguliwa na Dragonna mwenyewe.
"Baba mbona hivyo?" Akauliza Dragona akiwa na hofu kidogo.
"Utaelewa tu wala usijali."
Akaamua kuingiza watu ndani na kuagiza wakague kila sehemu.
"Baba unatafuta kitu gani?"
Dragonna akauliza kinafki na kumfanya baba yake amgeukie kwa ghadhabu.
"Atakuwa wapi?" Akauliza akionekana kutokuwa na utani.
"Nani tena baba?"
"Huyo mwanaume anayekuharibu."
"Hakuna mtu baba."
Dragona akasema kwa ujasiri baada ya msako kuisha bila kuonekana mtu yeyote mule ndani.Baba yake akamtazama na kutabasamu tu.
"Hakuna kitu mwanangu."
Akasema na kutoka na watu wake.Dragona akarudi ndani na kufunga mlango.
"Asante Mungu!" Akasema na kukaa kitandani.Hapo akateremka yule kijana.Kumbe alikua akining'inia juu ya paa.
"Unaitwa nani kwanh??"
"Amarilĺa jina langu."
Akajitambulisha yule mkaka.