Chereads / The crown's inheritance:Urithi wa taji / Chapter 11 - Sura ya 11:Mlinzi binafsi

Chapter 11 - Sura ya 11:Mlinzi binafsi

Zebrana akamtazama Amarilla kwa muda.

"Mbona unanitazama hivyo?"

Akauliza Amarilla kwa mapozi mengi.

"Ina bidi urudi kwenu Amarilla.Kwenu wapi?"

"Kwetu!"

"Ndiyo."

"Siwezi kurudi kwetu kwa sasa."

"Kwanini?"

"Kwasababu sikumbuki kwetu ni wapi."

"Ina maana hauna kumbu kumbu au?"

Zebrana akaukauliza kwa mshangao mkubwa mno.Ni nini kimemkuta kijana mzuri kama Amarilla mpaka asikumbuke kwao?Maajabu gani haya labda?

"Kwahiyo itakuaje?Utaishi wapi labda?"

Akauliza akïonekana wazi kuchanganyikiwa.

"Nitaishi nilipo sasa."

Akajibu Amarilla na kumfanya Zebrana ashtuke.

"Unamaanisha hapa?!?"

"Ndiyo."

"Acha utani wewe!"

"Namaanisha."

"Ngumu,baba yangu ni mkali sana ujue."

"Sijali.Tena ngoja nimuonyeshe."

Amarilla akasogea mlangoni na kuufungua alafu akatoka.

"Wewe unataka kufanya ñini?"

Akauliza Zebrana baada ya Amarilla kuanza kuita watu kwa mbwembwe.

"Subiri usiogope."

Amarilla akamuaminisha.Watu wakaja haraka eneo lile na kubaki kumshangaa tu Amarilla

"Nani wewe?"

Akaulïza mzee Omnan kwa ukali mno.

"Zebrana huyu ni nani?" akamuuliza binti yake kwa ukali.

"Baba huyu...huyu...."

Akabaki kujing'ata ng'ata tu mtoto wa watu.

"Naitwa Amarilla,nimekuja hapa kuomba ajira.."

Akajitambulisha Amaliĺala.

"Ajira gani?"

"Ya ulinzi.Mimi najua mtoto wako unampenda sana na uko tayari kufanya chochote kwa ajili yake.Uongo au ukweli?"

Akauliza Amarilla

"Ukweli lakini..."

"Hakuna cha lakini..watu wanaweza kumteka mtoto wako na kumtumia kukuangamiza kwenye biashara.Mimi naweza kumlinda mwanao vizuri.Je uko tayari?"

Amarilla akauliza.Omnan akakaa kimya kwa muda akifikiria jambo.

"Au niondoke?"

akauliza.

"Unajua watu wengi wanataka kuniajiri ila nimekuchagua wewe,kama hutaki sema niondoke."

Akatishia Amarilla.

"Sawa,nimekubali." Mwisho Omnan akakubali.Zebrana akajikuta akitabasamu kwa ujanja wa Amarilla.Ana nini huyu kijana mbona kama anamvutia taratibu?