" Hayo ndo maamuzi yangu...wewe utaolewa na Senet .Leo usiku Amarilla atawasili."
Akasema firauni Hadas.Annia hakujibu chochote zaidi ya kutoka kwa hasira
"Mungu anipe nini mimi?"
Kwa Emma ikawa ni furaha kubwa mno baada ya kuanza kuandaliwa tayari kwa kukutana na mumewe mtarajiwa,prince Amarilla.
~usiku wa manane kidogo kama saa tano hivi~
Dragona yeye fahamu ndio zikawa zinamrejea.Akashtuka baada ya kugundua mazingira aliyopo ni tofauti.Kwa haraka haraka tu akagundua labda huenda ametekwa na watu asiowafahamu.Haraka akasogea mlangoni alafu akageuka tena kutazama ndani.
"Asteria!" mawazo ya mdogo wake yakamjia tena na hapo hapo akatoka nje kumtafuta kwenye vyumba vinghne.
"Nitampataje mdogo wangu jamani lakini...?"
Akajiuliza akionekana wazi kuchanganyikiwa
Kwenye baraza kuu,tayari Amarilla alikaribishwa.
"Karibu sana mwanangu."
Firauni akamkaribisha na kumkombatia akifuatia na Senet.
"Annia hujambo?"
Akauliza Amarilla na hapo Annia akatabasamu.
"Bila shaka" Akajibu na kumkombatia lakini ghafla ....mlango ukafunguliwa na kuingia Dragona.
Moyo wa Amarilla ukashtuka vibaya mno baada ya kumuona Dragona.
"Dragona!"akaita kwa mshangao.Annia sasa ndio akashtuka zaidi.Kiufupi watu wote hata firauni.
"Dragona ....huyu si nilimmaliza tayari.Mbona awe hai?"Annia akajiuliza na kufumba macho.Hapo kumbukumbu za hilo tukio zikamjia kua alimsukuma kwenye bonde refu mno.
"Kwakuwa unataka kumchukua Amarilla wangu...kufa tu Dragona.Kufa wewe na mwanako wa tumboni."
Akakumbuka Annia kuwa hayo ndiyo aliyo mwambia Dragona kabla ya kumsukumia bondeni.