Amarilla akamsogelea Dragona na kumtazama kwa umakini mno.Ni wazi hakua akiamini kuwa anamuona Dragona mbele yake.
"Dragona!" akaita kwa upole na kumshika shavuni.
"Nakuchukiaa!!" ghafla akayakumbuka maneno hayo.Ni mambo makubwa mno yaliyotokea hapo kati kati
"Mungu wangu,kama huyu Dragona yuko hai inamaana nitajulikana kuwa mimi ndiye muhusika wa lile tukio lote na ndio chanzo cha Dragona kuwa bubu."
Annia akajisemea.
"Mke wangu...." Akasema Amarilla na kumkombatia Dragona.
"Huu ndio mwisho wangu ama la?"
Akajiuliza Annia.
~miaka sita nyuma~
Dragonna alikuwa na marafiki zake wale wale wakitembea tembea kando ya piramidi kubwa...
"nataman niingie mule ndani jamani...." akasema Dragona kwa hisia kali mno balaa.
"tunaweza kufanya ujanja tuingie ndani jamani." akasema Asteria na kukimbia kuzunguka nyuma.
Dragona akaamua kupita upande wake lakini ghafla akasikia sauti ya mtu kugugumia kwa maumivu makali.Akasimama na kutega sikio vizuri asikie .Haraka akazunguka na hapo akamuona mkaka akiwa amelala pembeni ya ukuta akivuja damu mno..
Akamsogelea na kumgeuza na hapo akakutana na sura nzuri mno...
"mungu wangu!" akashtuka na kurudi nyuma haraka