"jamani njoeni huku harakaa!" akpiga kelele lakni hakusikika hata kidogo.
"hapana,usiite watu." Akasema yule kijana na kumfanya Dragona amsogelee tena.
"Kwanini?" Akauliza kwa upole na huruma nyingi lakini yule kijana hakuweza kujibu.Akapoteza fahamu pale pale!
"Wewe!Wewe! hebu amka,Wewe!"
Akaita lakini hakukuwa na majibu yoyote.Akaamua kumsaidia kigumu gumu tu.
~baada ya muda mrefu sasa~
"Kwanini ulitukimbia?" Akauliza rafiki yake Emma kwa hasira kali.
"Poleni jamani."
Akasema kwa upole mno na tahadhali.
"Hujasema kwanini bado."
Akakazia Asteria,wakati huo akiwa kijakazi wake maana Dragona alikuwa mtoto wa mfanyabiashara mkubwa tu.
"Jamani nilipata wito tu ndio maana."
Akajitetea.
"Sawa,tukaribishe ndani basi kwanini leo utuache nje?"
Wakauliza wote.Ghafla wakasikia mguno wa kiume kutokea chumbani kwa Dragona .
"Kuna nani huko?" Akauliza Yusra akisogea mlangoni.
"Hakuna mtu.Mumesikia vibaya tu."
Akajitetea.
"Hebu tuangalie"
"Nimesema hakuna mtu!!" Akafoka na kuwafanya wote warudi nyuma kwa uoga.Hawakumzoea Dragona kwenye hali hiyo ya hasira.
"Tokeni haraka" Akasema na wote wakatoka kwa utii.
Dragona akafunga mlango na kwenda chumbani kwake.Hapo akamuona yule kijana akiwa amekaa kitako kitandani akishika kifua chake kuugulia maumivu makali.
"Kaka uko sawa?" Akauliza akimsogelea.
"Kaka..." Ghafla akavutwa na kulazwa kitandani kibabe balaa.
"Wewe nani na kwanini nipo hapa?" Akauliza yule kijana kwa ukali.
"Jamani mi..mimi ni ..nimefanya msaada tu."
Akajitetea Dragona.Yule kijana alikuwa juu yake kiasi wakawa wanashea pumzi zao kwa pamoja.Wakatazamana.Dragona mapigo ya moyo wake yakawa yaenda kwa kasi tu.Akataka kuinuka lakini akazuiwa!
Yusra sasa akapeleka umbea kwa baba yake Dragona.
"Haiwezekani,nani anamwaribu mwanangu wakati nategemea posa mimi?"
Akafoka na kuamua kwenda chumbani kwa Dragona akiwa na panga mkononi.