Baada ya kumfikia tu Annia,akamsukuma na kumkata upanga yule chui!
Yeye na chui wote wakadondoka chini kando kando.Kwa mara ya pili tena akawa ameumizwa.Kwa mara nyingine tena akawa ameumizwa .Chui yule alimkwarua ubavuni.Akajikuta akipoteza fahamu pale pale.
Ghafla sasa ndio akaja Emma.
"Dragona!"
akaita na kumkibilia .Annia alikuwa amelala chini hoi taabani.Emma akatwazama kushoto na kumuona yule chui.m
Akamsogelea taratibu kuhakikisha kama kweli amekufa ama la.
Ingawa kwa uoga,...akauchomoa ule upanga na kuutazama.
"Natamani mimi ndio ningekua nimemuuwa huyu chui"
Akasema Emma akitabasamu.
"Wewe ndiye uliyemuuwa huyu chui?!!"
akauliza Senet baada ya kuwa kawasili.Yeye alichosikia tu ni kuwa "nimemuuwa huyu chui."
Emma akabaki kimya asiamini
:Mimi...."
"Tuongozane tafadhali.."
"Lakini... " Emma akaogopa mno akijua labda amebebeshwa msalaba wa dhambi bure.
Annia akanyanyuka na kumtazama Senet kisha Dragona.
"Tuondoke kaka."
akasema na kutoka haraka eneo lile.
~kwenye kasri kuu~
Dragona akapatiwa msaada wa kimatibabu yeye na mdogo wake Asteria.Wakati huo Emma akiwa amepelekwa kwa firauni
"wewe ndiye uliyeuwa chui?"
akauliza firauni .Emma akabaki kimya .Moyoni akamlaani mno Dragona kwa kumsababishia matatizo.
"Ukimya wako unamaanisha kuwa ni kweli."
kauli hiyo ikamfanya Emma atake kuzimia kabisa kwa uoga.Firauni akavuta pumzi ndefu na kumtazama Emma.
"Umefanya jambo la kishujaa mno kumuuwa chui yule maana alikuwa anatusumbua sana.Angelikuwa binti yangu Annia ndio amefanya hivi basi angekuwa mrithi wa mali zangu na mrithi wa taji langu pia.Kwakuwa wewe sio mtoto wangu...utaishi hapa na kuolewa na kijana wangu mmoja."
Akasema firauni na kumfanya Emma acheke kwa furaha.
"Sio mimi niliyeuwa chui ila manufaa nayapata mimi."
akajisemea Emma moyoni
"uUtaolewa na kijana wangu Amrilla."
Firauni akasema na kumfanya Annia ashtuke.
"Baba!Huyu aolewetna Amarilla binamu yangu?"
Akauliza kwa mshtuko.Moyoni mwake mwanaume aliyekuwa akimtamani ni Amarilla tu,alafu Emma ndio aolewe.we!Ngumu kukubalika.