Dragona yeye alikuwa akiikimbiza ile pete lakini ghafla akajikwaa na kudondoka chini chali.Pete nayo ikadondoka chini.Harqka Dragona akaiwahi na kuitazama
"Sasa niifanyaje hii pete?"
akajiuliza Dragona na mwisho akapata wazo.Akaamua kuimeza ile pete.Ile anamaliza kuimeza tu,akazungukwa na watu wale.
"tupatie pete haraka!"
wakasema kwa ukali lakini wala Dragona hakuwa na uwezo wa kuwajibu.
Wale watu wakaona kama anawadharau hivyo mmoja akachomoa upanga na kumchoma nao Dragona tumboni.Dragona akadondoka chini pale pale.
Wale watu wakaanza kuitafuta pete,lakini hawakuiona.Wakaamua kuondoka zao haraka eneo lile.Emma sasa ndio karoho kakaanza kumuuma...akaamua kumrudia Dragona lakini wala hata hakumkuta pale chini.
"Atakuwa ameenda wapi huyu?"
Emma akajiuliza .Ghafla akaiona michirizi ya damu.Akatabasamu na kuanza kuifuata ile michirizi ya damu ili ampate.
Dragona mwenyewe alikuwa akijitahidi kutembea kutoka ndani ya msitu,tayari alipata hisia za alipo muhusika wa pete.
Msituni hapo pia.Annia na kaka yake walikuwa wakifanya mazoezi ya kuwinda.
Dragona akiwa anatembea tembea ghafla akamuona chui amelala mbele yake.Kwa uoga na utaratibu,akaanza kurudi nyuma.Akiwa anarudi nyuma ,akajikuta akikanyaga majani makavu na hapo sauti ikatengenezeka.Chui akageuka haraka na kumuona Dragona.
Dragona akadondoka chini kwa uoga baada ya chui kuanza kumfuata mbio mbio.Akafumba macho akisubiri kifo chake lakini kabla hata chui hajamfikia,akatokea Annia na kumsukuma mbali yule chui!!Chui akadondokea kando.Annia akatupa upanga
"Nitafurahi kukuuwa kwa mikono yangu."
Akasema Annia na kutoka haraka kumkabili.Dragona akainuka haraka haraka na kusimama.Annia akaendelea kupigana na yule chui mpaka chui akalala chini.Annia akatabasamu na kumgeukia Dragona taratibu
"Aah!" akajikuta akishangaa baada ya kumuona tu Dragona.
Akiwa amezubaa kumbe chui aliamka na kuanza kumkimbilia Annia amrarue.Dragona akatamani kumshtua Annia lakini hakuweza maana bubu na kila akimpa ishara Annia hamuelewi..
Alichoamua na kuokota upanga na kumfuata Annia ili amuokoe.