"Mungu wangu!Hii @si ni pete ya kifirauni na naijua historia yake...yeyote atakayeshika na hana damu ya kifirauni basi atakufa ama kupalalaizi."
Akajisemea moyoni Dragona.
"tutaiuza dada?"
akasema Asteria baada ya kuwa kampokonya pete dada yake.Dragona akatoa ishara ya kukataa.
"Kwanini dada?"
Akauliza kwa hofu lakini pale pale akadondoka chini!Dragona akajitahidi kumtikisa lakini wapi.....
"Lazma niirudishe hii pete kwa lengo la kumuokoa dada yangu."
kabla ya kufanya hivyo akaona bora aite waganga wa kienyeji.hata hivyo...hawakufua dafu.
Dragona akiwa anamfuta futa jasho mdogo wake Asteria..ghafla akashangaa pete inatikisika.Akabaki anaitazama kwa muda asielewe.Mwisho pete ikadondoka chini!
Ikabidi Dragona aiwahi maana alihisi huenda kuna watu wanataka kuiiba kichawi.Akiwa anaitazama ghafla ikamuunguza na kumfanya aidondoshe chini!
Akakamata kitambaa na kuoshika tena vizuri alafu akaifungia ndani ya boksi la kutu
la chuma.
Sasa kumbe Annia ndiye ambaye alikuwa akiivuta kichawi ile pete.Akajikuta akifeli na kudondoka chini.Haijawahi kutokea akashindwa hata mara moja.Hakuelewa kwanini.Akalala sakafuni akihema vibaya mno.kwa upande wa Dragona akaamua kulala.
Asubuhi na mapema sasa ndio akaamka kama kawaida yake na kukamata fagio tayaeri kwa kwenda kufagia.
Akiwa anatoka ghafla akashtuka baada ya kumuona Emma akiwa anakuja mbio huku akikimbia kumfuata.
"Dada Dragona..."
akamkombatia akilia vibaya mno.Dragona akatoa ishara ya kuuliza tatizo nini?
"Dada,watu wanakufa hovyo hovyo na sababu haijulikani."
akasema akizidi kulia.Dragona akashtuka vibaya mno maana alianza kupata mashaka huenda ni pete ile ile tena sababu.na kuirudisha ingekuwa tatizo maana nchi ya misri hawaruhusu bubu kuingia..