Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 20 - NINI KINAENDELEA

Chapter 20 - NINI KINAENDELEA

Ghasia katika fikra za Ed ziliendelea kwa takribani wiki nzima na kuleta ugumu kidogo kwa watu waliomzunguka ofisini na nyumbani pia.

Mara zote alikuwa akikagua hiki na kile akiita huyu mara yule kati ya wakuu wa idara kila alipoona dosari.

Allan alikuwa na kibarua cha kulainisha mioyo ya wote waliotoka ofisini kwa Ed wakiwa hoi kwa maswali.

"Boss vipi hii wiki kuna wakaguzi nini maana Mkuu ameshika mpini mwenyewe" aliuliza msimamizi wa mambo ya ugavi!

"Usijali Beno, ni kuhakikisha mambo yanaenda sawa" Allan alimpa jibu la kumtuliza asiendelee kuhoji.

Loy alikuwa busy hata muda wa kushika simu yake binafsi aliupata wakati wa chakula cha mchana. Muda huo pekee ndio aliweza kujibu jumbe alizopokea. Wakati mwingine alilazimika kuchukua chakula na kula akiendelea na kazi.

"Allan ni nini kinaendelea uwhhh, vidole vyangu vinauma kwa kuchapa ripoti" alilalama Loy wakati wakitoka ofisini, wakimuacha Ed ambaye alirudi jioni hiyo na ndege akitokea G-Town alipoenda jioni ya siku iliyopita.

"Acha uzembe wewe" Allan alimtania Loy

"Sio uzembe boss bwana, Big boss hii wiki sijui kinachoendelea kichwani kwake, au kuna kikao cha bodi ya wanahisa?" Aliuliza Loy wakiwa kwenye lifti. Ilikuwa saa mbili na jengo lilikuwa na ofisi chache sana zilizokuwa wazi muda huo.

Allan na Loy walitoka mida hii baada ya Ed kuwakabidhi mambo ya kufanya kesho yake hivyo kuifanya leo kuwa siku ambayo wamewahi kutoka kulinganisha na siku tatu nyuma ambapo walitoka saa tatu hadi na saa nne

"Loy acha kusumbuka, hizo ni kazi za kawaida. Big boss ameamua kuangalia kampuni yake" Allan kama kawaida akijaribu kuweka mambo sawa.

Ukweli wa mambo Allan aliujua maana aliporudi nyumbani walijadili na Li mambo haya haya. Huku Li akimshuhudia Allan hata wao nyumbani wanakutana na hali hiyo hiyo.

"Kaka Li, kuna nini kinaendelea maana big bro amekuwa tight sana. Mara ya mwisho alikuwa hivi wakati baba alipofariki, nini kinamsumbua?" Aliuliza Coletha

Li hakutaka kuzungumza kile anachohisi mbele ya mdogo wake, maana alimjua ataanza harakati kama alizonazo yeye na angeharibu mapema.

"Atakuwa na changamoto ofisini, anafanya ukaguzi wa ndani!" Alijibu Li

"Mhhhh basi tutakoma, ameenda kwa mama kweli! maana jumatatu ni birthday yake, asiende yuko hivyo atampa stress ma" Coletha alimwelezea Li

"Oooh kweli bora hata umenikumbusha, nitaongea nae kuhusu hilo. Au ushafanya maandalizi yako maana unapenda sherehe wewe!"

"He he he usijali kaka Li, tutakuwa na chakula cha pamoja nyumbani na watu wachache ambao nitawajulisha. Mama kasema hataki sherehe".. alimpa maelezo kaka yake.

"Oooh basi sawa, itakuwa vyema". Alimaliza Li

***********

Ed alijua kabisa hizi siku amejaribu kuizamisha akili yake katika kazi ili kupambana na ghasia katika hisia zake ambazo zilileta ukorofi kila wakati alipotaka kuchukua hatua kumfuatilia Aretha.

Ilikuwa ajabu kwake binafsi maana hakuwahi kusumbuliwa na hisia za mapenzi kama hizi zilizompata ndani ya wiki mbili tu.

Alitamani kumuona Aretha, alitaka kumsikia lakini hakuwa na namba yake, kumuomba Loy ilikuwa hatari zaidi kwake.

Aliondoka mchana mmoja na kukuta ameegesha gari kwenye maegesho ya Capital University. Alikaa pale kwa muda lakini hakuweza kushuka chini. Alijiuliza angesema nini ikiwa angeulizwa sababu ya ujio wake.

Aliondoa gari yake taratibu na kurudi ofisini, na wakati huo akimuagiza Loy kumtafutia tiketi kuelekea G-Town jioni hiyo baada ya kuhisi hisia zake zitamuendesha vibaya.

Wakati akiwa pale chuo hakujua kuwa kuna watu wawili macho yao yaliona kile kilichoendelea,. Charles, rafiki wa Derrick mdogo wake aliona gari yake. Mtu mwingine alikuwa ni Theo ambaye ni mtu aliyepewa kibarua na Li kumfuatilia Aretha. Wote hawa walitoa ripoti kwa ndugu zake.

Ed usiku huu aliendelea kuangalia ripoti zilizokusanywa ofisini kwake na wakati huo simu yake iliita na hakuweza kupokea. Ni Joselyn. Hakumdharau, kilichomtisha kilikuwa ni kumdanganya msichana huyu iwapo angemuuliza kwa nini yuko hivyo.

Tangu juzi Joselyn alianza kumsumbua akitaka kujua nini kinaendelea sababu haikuwa kawaida yake kutopokea simu mara kwa mara.