Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 23 - DO I LOVE HER

Chapter 23 - DO I LOVE HER

"Champ, ni wewe pekee unaweza kuchambua kile unachokihisi, lakini kuna mstari mwembamba unaotenganisha kile kinachoendelea ndani yako. Unahitaji kuiambia nafsi yako ukweli. Je ulimpenda Lyn kwa dhati ya moyo au la?"

Maneno haya kutoka kwa Brian yalimsababisha Ed kuinama chini taratibu akishusha pumzi. Kimya cha dakika kadhaa kilipita na Bri alimalizia chakula chake huku akimpa rafiki yake nafasi ya kufikiri.

"Champ, ninaweza kusema ukweli huu, kwa Lyn it was easy! I didn't chase her, but kwa Aretha ninataka kumfuata, nataka kujua kila kitu kinachomhusu yeye. Ni mimi ndio namtaka zaidi. Ni mara mbili tu nimeongea nae lakini nataka kuongea nae tena na tena. Nikiongea na Lyn nahisi kama ninamdanganya maana moyo hautaki kusema maneno ambayo natamani kusema kwa Aretha! Napata shida kutulia kila nikimuwaza. Nipe maana moja ya haya nayofanya Bri, do I love her?"

Ed alinyanyua glasi ya maji na kunywa kisha akaegama kwenye kiti huku akimuangalia Brian ambaye alikuwa makini kumsikiliza.

Alimshangaa sana rafikiye, sababu hakuwahi kumuona hivyo akiwa na Joselyn. Alichofanya ni kumtambulisha kwake walipokutana kwenye sherehe za uzinduzi wa programu ya mabadilishano ya utaalam kati ya City Hospital na Country C. Brian alimfahamu kwa ufupi hapo lakini hakuwahi kumuona Ed akimsimulia mambo haya katika uzito anaofanya sasa kwa huyu Aretha.

"Kama rafiki yako, natamani kukuona unafanya maamuzi sahihi linapokuja suala la mwenzi. Kabla sijakupa maana ya kile kinachoendelea, mfahamu Aretha. Tafuta muda kumfahamu, take her as a friend you have met!. Kisha tuone maendeleo"

Ed alisikia ushauri wa rafiki yake Brian, kisha akauliza

"Kwa muda gani Champ? Nina wiki sasa mbele kumtambulisha Lyn. Na kama unavyomjua Lyn atatafuta kujua why namfuata huyu dada?"

Brian alishusha glasi na kutabasamu,

"Muda utaamua wewe, na ukiwa karibu nae utajua namna ya kukabiliana na Lyn, maana sitaweza kukwambia nini ufanye kuhusu kumtambulisha Lyn, unamjua na unaweza kukabiliana na chochote ikiwemo kusogeza mbele utambulisho... na kama utagundua hisia zako ni halisi kwa Aretha kuliko Lyn, you are a gentleman deal with it respectively. Talk to her. Mwambie ukweli bila kupepesa lakini kwa heshima na upole".

Mazungumzo haya yalimuacha Ed akiwa na ahueni ya kutosha kuliko alivyokuwa siku chache nyuma. Alishukuru sana kuwa na Brian, ambaye amekuwa msaada kwake mara zote kunapokuwa na changamoto za kimaisha. Hakufahamu kuwa Brian alikuwa anafahamu taarifa ya Aretha mapema kabla ya kumtaarifu. Linus alishampa hali ilivyo tangu siku ya kwanza alipomuona Aretha.

Walipomaliza alielekea nyumbani huku akikusudia moyoni wikiendi kumfuatilia Aretha. Akiwa njiani aliwaza kuitumia wikiendi hii pia kutengeneza mahusiano yake vyema na mdogo wake Derrick. Akachukua simu yake na kupiga namba ya Derrick, baada ya kuita kwa muda ikapokelewa. Mazungumzo yao yalikuwa mafupi lakini yalimpa Ed kujisikia vyema maana Derrick alikubali kuja nyumbani jumamosi kuonana nae.

Moyoni alihisi ushindi na furaha kabla kioo cha simu yake kuwaka kuonesha kuna mtu alitaka kuongea nae. Alipoangalia alipokea haraka huku mkono ukibaki kwenye usukani.

"Sema Captain" alisema Ed mara baada ya kupokea huku akiweka sauti kusikika

"Mkuu, kuna taarifa za kuvutia kutoka kwa Martinez" upande wa pili ulisikia

"Nambie" Ed alimpa ruhusa kuendelea!

"Our suspicions were true, Martinez ana kupe pale Boric ambaye ana cheo. Sababu ya delay nyingi ni huyu bwana anaingilia kati kila proposal za SGC zinapotumwa."

"Mmmm" aliitikia Ed huku mistari ikionekana kwenye paji la uso wake kuonesha hakupenda alichosikia..

"Lakini si hivyo tu tunaifuatilia nini kinaendelea kati yake na Waziri. Kesho watakutana. Tutakujulisha zaidi".

"Ok" aliitikia na kukata simu. Sasa alikuwa kafika nyumbani. Baada ya kuegesha gari aliingia ndani na kukutana na Coletha ambaye alikaa mezani tayari kupata chakula.

"Big Bro umewahi, karibu ufikie hapa" Coletha alimkaribisha kaka yake.

"Usijali sisy, niko vizuri, endelea tu tafadhali." Ed alimjibu na kuanza kuelekea kwenye ngazi zinazoelekea chumbani kwake.