Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 5 - KUFURAHIA MAMBO MADOGO II

Chapter 5 - KUFURAHIA MAMBO MADOGO II

Baada ya kuwasili, Ed alipokelewa na Meneja wa matangazo na kuelekezwa chumba maalum cha maandalizi. Haikuwa mara kwanza kwa Ed kuwa katika vipindi vya namna hii, alifahamu hatua zote kabla ya kuonekana kwenye runinga. Ndani ya chumba cha maandalizi, Ed aliendelea kupiga simu za kikazi huku nyingine zilizoingia akizielekeza kwa Allan aliyekuwa pamoja nae. Wakati huo Loy alitoka na kwenda kukaa kwenye jukwaa la hadhira ambalo hukusanya vijana wengi wa kike na wa kiume.

Maandalizi yalipokamilika, Rogders tayari aliingia ukumbini huku makofi mengi yakimkaribisha. Watu walimkubali sana sababu ya ubunifu wake na maswali yake kwa wageni ambayo yaliwapa msaada mkubwa wasikilizaji wake.

"Karibuni sana Ijumaa ya leo, tuamshe tena shauku ya kufanikisha ndoto zetu kwa kuwasikiliza wenzetu wanafanya nini" mwenyeji wako katika safari hii ni kapten Rodgers"

Makofi yalifuata hadi alipokaa kwenye sofa huku akiwa amezungukwa na kamera ambazo ziliongozwa kwa ustadi kutokea mbali.

"Macho yetu sasa tuyaelekeze kwenye screen kubwa kuona mambo machache kuhusu mgeni wetu?"

Kwenye screen alionekana Ed, katika matukio mbali mbali ya kiuchumi ambayo alishiriki, lakini pia alionekana hadi alipoingia kwenye eneo hili. Ilipomalizika clip fupi, Rodgers akaendelea

"Tayari kama mlivyoona mgeni wetu yuko ndani ya mjengo huu, without further ado weka mikono pamoja, inuka tumkaribishe Edrian Simunge the senior bachelor!

Watu waliokuwa wamejaa jukwaani waliinuka na kupiga makofi kumkaribisha Ed ambaye sasa aliingia huku akipunga mikono na kuinama ishara ya heshima kwa hawa watu waliosimama.

Baada ya kukaa, Rodgers aliendelea na mahojiano akifuata mtiririko wa maswali yaliyokuwa yameandaliwa tayari. Na baada ya kuwa amemaliza maswali ambayo Ed aliyajibu vyema na kufanya kila mara baada ya majibu makofi mengi kupigwa.

"Hebu tuangalie love life yako Ed" aliendelea Rodgers

Ed alitabasamu maana alimfahamu Rodgers kuwa ni mtu asiyechukua jibu jepesi, hutaka kutibua tibua hadi apate anachokitaka.

"Kuna mtu wa karibu alinidokeza kuwa mwaka huu utamvisha mtu pete, nini kilichokuvutia kwa huyu mwanamke tusiyemfahamu bado"

Ed alitabasamu na kuvuta ndevu zake fupi kidevuni kisha alijibu

"Rodgers, macho ya mwanaume huvutiwa na vitu vizuri hasa tunapoongelea jinsi ya kike, hata mimi nilivutwa katika uzuri huo huo, lakini namjua ni binti mwenye kujituma, hivyo naamini tuna sehemu tutafika pamoja"

Baada ya makofi, Rodgers aliendelea,

"Ni mzuri umetuambia, na anajituma, vipi kuhusu pesa zako hazina mchango wowote katika kumvutia yeye kuja kwako"

Ed alisita kujibu lakini hakuonesha usoni, hili swali kuna namna lilimpa mawazo, akaachia tabasamu na kujibu,

"Siwezi jua nia ya moyo wake, kama ni pesa au ni mimi, nitafahamu pale nitakapoishi nae. Siogopi maana kila siku watu wengi wananizunguka siwezi jua nia ya kila mtu, wengine nawagundua mapema na wengine nachelewa. Inawezekana hata wewe Rodgers unaweza kuwa mmoja wa wanaonitumia sababu ya pesa au la. Nitapojua nitakuwa na maamuzi ya kufanya, kwa sasa niseme tu tunapendana"

Rodgers alitabasamu na kusema,

"I wish you all the best Senior bachelor, ila kweli natamani huyo mwanamke akupe kufurahia maisha ya ndoa, huwezi jua nikikuona na raha naweza badili uamuzi nami nikaoa"

Watu walicheka na kupiga makofi tena. Baada ya Rodgers kumaliza maswali ilikuwa zamu ya waalikwa jukwaani kuuliza maswali yao katika sehemu ya mwisho ya kipindi. Nafasi ilikuwa kwa maswali matano ambayo Ed mwenyewe atashika kipaza sauti na kumkabidhi aliyependa amuulize. Ed alikabidhiwa kipaza sauti na kuanza kushuka ngazi kuelekea jukwaa. Wakati huo kamera ziliondolewa kwa Rodgers na kumwelekea Ed.

Mtu wa kwanza alikuwa ni kijana wa kiume ambaye alimuuliza Ed ni kwa namna gani anashiriki kuwasaidia vijana wengine katika kuendeleza ndoto zao. Ed alijibu vyema kwa kuonesha fursa za ajira wanazotoa lakini pia watu wanaowawezesha katika masomo yao.

Mtu wa pili akamuuliza kuhusu afya za watu wanaokaa maeneo ya migodi inayomilikiwa na kampuni yake kutokana na matumizi ya kemikali. Ed alionesha kwa kiasi gani wametenga maeneo yao ya machimbo mbali na makazi ya watu, lakini aliwahakikishia kuwa wanafuata taratibu za kimazingira.

Watu wengi walinyoosha mikono na ilikuwa ni kazi ya Ed kuchagua nani aulize. Maswali yalitakiwa matano tu kutoka kwa watu watano.

Baada ya mtu wa tatu kuuliza swali la mchango katika vipaji vya michezo, Ed alimhakikishia watafanya utafiti kuona kwa namna gani Simunge Group of Companies itaweza saidia eneo la michezo pia.

Wakati anageuka alimuona binti mmoja aliyenyoosha mkono huku ameinama chini kana kwamba alikuwa akiomba apate nafasi ya kuuliza. Ed alisogea hadi alipokuwa na kumshtua kwa kumgusa bega ili kumpa kipaza sauti, yule binti alishtuka na kuinua macho ambapo macho yake yalikutana moja kwa moja na ya Ed. Akaona aibu na kuyakwepesha ya kwake, alishusha mkono akaanza kutetemeka.

"Hey zamu yako, niulize swali si umenyoosha mkono?" Ed alimwambia kwa sauti ya chini huku ameinama kidogo

"Aaah, ooh asante!" Alijibu na kuinuka huku akiwa akiinama vile vile, akapokea kipaza sauti.

Kwa kawaida, unapouliza swali kwenye kipengele hiki unapaswa kumuangalia unayemuuliza, binti huyu alipata shida kukutanisha macho yake na Ed na alionekana kutetemeka hata aliposhika kipaza sauti. Ed kwa kuwa muungwana alimshika mkono mmoja ili kumpa hakikisho la kwamba anaweza kumuuliza. Kitendo hiki kiliwafanya wenye kamera kuvuta hadi kwenye mkono wa Ed uliomshika yule dada. Huku akimuangalia Ed kifuani na si machoni akaanza kuongea kwa sauti ya chini

"Naitwa Aretha, ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho, Capital University, swali langu aamh.. ni kuwa je una furaha na maisha uliyonayo sasa? Hujawahi kutamani uwe mtu wa kawaida tu unayeishi pasipo kufuatiliwa katika maamuzi yako?"

Alipomaliza kuuliza alibaki ameshika kile kipaza sauti na mara akainua macho kumwangalia Ed machoni yaliyobeba hisia za kujali. Lakini hakuendelea sana akayarudisha tena macho chini

Ed alijikuta akivutiwa na muonekano wazi wa hisia za huyu dada ambazo ungezisoma usoni ungezipa neno moja tu "concerned".

Alichukua kipaza sauti huku akibaki ameshika mkono wa huyu dada na kumjibu

"Aretha, nina furaha, japokuwa furaha hii hupata mashambulizi ya hofu, wasi wasi na wakati mwingine uoga. Lakini nina familia yangu inaninyeshea upendo na kunifanya nisahau umaarufu wangu na kujiona mtu wa kawaida ninapokuwa nao. Pia sipendi kufuatiliwa lakini siwezi zuia watu kunifuatilia. Natamani wakati mwingine niwe mahali watu wasiponifahamu kabisa. Napenda wepesi katika maisha"

Alipomaliza kujibu aliachia mkono wa Aretha, wakati huo hadhira ilipiga makofi mengi sana. Alipogeuka kuondoka huyu dada alimgusa begani na kumfanya Ed kugeuka tena na kumwangalia kujua anataka kumwambia nini

"Huwa unapata muda kufanya utani na wengine au kufanya mambo madogo yakuchekesha?" Aliuliza swali hili pasipo kipaza sauti na kumfanya Ed kumsogelea karibu ili kusikia, ambapo alirudia swali kwa sauti ya chini. Ed alisikia na kumwangalia tena usoni kisha akapiga hatua chache na kusimama.

Watu wengine walianza kunong'ona huku wakinyoosha mikono maana sasa nafasi ilibaki moja tu.

Ed alitabasamu na kumwangalia huyu dada kisha akasema,

"Maswali manne nimeulizwa tayari ila Aretha ameuliza swali la pili na kufanya kuyafanya yawe matano, je ni sawa nijibu hili swali la mwisho la Aretha?

Watu walianza kuguna na kulalamika, kitendo kilichomfanya Aretha kukaa na kuinama kwa aibu. Ed akanyoosha mkono kuwanyamazisha kisha akasema

"Basi msiwe unfair sana kwa hili, mtu wa tano na aniulize swali, lakini si sawa kutomjibu Aretha, naomba nimpe nafasi ya kumjibu nje ya jukwaa hili. Loy uko wapi?"

Baada ya Loy kusimama, Ed akaendelea.

"Loy muone huyu dada ili kupata nafasi ya kujibu swali lake... Haya ngoja nichague mtu wa tano"

Mtu wa tano alitoa ombi kwa Ed kuhusu kuweka mashindano ya wazo la mradi litakalowezeshwa na SGCC. Ed alikubali na akawaahidi watalifanyia kazi mapema na kutoa mrejesho wa mambo yatakavyokuwa.

Watu walipiga makofi na kuinuka maana baada ya hapo Ed alikuwa anatoka kabisa mle ukumbini sawa na utaratibu wa muongozaji.

Alipofika jukwaa la nyuma, alipokelewa na Allan aliyesimama na meneja wa matangazo. Walimpongeza na kumuelekeza katika ukumbi wa mapumziko kwa wageni. Wakiwa wameketi pale na Allan waliletewa juisi na vitafunwa kama sehemu ya mkono wa shukrani.

"Allan fuatilia tupate kipindi chote kwenye flash nikitunze kwenye maktaba yangu"

Alizungumza Ed.

"Sawa kaka bila shaka. Lile wazo la mwisho ninaona linaweza kutekelezeka, au unasemaje?" Aliuliza Allan

"Sawa, liangalie namna ya kulizalisha, check na watu wa masoko wanaweza kutusaidia zaidi."

Kimya kifupi kilipita kati yao hadi alipoingia Mkurugenzi wa MBC, aliwasalimia, na kukaa kwenye sofa huku wakiendelea na mazungumzo ya hapa na pale kuhusu mambo ya biashara. Dakika 15 zilipoisha walisimama na kuaga kuelekea nje. Baada ya kufika walipoegesha magari walimkuta Loy amekaa pembeni akiongea na mlinzi aliyempa kiti na yeye kubaki amesimama. Alipowaona aliinuka na kumshukuru mlinzi na kuelekea aliposimama Ed.

"Boss, nimeshachukua taarifa za yule dada. Nimempa appointment ya Jumatatu mchana" alisema Loy

"Oooh, asante Loy.. ana aibu sana, ulimuona Allan" akamgeukia Allan.

"Nimemuona lakini swali lake ni kama vile lilikuwa na mwendelezo" alijibu Allan

"Mmmm!" Aliguna Ed kisha akaendelea

"maswali yake ni kama ya mama anayemuuliza mtoto wake, lakini nimeyafurahia. Nitamjibu hilo la pili."

Alijibu Ed na kisha akawa amezama katika mawazo.

"Hey Ed unasemeshwa na Loy" Allan akamshtua kutoka kwenye mawazo

"Ahm. .. Boss, muda wangu wa kazi umeisha naondoka" alisema Loy

"Oooh sawa Loy, ila kesho utakuja kwenye Dinner Banquet iliyoandaliwa na Waziri. Allan atakupitia"

"Sawa boss." Aliitikia Loy, Allan alimuashiria aingie kwenye gari ili ampeleke.

"Allan, drive safely, tuonane kesho, ila sio asubuhi. Tupumzike, tutaresume Jumatatu.."

"Ooh sawa bro, let's rest" aliitikia Allan na kuingia kwenye gari tayari kuondoka.

Ed aliingia kwenye gari na kukaa, aliangalia mikono yake akikumbuka kitendo alichokifanya kumshika Aretha mkono. Akatabasamu alipofikiria macho yake na namna alivyoona aibu kumuangalia. Hakujua ni muda gani alisema

"Aretha"

Akashusha pumzi na kuondoa gari tayari kuelekea nyumbani ikiwa ni majira ya saa kumi na mbili jioni.

**********************************

Kwenye gari Allan aliendelea kupiga stori na Loy..

"Hivi Allan, nini kilitokea mpaka boss akamshika mkono huyu Aretha....anamfahamu?

"Loy, unataka tumtete boss wako eeeh?" Alijibu Allan na kumtupia jicho la kumhukumu

"Aaah kidogo tu, lakini hatumteti tunaongea kilichoendelea, au tunakosea?" Akaendelea kulalamika Loy

"Kaka Allan jamani kwani huu ni umbea?, tunaangalia tu kile kilichotokea kwenye show"

"He he he mbona uongelei mengine kama wazo la yule dada wa mwisho kuhusu kuweka shindano la mradi...Loy alichoona ni mkono wa boss wake na Aretha eeh"

"Eeewh Allan, wenye kamera wenyewe walizoom tukaona hadi kwenye screen. Halafu boss alivyomuangalia mhh hata mimi haniangalii hivyo"

'Unatafuta shida wewe.... ngoja tumuulize mwenyewe nipe simu yako"

"Ooh no niache Allan, nitamwambia nini alivyo serious.... ila alivyomshika nikatamani ningekuwa mimi?" Alisema Loy huku akifumba macho kuvuta hisia. .

"Eh he he wewe acha kuota, kila siku uko nae muombe mikono yake uishike yote mphweee!"

"Sssh! Unaniharibia mawazo yangu." Alisema Loy

"Tumefika Loy, toka kwenye gari yangu, unaipa nuksi na ndoto zako". Allan alimshtua na kuegesha gari karibu na nyumba aliyoishi Loy.

"Ooh Allan, asante wala usijali sina ndoto yoyote ni vile sijawahi muona boss so lovely kama leo"

"Mmmhh... mbona yuko hivyo hivyo hata akiwa na Joselyn" alijibu Allan

"He He he yaani umemrejea Lyn basi hata wewe umeona tofauti"

"Hey hebu shuka unanifundisha umbea" alisema Allan na kumsukuma kidogo kwenye bega Loy ambaye aligeuka na kuweka mikono yake pamoja

"Haya boss wangu. Asante kunileta, kesho unishtue mapema kabla ya kuja, nitashukuru" alitoka kwenye gari

"Usijali, wewe bila kukwambia mapema tutachelewa.. jiandae kuanzia saa kumi na moja"

"Sawa Allan"

Baada ya Loy kushuka, Allan alimwangalia mpaka alipoingia getini ndipo akaondoka huku akijisemea

"Boss so lovely ha ha ha"

Simu yake iliita na kumshtua toka kwenye mawazo, alipokea kwa bluetooth earphone na kuongea,

"Hello" upande wa pili uliitika

Allan aliijua sauti kuwa ni ya Linus

"Niambie comrade"

"Vipi una nafasi uje mitaa yangu huku" aliuliza Linus

" Hey tukutane Mocca Food hapo nina njaa hata siwezi kukusikiliza" alijibu Allan

"Okay, tuonane hapo ukifika niambie nishuke"

"Sawa comrade" alijibu na kukata simu, sasa alibadili mwelekeo ili kukutana na Linus kwenye mgahawa ulikuwa karibu na ofisini kwake kwenye Exchange Tower.

Baada ya dakika 20 alikuwa tayari kwenye mgahawa wa Mocca akiagiza chakula huku akimsubiri Linus ambaye alijiunga nae muda mfupi baadae. Chakula kilipomalizika waliendelea na maongezi huku Linus akimsimulia tukio la asubuhi lililotokea kati yao na Ed.

"Sasa comrade, nimejaribu kumchunguza Martinez, si mwepesi kama unavyodhani" Allan alimwambia Linus, akaendelea

"Nina uhakika ana agenda yake na bila shaka amejipanga vyema, sema sijapata eneo la udhaifu wake. Nina wasi wasi na delay tunazozipata kwenye kemikali ni kama kuna mtu anajaribu kutuzuia.. kuna wakati nahisi ni yeye ila sina uthibitisho." Alieleza Allan

Linus akakuna kichwa chake na kusema

"Kupata udhaifu wa Martinez inaweza ikachukua muda lakini bro alishaapa atamvisha pete mwanamke atakayemuoa wiki tatu kuanzia sasa. Joselyn ni mbweha, atatufarakanisha na bro, please Allan tutafute kitu cha kusitisha maamuzi ya bro"

"Duh!" Allan aliguna na kuchukua glasi ya maji na kunywa

"Nakwambia comrade, ninahitaji mtu, kitu au wazo litakalombadilisha bro kuona yule mwanamke ni bomu litakalolipukia familia hii. Derrick amefadhaika sana, sitaki mambo haya kwenye familia yetu " aliendelea Linus

Allan alikuna kidevu chake na kumuangalia Linus akashusha pumzi nzito

"Mmh... leo bro kafanya kitu ambacho mimi binafsi sikudhani kama angekifanya, kuna dada mmoja ambaye alimuuliza swali, kwa namna namfahamu Ed lile jicho lilikuwa na hisia naweza sema ni jicho ambalo Ed humuangalia mama pekee."

Macho ya Linus yaling'aa ghafla na tabasamu jepesi likaonekana usoni kwake,

"Tell me the goodnews comrade" alimwambia Allan

"He he sina uhakika lakini Loy ameuliza kama wanafahamiana anasema hajawahi muona Ed so lovely kama leo"

"Yuko wapi huyo dada comrade... nimtafute kabisa anaweza kuwa mwokozi" aliuliza Linus kwa shauku

"Comrade, acha kuharakisha mambo, hebu subiri kwanza maana ana appointment na bro jumatatu kama atakuja basi tutapata starting point" alitahadharisha Allan

"Comrade am about to celebrate, hii ni good news balaa... mbona hukunishtua niangalie hiyo show?" Alizungumza Linus kwa uso uliojaa matumaini..

"He he he usingeangalia najua ila usijali kesho nitafuatilia kilichorekodiwa ila kwa muda wako tafuta You Tube sijui kama wana akaunti"

"Safi comrade... nahitaji kuona ule uso wa bro... nadhani Brian atatusaidia tumshirikishe, yeye ni rafiki wa karibu sana wa big bro halafu ameshaoa"

"Sawa, ila kama hakuna mafanikio hapo itabidi tutafute njia nyingine au tumwekee tail Joselyn" aliongeza Allan

"Kama alivyo baba yake, Joselyn ni mjanja sana. Let's plan our move. Sitapumzika ikibidi nimuumize bro lakini asioe huyu mwanamke" alisisitiza Linus

Baada ya mazungumzo waliagana ikiwa ni saa nne usiku. Allan aliishi katika Heaven apartment mwendo wa dakika 15 kutoka Exchange Tower.

Linus alifika nyumbani majira ya saa tano kasoro usiku. Alielekea ndani na alipofika aligundua Ed amesharudi nyumbani, lakini hakumkuta sebuleni akaelekea chumbani kwake ili amsalimu, baada ya kugonga bila majibu akahisi ameshalala.

Linus akaondoka kuelekea chumbani kwake. Baada ya kutoka bafuni alivalia nguo za kulalia na akajitupia kitandani huku akigusa simu yake. Akaingia You Tube na kutafuta akaunti ya Rising Star baada ya kuangalia aliona mahojiano ya Ed ambayo yalikuwa yamewekwa muda mfupi uliopita. Macho ya Linus yaling'aa na kumfanya ainuke na kuwasha taa ya pembeni ya meza na kuanza kufuatilia hatua kwa hatua.

Ilipita dakika 30 bado ile sehemu ya Aretha haijafika, akaamua kuvumilia maana muda sasa ulielekea saa saba usiku. Mara uso wa Linus ukabadilika na akawa makini akiangalia kipande cha Ed na Aretha. Alipomaliza aliingia kwenye namba na kumpigia Allan ambaye muda huu alikuwa ameshalala.. na simu yake ilizimwa. Linus akaamua na yeye kulala lakini furaha yake haikuweza fichika huku akiita "Aretha"

**************************************