Jumatatu hii Ed aliingia ofisini kwake mapema kabla ya mfanyakazi yoyote kufika. Alikaa kwenye kiti chake huku vidole vyake vikigusa kompyuta yake na kuufanya uso wake kuonesha alikuwa akifanya kitu chenye kuhitaji umakini mkubwa sana.
Loy alipofika hakugundua kuwa bosi wake alikuwa tayari ndani ya ofisi. Alichelewa dakika tano, aliposhuka kwenye lifti alikimbia kuelekea upande wa ofisi huku akitoa funguo kufungua mlango uliomruhusu kuingia sehemu ilipo ofisi yake ya CEO na Meneja Oparesheni. Aliambulia mshangao maana mlango ulikuwa ushafunguliwa. Mapigo ya moyo yakaongezeka, akaingia na kuelekea kwenye sehemu ya meza yake. Akajiweka sawa na kuchukua diary ili kuangalia ratiba za leo, lakini alishtuliwa na simu iliyopigwa maana alijua ilitokea ofisini kwa CEO
"Habari ya asubuhi boss?" Alisalimia huku akiweka sawa blauzi yake
"Umechelewa Loy" ilikuwa sauti ya Ed aliyeongea kwa taratibu kuonesha kukerwa
"Nisamehe boss, nilipitiwa na usingizi" alijitetea Loy huku akifumba macho
"Nitumie muhtasari wa kikao, sijauona" aliongea Ed.
"Ooh sawa, nautuma sasa hivi, boss kahawa?" Aliuliza Loy
"Ninayo, nitumie kisha uje" alijibu Ed
"Done sir, " alijibu Loy na kurudisha simu maana Ed alikuwa kashakata.
Loy alikaa kwenye kompyuta yake na kutuma muhtasari, baada ya hapo akaangalia diary yake na kisha akainuka kuelekea ofisini kwa Ed.
Baada ya kuingia Loy alisogea mezani kwa Ed na kusimama.
"Mmmmmh" alishusha pumzi Ed pasipo kumuangalia Loy, akaendelea na kazi kwenye laptop yake
Loy alifungua diary na kuanza kumsomea ratiba Ed ambaye hakuinua hata jicho kumuangalia.
"Mr Hussein kutoka Rocky Tires atakuwa hapa saa tano na baada ya Lunch utakuwa unakutana na Aretha na saa 10 unatakiwa kule Peace House kwa ajili ya kupokea misaada ya watoto kituoni"
Ed aliinua macho na kumwangalia Loy aliyemsomea ratiba yake ya kazi. Loy alipomaliza, akaacha kuigusa kompyuta kisha akaegama kwenye kiti chake
"Kwa nini uliweka appointment ya Aretha baada ya Lunch hour?" Aliuliza huku akimkazia macho Loy ambaye alijitahidi kuyakwepa kwa kuangalia pembeni
"Aah niliona baada ya lunch kuna muda mrefu uko wazi boss" alijibu Loy huku akiyazungusha macho kwingine ilimradi yasikutane na yale ya Ed.
"Mmmm, okay, wasiliana nae kujua atakuja au la" alisema Ed na kurudisha mikono yake kwenye laptop
"Aa.. Sawa boss, kitu kingine unahitaji labda? Aliuliza Loy
"Nope" akajibu Ed
Loy akatoka haraka na kuelekea kwenye meza yake. Akashusha pumzi kwa nguvu na kuchukua simu yake kisha akapiga namba ya Aretha ambayo aliichukua baada ya show.
Simu iliita kwa muda bila kupokekelewa,
"ashhhh pokea Aretha uniokoe maana sijui nitasema nini" alijisemea kwa sauti Loy, na mara mlango ukafunguliwa Allan akaingia
"Habari ya asubuhi Loy" akamsalimia
"Salama boss, karibu." Alijibu na kuendelea kuweka simu sikioni ambayo bado iliita bila mafanikio
"Eeewhhh, huyu Aretha anataka niache kazi jamani"alisema Loy na kumfanya Allan aliyekuwa akimimina kahawa kugeuka
"Aretha amefanyaje tena Loy?" Akamuuliza
"Shhh Allan boss atasikia... hapokei simu"alijibu Loy. Allan akamsogelea na kutikisa kichwa
"Tsk tsk. .. Loy unamsumbua mwanafunzi labda yuko darasani" Allan akajibu huku akiachia tabasamu la dhihaka
"Eti eeeh, itakuwa hivyo ngoja nimpigie baadae kidogo"alijibu Loy na kuweka simu pembeni
"Vipi kwani mbona mapema wamtafuta?"aliuliza Allan
"Shhhh unaongea kwa sauti Allan... boss ametaka nimuulize kama anakuja au la"
"Ooooh, basi sawa"
Allan alicheka na kuingia ofisi yake iliyokuwa upande wa kulia na kumuacha Loy akiendelea na shughuli zake.
*****************************
"Goodmorning Comrade" Allan alisalimia kwenye simu baada ya kuwa amekaa kwenye kiti ofisini kwake.
"Nina good news, vipi ukija Ashanti leo mchana, mwokozi wako anaweza kuwa hapa" aliongea Allan akiachia tabasamu
"Okay, basi tafuta namna ila bro asijue hapendi kufuatiliwa si unamjua" aliendelea kuongea na upande wa pili.
"Basi sawa. See you then" alimaliza Allan na kukata simu kisha akacheka na kusema "Bro let's wait for her"
******************