Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 14 - NATAKA NIMFAHAMU

Chapter 14 - NATAKA NIMFAHAMU

"Usijitaabishe sana Comrade, acha tumwamini bro, kama atakuwa na hisia tofauti kwa Aretha hatokubali kuziacha japokuwa he is a man of his word." Alimtia moyo Li

"Exactly, hilo ndilo linanikatisha tamaa, a man of his word, na ameshaahidi kumvisha pete Lyn, atakubali kuyapinga maamuzi yake mwenyewe?" Aliuliza Li huku akiegama tena kwenye kochi..

Allan akanyamaza akimwangalia rafiki yake ambaye alijua kwa hakika anaumia kwa yale ambayo Joselyn anayafanya. Hakujua kwa nini ila alihofia familia yake kupata maumivu kwa mbinu chafu alizozitumia Joselyn.

Baada ya muda walisikia mlango ukifunguliwa, sauti ya Aretha na Ed zilisikika kwa mbali na kumfanya Linus kuinuka kuelekea mlangoni lakini kabla hajafika Allan alimshtua

"Comrade usiende, kumbuka bro atakushtukia kama utatokea tena baada ya mazungumzo yake na Aretha kuisha."

Li alisimama na kufikiri alichosema Allan, akakubalina na ukweli huo akageuka kumuangalia Allan kisha akasema,

"Nataka nimjue kwa sehemu huyu Aretha, nitamfuatilia, muda ule nimepata dakika chache za kumsalimia kabla hajaenda ofisini kwa bro....she is so pure I can tell"

"Unataka umfuatilie ujue anapoishi au kuna kingine tuwahusishe "4D"?" Allan aliuliza

4Diameters ni kikundi cha siri cha SGC ambao kazi yao ni kufuatilia taarifa zisizoweza kupatikana kirahisi. Watu hawa wanne ni wataalam wa kompyuta, SGC huwatumia hasa wanapotaka kuhusiana kibiashara na mtu au kampuni. Wanaweza kuingia sehemu pasipo kujulikana kwa kutumia utaalamu wao wa kompyuta na wakapata taarifa za siri.

"No.... hao watamwambia Ed bila shaka comrade... nitamfuatilia mwenyewe" alisema Li

"Oooh okay"Allan akajibu kisha akabonyeza kitufe kwenye simu na sekunde chache Loy alisikika

"Hey Loy, inua mkonga wa simu nataka kukuuliza kitu" Allan alimwambia Loy kwa sauti ya chini

"Okay vizuri, vipi bro katoka na mgeni wake" aliuliza taratibu huku akimwangalia Li

"Hapana, amerudi ofisini" alijibu Loy.

"Basi sawa" alimaliza na kukata simu huku akiachia tabasamu dogo la kijanja

Li alikuwa makini akisubiri kile atakachosema Allan

"Bro hajamsindikiza, ila atashuka chini maana anaelekea Peace House jioni hii"

"Great" alisema kwa furaha Li huku akichukua funguo za gari alizozitupia mezani

"Ngoja niwahi naweza kutana nae hapo kituoni" Li alimwambia Allan akiwa na haraka tayari kutoka.

Alipofungua mlango kutoka, alishangaa maana Ed naye alikuwa mlangoni tayari akiwa na funguo mkononi kuonesha alikuwa akitoka.

Ed alimuangalia Li kwa uso wa maswali,

"Vipi mmemaliza?" Swali hili lilimfanya Li aangalie mlango wa kutokea kisha akarudisha macho kwa kaka yake.

"Yes, tumemaliza na nakimbia E Towel mara moja" alijibu Li na kuanza kuelekea mlangoni huku akiomba Ed asimuite tena.

"Okay" alijibu kwa ufupi Ed na akaelekea kwenye dawati la Loy. Li akachukua nafasi hiyo kutoka kwa hatua za haraka akiingia kwenye lifti huku akiomba amkute Aretha kituoni.

Ed alimpa maagizo mafupi Loy, akatoka naye katika haraka kidogo ili kuhakikisha Li hatomfuatilia maana alikusudia kuangalia uwezekano wa kumchukua Aretha kabla hajaelekea Peace House.

***********************

Li aliendelea kuendesha taratibu huku akiangaza huku na kule walau amuone Aretha lakini mpaka alipofika kituoni hakuwa amefanikiwa kumuona.

Akaegesha pembeni akaangaza kati ya kundi la watu waliosimama kituoni hakumuona Aretha duh! Akachoka na kushusha pumzi akifikiri ni kwa kiasi gani alipoteza bahati ya kumfahamu huyu binti. Taratibu akaanza kuondoa gari huku akijitia moyo kuwa bado atapata nafasi ili mradi anajua pa kumpata, Capital University.

Wakati anawaza hayo upande mwingine pembezoni mwa kona moja iliegeshwa SUV nyeusi. Ed alibaki akitazama gari ya mdogo wake huku kichwani maswali yakianza kutiririka.

Je Li anamfahamu Aretha au wana mahusiano?

Kwa nini yuko hapa?

Au amegundua tofauti yake kwa Aretha?

Ed alikuna kidevu chake taratibu na kuamua kuondoa gari kuelekea Peace House baada ya kumuona Li akiondoka eneo lile.

Ndani yake alikuwa amejaa shauku ya kuonana na Aretha tena.

Akiwa njiani simu yake iliita kumfanya kushtuka, Joselyn alimpigia.

*********