Aretha baada ya kushuka kwenye lifti akitokea ofisini kwa Ed, alielekea kwenye mlango mkubwa wa kutokea, akiwa amebeba mfuko wake. Huku akiwa ameweka "earphone masikioni mwake alionesha kuburudishwa na alichokuwa akisikiliza
Ghafla mtu alimgonga kwa nyuma kwa bahati mbaya, na kusababisha mfuko wake kuanguka kwa mbele huku makaratasi yaliyokuwa mkononi mwa yule mtu yakizagaa mahali pale
"Ooooh samahani sana" alisema yule mwanaume ambaye alionekana kuwa kijana bado
"Hamna shida"alisema Aretha na kugeuka kumuangalia usoni aliyemsemesha kisha akaangalia karatasi zilizoanguka chini. Akainama haraka kuokota akimsaidia yule kaka ambaye nae alikuwa ameanza kuzikusanya.
Baada ya kumaliza, yule kaka alimkabidhi mfuko kisha akasema
"Samahani sana nilikuwa naangalia karatasi na sikukuona mbele."
"Usijali, hata mimi nilikuwa na earphone sikusikia hatua zako nyuma yangu" alijibu Aretha kama kawaida usoni akionesha aibu kumuangalia usoni yule kaka.
"Naitwa Derrick, mwenzangu?" alinyoosha mkono kumuelekea Aretha ambaye aliuangalia kwa dakika kisha akafanya kama alichofanya.
"Aretha"
Derrick alimwangalia na kutabasamu kisha akaendelea
"Unaelekea wapi nikusogeze kwa usumbufu mdogo niliokupa" akaongeza na tabasamu lake ambalo humfanya mtu ashindwe kukataa.
Aretha alimwangalia usoni mara moja na kushusha macho yake akitabasamu,
"Naenda Moon Street" alijibu kwa sauti ya chini
"Great twende sasa" alijibu Derrick na kwa haraka akachukua mfuko mkononi kwa Aretha akaanza kuelekea alipoegesha pikipiki yake.
Aretha alimfuata kwa nyuma huku akikubaliana moyoni mwake kuwa huyu kaka ana sura mzuri na ni mtanashati. Bado alifurahia kitendo chake cha kiungwana cha kuomba msamaha.
Walipofika kwenye pikipiki, Derrick alitoa kofia ya ziada akampa Aretha.
"Oooh asante" alisema Aretha.
Derrick akaweka karatasi zake kwenye begi dogo aliloliacha kwenye pikipiki yake na ule mfuko akauweka pembeni kwenye mshikio wa pikipiki. Akapanda na kuwasha pikipiki akimpa ishara Aretha kupanda.
Aretha alitabasamu kwa aibu na kupanda huku akijitahidi asigusane na mgongo wa Derrick.
Wakaondoka huku Derrick akiachia tabasamu lake la ushindi kwa hatua hiyo. Aretha hakujua kuwa ile haikuwa ajali bali ni kitendo kilichopangwa makusudi na Derrick ambaye alitaka kuwa karibu naye.
*************************
Derrick alikusudia tangu alipoona kile kipindi cha Ed kumtafuta Aretha. Alijua Linus kaka yake aliona na atakuwa na hatua zile zile kama zake, kutaka kumfahamu Aretha.
Hakunua nini kingetokea baada ya kumpigia Loy Jumatatu asubuhi kumuuliza ratiba ya kaka yake ili aweze kuonana nae. Aliamka akiwa amekusudia kumaliza lile lililotokea kati yake na kaka yake. Aliamua kumwambia ukweli Ed. Mazungumzo yao yalikuwa hivi..
********************
Loy aliingia kwenye gari la ofisi lilomfuata nyumbani kwake kama kawaida kila asubuhi. Jumatatu hii alijua ana mengi ya kufanya. Aliendelea kupitia diary yake akirekebisha hapa na pale.
Walipokaribia jengo la ofisi, simu yake iliita na kwenye kioo paliandikwa 'HB Derrick'
Loy alipokea
'Hello Handsome' alisalimu Loy
"Hey Loy, mambo vipi" alijibu Derrick kwa sauti ya uchovu
"Safi, mbona uko down?" Aliuliza Loy maana alimjua Derrick ni mchangamfu wakati wote.
"Niko pouwa tu Loy, ndio naamka" alijibu Derrick kumuondolea Loy wasi wasi kisha akaendelea
"Vipi ratiba ya bro mchana, nataka nije hapo" alinyamaza kusubiri majibu ya Loy
"Oooh Derrick, mchana ana mkutano na Aretha sasa sijui atamaliza mapema au la. Nitajaribu kuangalia kama ratiba itaruhusu" Loy hakuona shida kusema hivyo maana alijua Derrick atakuwa aliona kipindi asijue Derrick hakuwa na taarifa yoyote kuhusu Aretha na hivyo kumfanya aulize
"Aretha ni nani Loyce?"
Loy aliposikia Derrick kamuita jina lake lote akajua hajui chochote na aliuliza kwa u-serious zaidi
"Hukuona kipindi cha MBC?" Aliuliza kwa mshangao..
"Hapana Loyce, niambie"
"Okay nenda You Tube angalia Rising Star utamuona huyo Aretha" alijibu Loy ambaye hakutaka kuelezea maana alikuwa na dereva wa kampuni. Haikuwa sawa kwake kujadili mambo ya boss wake.