Ed aliinuka tayari kumtoa mgeni, lakini akakumbuka ule mfuko uliokuja na biskuti
"Aretha subiri" Ed akamshika mkono Aretha aliyekuwa amepiga hatua mbele yake na kumfanya ageuke nyuma.. Kitendo kile ni kama kiliamsha hisia za Ed na kukumbuka siku tatu nyuma.
Wakati huu Aretha alibaki amesimama akiuangalia mkono wa Ed uliomshika na hakujua namna gani angepata kuelewa kile alichohisi mwilini mwake.
Ed hakujua ni sekunde ngapi zilipita akiwa ameushika ule mkono wa Aretha mpaka aliposikia sauti yake ikimsemesha
"Umeniita Edrian"
"Oooh yes.. " alishtuka na kuuachia mkono wa Aretha. Akarudi nyuma na kuchukua mfuko mweupe wenye boksi la biskuti na kumkabidhi
"Kamalizie na hii hapa"
Aretha alipokea na kushukuru huku akiangalia ndani ya mfuko na kufanya tabasamu kuonekana usoni kwake lakini likayeyuka ghafla, akamwangalia Ed
"Mbona umenipa zote? Na wewe je?" Aliuliza Aretha
Ed akamwangalia Aretha kwa hisia za ajabu kisha akaendelea
"Worry not, huwa sipendi vitu vya sukari nyingi" alijibu
"Oooh.... sawa. Asante sana" lilikuwa jibu la Aretha
Ed akatangulia ili kumfungulia mlango mgeni wake, lakini mkono uliposhika kitasa akakumbuka, akaingiza mkono mfukoni kutoa pochi yake ambapo alitoa business card yake na kumpa Aretha kisha akasema
"Utanijulisha ukiwa tayari nione picha unazochora"
Akapokea ile kadi, na kushukuru kisha akaiweka kwenye begi lake.
"Unaelekea wapi kwa sasa, naweza kukusogeza maana nina ratiba ya kutoka" aliuliza Ed ambaye wakati huu alijaribu kutafuta namna ya kumuomba namba yake ya simu lakini alihisi ataonekana vibaya mbele ya binti huyu.
Aretha aliwahi kujibu
"No...no no usijali nitaenda tu mwenyewe, naenda nyumbani, hata hivyo kutoka hapa sio mbali na kituo cha basi"
"Basi sawa." akajibu Ed kinyonge, akafungua mlango na Aretha akatoka.
Wakati huo Ed aliangalia kwenye mlango wa Allan ili asije kutana na mdogo wake... Akachukua hatua kumtoa Aretha ambaye alielekea kwa Loy kumshukuru.
Ed akabaki akimsindikiza kwa macho wakati akifungua mlango na kutoka huku akimpungia mkono.
Macho ya Loy yalikuwa kwa bosi wake, akishangaa tabasamu lake ambalo lilikuwa wazo usoni pake. Kwa kawaida Ed huwa na tabasamu hilo pale ambapo mradi wake unapofikia upeo wa mafanikio, mbali na hapo ni mara chache kumuona akitabasamu hivi.
Ed aligeuka na kumwangalia Loy ambaye alikwepesha macho na kuyarudisha kwenye kompyuta iliyokuwa mbele yake kuendelea kuchapa barua za ofisi.
****************************
Ofisini kwa Allan...
"Comrade umemuona mwokozi wako?" Aliuliza Allan akamwangalia Linus ambaye alikuwa amekaa kizembe kwenye kochi la mtu mmoja pembeni ya meza
"Ha ha ha nimemuona" alijibu Li kisha akaendelea huku akikaa vyema sasa
"Kinachonipa raha ni muonekano wa bro baada ya kumuona... sijui nini ambacho anakiona kwa huyu binti lakini naweza sema kinamuathiri"
"Heh?" Alishangaa Allan,
Linus akatulia kisha akaendelea,"Na hivyo kinachomuathiri bro, ndio strong point ya Aretha"
"Comrade unawaza nini tena?" Allan aliuliza baada ya kuona hampati vyema Li
"Sikia Allan nachosema ni hiki; Joselyn ni mzuri wa sura kuliko hata Aretha, lakini kwa macho yangu sijawahi muona bro anakosa maneno kwa uwepo wake"
"Mhhhh?" Aliguna Allan kumuashiria aendelee,
"Huyu Aretha ni sawa na sumaku na bro ni chuma, ngoja tuone. Amechukua muda mrefu sijui wanaongea nini?"
"Ha ha ha comrade unasahau patience is the key" alijibu Allan akicheka taratibu
"Haaaa, sawa Comrade, nimempenda yuko so simple ila nahofia Joselyn na baba yake, hawataruhusu amsogelee Ed wakijua nini kinaendelea." Alisema Li huku akitafakari sana
"Usijitaabishe sana Comrade, acha tumwamini bro, kama atakuwa na hisia tofauti kwa Aretha hatokubali kuziacha japokuwa he is a man of his word." Alimtia moyo Li
"Exactly, hilo ndilo linanikatisha tamaa, a man of his word, na ameshaahidi kumvisha pete Lyn, atakubali kuyapinga maamuzi yake mwenyewe?" Aliuliza Li huku akiegama tena kwenye kochi..
Allan akanyamaza akimwangalia rafiki yake ambaye alijua kwa hakika anaumia kwa yale ambayo Joselyn anayafanya. Hakujua kwa nini ila alihofia familia yake kuhusiana na Martinez