Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 6 - PICHA YAKE HAINITOKI I

Chapter 6 - PICHA YAKE HAINITOKI I

Siku ya pili, Jumamosi Linus aliamka saa kumi na mbili za asubuhi tayari kuelekea kwenye chumba maalum cha mazoezi. Alimkuta Ed ambaye alikuwa kwenye mashine ya kukimbia akiwa tayari ametota jasho,

"Hey bro, za asubuhi?"

"Safi Li" alijibu Ed huku alihema, alianza kupunguza spidi ya mashine.

"Jana niligonga sana naona ulilala mapema"

"Oooh pole, nililala mapema kwa uchovu, vipi kuna cha kuongea?" Aliuliza Ed huku akiwa anajifuta jasho

"Hapana bro, nilikucheck tu" alijibu Linus ambaye sasa alikuwa kwenye mashine aliyokuwepo Ed

"Ooh basi sawa, Derrick ameenda kwa mama?"

Linus alitabasamu kwa kujua kuwa bro bado anajali, akamjibu

"Yuko Heaven, usihofu yuko salama, japokuwa yuko down"

"I know, tuache hiyo topic" alijibu Ed na kuonesha alijisikia vibaya.

Waliendelea na mazoezi hadi ilipotimia saa moja walienda kujiandaa tayari kwa ajili ya kifungua kunywa. Walikutana mezani huku Coletha akijiunga nao mezani. Walikula kimya isivyo kuwa kawaida, Ed alijua ni matokeo ya kitendo cha jana. Hakuwahi kufikiri angeweza kufanya alichofanya.

Baada ya kumaliza kifungua kinywa wakaendelea na ratiba zao huku Ed muda mwingi alikuwa chumbani kwake.

Linus naye alikuwa akiwasiliana na Allan ili kupata kile kipindi kwenye flash maana kwenye akaunti ya You Tube kilikuwa kilifungwa hauwezi kukipakua zaidi ya kukiangalia. Na baadae akaongea na Brian kumuomba aweze kuonana nae. Dakika chache baadae alikuwa njiani akielekea kwa Brian ili kuzungumza nae.

Ed aliendelea na kazi zake akiwa chumbani huku akichat na Joselyn akimbembeleza kuvumilia maana jioni hatoweza kuongozana nae japokuwa watakuwa kwenye sherehe hiyo pamoja.

Ed: "Lyn, nielewe, nikiongozana na wewe kwenye red carpet tayari wataanza kuandika na kutufuatilia. Please wait few days, i will announce it. Usiwape nafasi paparazzi watatuvuruga"

Lyn: kama ni hivyo sawa, but I really want to be by your side"

Ed: you will always be by my side Lyn as my wife.

Lyn: 😍thanx babe, naisubiri hiyo pete kwa hamu zote"

Alipomaliza kutuma ujumbe ghafla alijisikia hofu na hisia ya usaliti ikimshika. Aliwaza kwa nini anahisi kama anamsaliti mtu asiyemjua.

Akaamua kuangalia tena kile kipindi huku akijishangaa kwa nini anatamani kuiona sura ya Aretha. Alirudia ile sehemu na kurudia huku akitabasamu.

"What's goin in my heart" alijiuliza maswali kila mara alipojikuta anawaza kuhusu Aretha. Akaamua kutoka kuelekea mjini walau kuona cha kununua ili kuyaweka mawazo mbali na yale yaliyotokea jana. Akaelekea chumbani kwa Coletha na kumuomba aongozane naye.

Waliingia kwenye gari na kuondoka, njiani Ed alikuwa kimya na mara nyingine aliguna tu mwenyewe mpaka alipoamua kuanzisha mazungumzo. Alimfahamu mdogo wake vyema, alijua kimya hiku ni matokeo ya kile alichofanya asubuhi ya jana yake. Coletha ni mchangamfu wakati wote, lakini muda huu alikaa kiti cha nyuma akiendelea kuangalia simu yake.

Ed aliamua kuuvunja ukimya

"Coletha, am sorry, najua umenikasirikia kwa sababu ya Derrick. Nilikasirika baada ya kujua but niamini simchukii Derrick.. natafuta namna ya kulishughulikia hili, sijui nini kilimuingia mdogo wangu"

Coletha alimsikiliza kaka yake kwa utulivu na aliamini kuwa atakuwa pia hajisikii vyema kwa kile kilichotokea.

"Lakini kaka mbona haukumpa nafasi akwambie nini kilitokea?" Coletha alimuuliza Ed

"Mmmh!" Aliguna Ed

Coletha akaendelea, "bro Derrick sio mkorofi kihivyo hata afanye kitu cha namna hiyo, halafu hakuwepo muda mwingi nyumbani naomba usimfanyie hivyo"

Ed alikaza mikono yake kwenye usukani huku akijilaumu kwa nini alikasirika. Lakini ndani alijiuliza mbona Joselyn hajawahi mdanganya kitu chochote toka afahamiane nae. Bado alibaki njia panda, akashusha pumzi na kumwambia Coletha,

"Ikiwa hakufanya au alifanya haitabidili kuwa nilimuumiza Coletha. Nisamehe, nitatafuta namna ya kuongea nae, kwa sasa acha awe huko nitamfuata soon"

Coletha alifurahi kusikia hivyo, akachangamka na kusema, " Sawa bro, hata sisi hatujakukasirikia, ila Joselyn kuwa nae makini"

Ed akacheka "kwa hiyo mdogo wangu amekua sana hata ananipa lecture mimi"

Wakacheka wote,

"Hapana bro, ila penye wengi pana mengi"

"Sawa Coletha hebu tuachane na hii habari, vipi maandalizi ya mitihani ya semister"

Ed aliuliza huku moyo wake ukifurahia walau kuona tabasamu usoni kwa mdogo wake.

"Yako vizuri tu bro, tukimaliza mitihani natamani niende nawe K-Town kama utakuwa na ratiba hiyo"

Kwa nini K-Town na sio G-Town? Aliuliza Ed

"Hahah bro, K-Town nasikia pana sehemu nyingi zenye vivutio, natamani nikapaone"

"Sawa, ila Allan anasimamia operation zote za K-Town, mara nyingi ndio huenda huko. Nitaangalia ratiba zangu"alijibu Ed huku akitabasamu baada ya kumuona mdogo wake akifinya vidole vyake

Waliendelea na mazungumzo hadi walipoingia kwenye Duka kubwa la nguo, ambapo Coletha alichagua nguo ya kuvaa jioni na viatu. Ed aliangalia angalia na hakuchukua chochote. Baada ya kulipa aliamua kumpitisha mdogo wake saluni kutengeneza nywele na akamuacha hapo yeye akaelekea nyumbani. Moyoni alifurahi kujua kuwa bado ndugu zake wanampenda.