Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 4 - KUFURAHIA MAMBO MADOGO I

Chapter 4 - KUFURAHIA MAMBO MADOGO I

Baada ya kumshusha Joselyn kwenye geti la kuingia nyumbani kwao, Ed aliondoa gari kuelekea ofisini huku akiwasiliana na msaidizi wake Allan

"Kuhusu uagizaji wa zile chemical, please consider well huyu muuzaji aliyejitokeza, kabla ya kufika hapo mwambie Loy aprint hizo bidding na atoe copy nisubiri ofisini kwangu nataka kuongea na wewe"

Alimaliza kutoa maelekezo kwa Allan, akaweka simu pembeni na kuendesha gari hadi alipoingia Ashanti Tower mahali ambapo ofisi za Simunge Group of Companies zilikuwapo. Ikiwa pia jengo hilo ni sehemu ya miradi yake binafsi, aliegesha gari kwenye maegesho ya VIP kisha akapanda lift kuelekea ghorofa ya saba ambapo ofisi yake ilikuwa.

Alipoingia alipokelewa na sekretari wake Loyce, wengi humuita Loy.

"Kahawa Loy, umeprint hizo bidding?

"Yes boss, ziko tayari. Kahawa inakuja sasa hivi" alijibu Loy na kuelekea ilipo mashine ya kutengeneza kahawa. Wakati huu Ed aliingia ofisini kwake na kukutana na Allan aliyekuwa akiperuzi faili mkononi mwake.

"Kaka, karibu tena", alisema Allan huku akiinuka na kumpa mkono.

"Asante Allan, vipi shughuli zinaendaje?"

"Vizuri kaka" alijibu Allan

Baada ya salamu, Ed alielekea kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya meza kubwa ya kiofisi. Kabla ya kukaa alisimama na kuangalia mandhari ya nje iliyoonekana kwenye dirisha la kioo nyuma ya kiti chake. Ofisi ya Ed ilikuwa na muonekano wa kuvutia ungeweza kudhani ni sebule ya jumba la kifahari, makochi nadhifu yalijaa upande wa kushoto huku upande wa kulia kulikuwa friji ndogo rangi ya kijivu. Pembeni kulikuwa na kabati la vitabu lililopangwa kwa ustadi. Dari yake ilinakshiwa na rangi ya bluu bahari na kufanya muonekano wake uwe kama unaangalia mawingu.

"Allan, tunahitaji kuboresha mashine za G-Town maana kuna operations zinachelewa kukamilishwa" aliongea taratibu Ed.

"Kabisa kaka, Boric wamenitumia tayari sample ya mashine mpya, nimeforward email, hujaiona?" Aliuliza Allan

"Kama uliituma alfajiri sijaangalia, I had some issues at home"

" Is everything okay Ed?" aliuliza Allan

Kabla ya kujibu swali Ed alimuuliza "Allan, unamuonaje Derrick?"

"Bro, that is a very broad question, what is happening?" Aliuliza Allan maana hakujua namna ya kulijibu

"Nothing much, lakini Allan, Lyn ameniambia jambo ambalo akili yangu inalifikiri sana. But it's okay. Tufanye kazi." Alijibu Ed na kukaa huku akifungua laptop yake.

Mlango uligongwa na Ed aliitikia kumruhusu Loy aingie. Aliingia na tray ya vikombe viwili vya kahawa, baada ya kuweka mezani alichukua diary yake aliyoiweka pembeni na kuifungua.

"Asante Loy" alishukuru Ed. Loy alitabasamu na kuendelea kufungua kurasa za diary yake,

"Boss leo saa tatu una kikao na Idara ya manunuzi pamoja na wahasibu." Loy aliendelea kumsomea Ed ratiba ya Ijumaa ya leo,

"Saa sita unatakiwa The Trust Bank mkutano wako binafsi na meneja."

"Saa tisa unatakiwa Mind Broadcasting co-operation, mgeni katika kipindi cha Rising Star Live Show, hii ndio ratiba ya leo boss."

"Oooh, Asante Loy, jiandae utatangulia kwenye show, angalia maswali yatakayoulizwa nitakukuta huko." Kisha akamgeukia

"Allan unaweza tangulia na Loy ikiwa ratiba zako ziko loose, sipendi kuwa alone na watu wa Tv"

Allan alikubali kuondoka na Loy kwa ajili ya maandalizi ya Live Show. Baada ya maelekezo ya kazi Ed aliendelea na shughuli za kiofisi mpaka muda wa kikao. Kabla ya kuingia kwenye kikao alipokea simu ya mama yake, ilimshtua na kudhani kuwa nduguze watakuwa wamempa mama yake taarifa. Lakini baada ya kumsikiliza akagundua hawakumwambia, akajihisi huzuni kwa kile alichomfanyia mdogo wake hata pasipo kumsikiliza. Akamaliza kuongea na mama yake na kuelekea kwenye kikao.

Ratiba zake zilienda vyema hadi alipoanza safari kuelekea MBC kwa ajili ya Rising Star Live Show. Kama kawaida kabla ya kurusha kipindi mgeni hupewa orodha ya maswali yatakayoulizwa, Loy alishapokea maswali na kuyaandaa sawa na ufahamu wake huku mengine akiyaacha kwa Ed mwenyewe kujibu. Rising Star Live Show iliongozwa na mtangazaji mahiri Rodgers Arthur, ambaye alijipatia tuzo mbali mbali kwa maudhui ya kipindi hicho.

***************************