Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 43 - NIAMINI MIMI

Chapter 43 - NIAMINI MIMI

Baada ya kushuka garini, Ed aliingia ofisini kwake na kukutana na wafanyakazi wachache waliowahi ambao nao walikuwa wamesimama kila mmoja mbele ya kompyuta yake. Edrian aliwaangalia kisha akasalimia, kusikia sauti wakashtuka na kugeuka. Wakasalimia, mmoja kati yao akamsogelea Ed....

"Jord vipi kuna shida gani hapa mbona mmesimama?" Akamuuliza

"Tumewasha kompyuta kaka lakini haiwezi kuendelea mbele inatuomba namba ya siri, tumejaribu kuingiza kila mmoja yake lakini bado haifunguki. Hapa nimempigia Alphonce wa ICT kasema tusifanye chochote anakuja yuko njiani "

Ed aliposikia hivi akapiga hatua bila kusema chochote hadi kwenye moja ya kompyuta zilizokuwa dawati la mbele..akaangalia na kisha akamgeukia Jord

"Msubiri Alphonce, na tafadhali wajulishe wengine kwenye idara zote wasiwashe kompyuta mpaka suluhisho litakapo patikana"

Jord akaitikia na kuelekea kwenye meza yake na kuchukua simu tayari kutoa taarifa kama alivyoelekezwa, akimuacha Ed ambaye alielekea ofisini kwake wakati akiwasiliana na Allan kwenye simu.

***************************

"Kama unataka baba yako nifilisiwe endelea na ukaidi wako kwako Ed" Martinez aliinua jicho lake lililoonesha kutoridhishwa na kitendo cha binti yake Joselyn kutofautiana na Edrian na asubuhi hii alikaa kwenye meza ya chakula kupata kifungua kinywa.

Joselyn ambaye alikaa mkono wa kuume wa baba yake, "Baba nimeshachoka na hii game, nataka kurudi SA..kwani lazima tumpate Ed?"

"Lyn sweetheart hebu jaribu kuwa mtu mzima tunapoongelea maisha. Hela unazotumia huko SA ni jasho langu. At once hebu jaribu kuwajibika. Nafanya haya kwa ajili yako, wewe fuata plan yangu..... sawa"

Sauti ya Martinez ilikuwa na msisitizo zaidi huku macho yake makali yalimwangalia Joselyn..

"Sawa baba" akaitikia kwa upole Josely akionesha kabisa kushindwa kujiokoa..

"Vyema sasa mpigie Ed"

"Baba bado sijajua niseme nini...naweza muudhi tena" alilalamika Joselyn

"Mwamini baba yako.....jana amekoswa koswa na ajali" Martinez akamwambia Lyn ambaye alishtushwa na taarifa ile

"Baba umefanya nini tena...hatujamaliza la Boric unaanza jingine" Lyn akalalamika

"Shhhhh sweetheart, sijafanya chochote. Nimepewa taarifa na mtu wangu tu aliyekuwa barabarani. Mpigie umjulie hali" Martinez akasisitiza

Joselyn akashusha pumzi na kupiga simu ambayo iliita kwa muda kidogo kisha ikapokelewa

"Goodmorning Lyn" akasalimia baada ya kupokea simu. Ed kwa uungwana wake hakuona ni vyema kutomsikiliza. Alimpa nafasi hata kama bado alikuwa na mashaka ya mambo ambayo Martinez anayafanya kwa kampuni yake.

"Goodmorning..... uko salama Ed?"

Martinez akamtupia jicho kali Joselyn akishangaa kwa nini binti yake kauliza swali ambalo hata mjinga akahisi kuna kitu anafahamu

"Niko salama, sijui wewe"

"Salama tu....nilikuwa nakusalimu" Joselyn aliongea kwa utulivu...Baba yake akampa ishara ya kwamba aendelee na kuomba msamaha. Joselyn akang'ata mdomo wake wa chini kisha akaendelea

"Edrian.... naomba unisamehe kwa yake yaliyotokea jana. Unajua nilipata wivu kuona namna ulikuwa unamuangalia yule dada A..anitha. am sorry"

Martinez akampa ishara ya pongezi binti yake kwa kuomba msamaha. Alifuatilia mazungumzo yote ya binti yake na Edrian.

"Okay Lyn. Yamepita hayo. And please usijaribu kunitawala. Nina maamuzi yangu." Maneno haya yalimfanya Martinez akunje sura maana hakutaka Ed ajione tayari kwenye zizi. Akasema moyoni mwake "just enjoy Simunge nakuja soon"

"Okay....Okay Ed. Can we talk later plz... naomba tuonane" Joselyn sasa alisihi kwa sauti ya upole

"Lyn....kesho itawezekana, leo ratiba yangu imejaa hadi jioni."

Lyn alitaka kulalamika lakini Martinez akatikisa kichwa kumuonesha asifanye hivyo, Lyn akafumba macho na kumwambia "Sawa Ed, kesho utanijulisha muda na mahali.."

"Sawa Lyn, siku njema" Ed alimaliza na kukata simu.

Joselyn alimwangalia baba yake kisha akaamua kuinuka ili kuondoka

"Lyn binti yangu usikasirike.. najua unajua kuwa nafanya haya yote kwa ajili yetu sote. Bado kitu kidogo tu tunavunja ngome yote ya SGC. Niamini mimi. Najua kwa kiasi gani umemiss maisha yako SA lakini unahitaji pesa. Vumilia"