Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 41 - MGUSO MMOJA

Chapter 41 - MGUSO MMOJA

"Brother kwani kuna tatizo gani umenishtua" aliongea yule dereva wa gari iliyokuwa nyuma.

Ed aliyekuwa ameinama kuangalia uharibifu kidogo kwenye gari yake akainua kichwa

"Samahani sana, kuna gari imeingia mbele yangu kwa ghafla"

Yule dereva akamwangalia Ed huku akiwa na mshangao akionesha kumfahamu..

"Eeeh.....ni Mr Simunge?"

Ed akamwangalia kisha akaachia tabasamu jepesi na kumuuliza, "ndio mimi, tunafahamiana?"

Kabla ya kumjibu honi za magari ziliwashtua kuwa kuna watumiaji wenzao wanahitaji kuitumia barabara...

"Nafikiri uharibifu sio mkubwa sana, naomba nikuachie kadi yangu. Naomba nitafute nitatengeneza" aliongea dereva yule ambaye alionesha kuwa bado alikuwa kijana mdogo kulinganisha na Ed. Akatoa kadi na kumpa Ed, ambaye aliipokea, akafungua mlango wa mbele wa abiria na kumtaka Aretha apande huku akimuaga yule dereva kijana...

"Asante sana brother, nitakutafuta"

Aretha akaingia na kukaa, Ed akazunguka na kuingia kwenye gari akifanya haraka.

Baada ya kuondoa gari, Ed akagundua wasi wasi ulioonekana usoni kwa Aretha ambaye alikuwa akituma ujumbe kwa mama yake...

"Naomba namba ya mama nimjulishe asijekuwa na hofu...." Ed alimuomba Aretha

"Hapana. .....aaah wala hakuna shida" Aretha akajaribu kumshawishi Ed kuwa si kitu...

"Aretha, please.." Ed alimwangalia na kurudisha macho barabarani...

"Nimeshamtumia meseji hata hivyo" Edrian akatabasamu baada ya kuambiwa hivyo hakutaka kuonekana anamlazimisha...

Mwendo wa gari ulikuwa wa kawaida sana, Ed alifanya hivyo baada ya kuona Aretha alivyoshtushwa na ile ajali ndogo waliyoipata..

Baada ya kimya cha sekunde 40, Ed akaona amuulize Aretha kuhusu ile picha aliyopewa na Derrick,

"Unamaanisha aliinunua na kuileta kwako?" Akauliza Aretha

"Alinipa zawadi, lakini nilihisi wewe tu ndio una uwezo wa kuchora mandhari ya ofisi yangu"

Aretha akamwangalia Ed na kumuuliza kwa haraka, "ikoje hiyo picha?"

Ed akashtuka akidhani inawezekana sio Aretha aliyeichora, " ni picha ambayo naifananisha na siku ile ulikuja ofisini, na hata nguo...." kabla ya kumalizia Aretha aliinama akiuficha uso wake kwenye mapaja yake.. "ooohh.. mama yangu aah"

"Nini Aretha?" Edrian akauliza akishangaa nini kiliendelea kichwani kwa Aretha..akainua mkono wake wa kushoto na kumgusa mgongoni akidhani labda ana maumivu.

Aretha akainuka ghafla baada ya Edrian kumgusa, sasa akageukia dirishani na hakutaka kumwangalia usoni. Uso wake ulijaa soni na alikuwa aking'ata midomo yake.

"Aretha kuna shida yeyote" akauliza Ed

"Aah. ..hapana... siijui tu hiyo picha..." akajibu pasipo kugeuka na kumwangalia Ed

"Then... mbona umeinama, una maumivu tumboni au kichwani" akauliza Ed ambaye alionekana kuwa na wasiwasi.. na wakati huu mvua za rasha rasha zilianza taratibu.

"Wala siumwi.... nilikumbuka tu kitu.. samahani kukushtua" aliongea akiendelea kuangalia pembeni. Moyoni akimlaumu mama yake....

Ed akamwangalia na akataka kumuuliza zaidi lakini walikuwa wameingia Moon street. Akaendesha huku akisubiri maelekezo ya Aretha. Wakasimama mbele ya geti la nyumbani kwao.

Edrian akashuka ili kumfungulia Aretha, lakini alipofika upande wa pili tayari alikuwa ameshuka. . Akachukua koti na kumfunika ili asilowanishe nywele zake katika manyunyu yale ya mvua. Akaelekea nae hadi getini..

Akatamani kumsindikiza hadi ndani lakini baada ya kusukuma geti Aretha akapiga hatua na kugeuka ili kumshukuru. Ed akajua hapo ndio mwisho wake kwa leo.

"Nashukuru Edrian"... alisema Aretha huku akimrudishia koti. Ed ambaye alikuwa akiyatazama macho ya Aretha ambaye alijaribu kuyakwepesha yasikutane na yake akatabasamu.

"Nenda usilowane. . Kumbuka kesho ahadi yangu..Msalimie mama." Akageuka pasipo kuchukua koti na kukimbia kurudi garini. Aretha alisimama pale kwa mshangao mpaka honi ya gari iliyokuwa ikiondoka ilipomshtua, akapunga mkono kwa Ed ambaye alikuwa akifanya hivyo..

Ed alitabasamu na kuendesha gari. Mawazo yake sasa yalikuwa na maswali ya kichokozi ya kwa nini Aretha alifanya vile baada ya kumpa maelezo ya picha. Akakusudia atakapofika ampigie Derrick.

Alitamani arudi nyumbani kwa mama yake....