Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 42 - USIJARIBU KUNITAWALA

Chapter 42 - USIJARIBU KUNITAWALA

Asubuhi ya siku iliyofuata Edrian alijiandaa kuelekea ofisini mapema. Alipomaliza akashuka kuelekea nje, ukumbini akakutana na Li ambaye naye alikuwa tayari kuondoka.

"Hey bro, umeamkaje?" Li akamsalimia Ed

"Salama ndugu yangu, vipi una miadi ya asubuhi?" Akauliza Ed

Ha ha ha... hapana bro, ninataka niwahi tu kupitia miamala ya jana niliondoka kabla ya muda....vipi jana ulimfikisha Aretha?" Akauliza Li sababu muda aliorudi Ed yeye alikuwa bado hajarudi. Alibaki wakiongea na Derrick kuhusu huyo huyo Aretha.

Edrian akatabasamu kwa sekunde kisha sura yake ikawa na mikunjo" ndio nilimfikisha.....japokuwa njiani kuna gari iliingia mbele yangu na kidogo tupate ajali..., nashangaa ilitokea wapi na wala haikusimama."

"Eh....gari aina gani hiyo? Check na Captain waangalie CCTV isije ikiwa ni jaribio la makusudi" Li aliongea na kudhihirisha wasi wasi wake...

"Nitafanya hivyo nitakapofika ofisini, kwa sasa naomba utaondoka na ile gari ili ukipata nafasi uipeleke kwa Preso atengeneze huko nyuma, kuna mtu alinigonga kwa nyuma" maneno haya yalimfanya Li atoke nje kuingalia gari huku Ed akimfuata kwa nyuma.

Edrian akakumbuka alipewa kadi na dereva aliyemgonga kwa nyuma lakini aliiweka kwenye kiti ambalo alimuachia Aretha..

"Sawa nitaenda, na kwa habari ya Derrick usihofu yuko upande wako kuhusu Aretha. Ni jitihada za upande..." Li alimaliza na kuachia tabasamu la utani.

"Duh! Ninyi wawili...oooh, sijui na Coletha akianza nitakuwa na hali gani, acheni.. am your brother, naweza kupata nachotaka bila kuwasumbua" Ed akajitetea

"Okay.....okay Bro, tutaacha kabisa ila kuhusu Lyn nitauliza what...."

"Please don't Li, nitaamua mwenyewe na nawaomba mnisaidie kwa kutoniingilia.... sawa? Ed akamtaisha Li kabla ya kuendelea.

"Sawa....not again bro, but kuhusu ile ajali naomba kujua na liweke kwa 4D." Li akamsihi Ed ambaye alikubali na kisha akaelekea ilipoegeshwa gari yake ambayo alikusudia kuitumia baada ya Volvo X2 kuwa imegongwa.

"Funguo ziko chumbani kwangu.. mwambie Preso aangalie pia breki... tuonane baadae!" Ed aliongea akifungua mlango wa Rover na kuingia ndani.

Akaondoka kuelekea kazini huku kichwani akiwaza matukio ya jana yake. Tabia ya Joselyn ilimkera na asubuhi hii hakutaka imharibie hisia zake, pia akakumbuka ile gari iliyotokeza mbele yake ghafla; akawaza kama ni kawaida au ilifanya makusudi. Akachukua simu yake kupiga, na ndani ya sekunde 30 alimalizana na Captain. Akakumbuka kadi aliyopewa na dereva aliyemgonga kwa nyuma....aaaah ipo ndani ya koti alilompa Aretha... "siwezi kumpigia sasa hivi bado mapema..." akawaza. Pamoja na kuwa na ahadi ya kukutana nae jumanne bado Ed hakuwa na hakika kama Aretha angekuja sababu hakuwa amesema chochote. Ghafla mlio wa simu ukamshtua....

"Joselyn.....duh i can't have a peaceful morning" Aliwaza Edrian.

"Goodmorning Lyn" akasalimia baada ya kupokea simu. Ed kwa uungwana wake hakuona ni vyema kutomsikiliza. Alimpa nafasi hata kama bado alikuwa na mashaka ya mambo ambayo Martinez anayafanya kwa kampuni yake.

"Goodmorning..... uko salama Ed?"

Edrian alishtushwa na swali hilo maana sauti ya utulivu ya Lyn sasa ilisikika na wasi wasi kwa mbali. Akaamua kujibu katika hali ya kawaida

"Niko salama, sijui wewe"

"Salama tu....nilikuwa nakusalimu" Joselyn aliongea kwa utulivu...akavuta pumzi na kuendelea kabla hata Ed hajajibu..

"Edrian.... naomba unisamehe kwa yake yaliyotokea jana. Unajua nilipata wivu kuona namna ulikuwa unamuangalia yule dada A..anitha. am sorry"

Ed ambaye sasa alikuwa ameingia Ashanti Tower akiwa kwenye maegesho maalum.

"Okay Lyn. Yamepita hayo. And please usijaribu kunitawala. Nina maamuzi yangu." Maneno haya yalimtoka Ed taratibu lakini yalidhihirisha msimamo wake..

"Okay....Okay Ed. Can we talk later plz... naomba tuonane" Joselyn sasa alisihi kwa sauti ya upole

"Lyn....kesho itawezekana, leo ratiba yangu imejaa hadi jioni." Sauti ya Ed ilionesha dhahiri alimaanisha kile alichosema na si kwa sababu ya yale yaliyotokea jana yake.

Lyn alitaka kulalamika lakini ni kama alikuwa na mtu akamzuia, "Sawa Ed, kesho utanijulisha muda na mahali.."