Chereads / MALAIKA WA UPENDO / Chapter 4 - SEHEMU YA NNE

Chapter 4 - SEHEMU YA NNE

Marandola alikuwa akiendelea na vibarua vyake vya ujenzi Kama kawaida baada ya siku kadhaa alipata pesa na kumununulia mwanae Kamusi ya kingereza na kiswahili. Wadhati alifurahi Sana, akijisemea moyoni Sasa basi ugonjwa umeisha. Wadhati akajiwekea ratiba ya kukalili misamiati kumi kila siku ya kingereza, Ndani ya mwezi mmoja Wadhati akaanza kuonesha mabadiriko darasani hasa nae alipoanza kujibu maswali kwa ufanisi Kama wanafunzi wengine hii ilimfanya kuongeza bidii zaidi na zaidi na hata kupeleka kuipenda shule. Siku moja moja tayari akaanza kuhudhuria na kuchangia hoja kwenye midaharo ya shule. Siku zikazidi kwenda Wadhati akaendelea kupata umaarufu taratibu, sababu ya uwezo wake alikuwa akiuonesha ndani na nje ya darasa hivyo alipata marafiki wengi zaidi hata walimu nao kwa juhudi zake alizozionesha. Hata waliomcheka ile siku ya kwanza darasani aliposhindwa kujibu swali wakawa marafiki zake. maswali yalipowashinda walimpelekea, Wadhati hakujari Wala kuwabagua aliwasaidia. Iliwashangaza Wanafunzi wenzake nakuwaacha midomo wazi. " Jamani... mmoja wa wale aitwae Ciama akaguna tu. "Mmh sijapata kuona yani huyu mkaka anaroho nzuri kweli.... Lakini Kachoyona na Birika, walivoanza tu kubukua darasani hawataki Tena urafiki na mtu mwingne, Nhee wanamaringo hao, Chausiku nae akadakia we acha tu tutawaona mtihani unaokuja Kama wataongoza.

Juria akajifungua mtoto wa kike akamuita Cheichei kwa kiruga Chao mfunga mlango kwa pamoja wakafurahi Sana hasa kwa Wadhati na Wakamba kupata mdogo wao wa kike, Marandola alianza kutembea mtaani akiringa "ngoja nianze kuandaa zizi taratiibu ng'ombe tayari watanikoma tu mwaka huu"

Wadhati alikuwa akijiandaa na mtihani wataifa wa kumaliza kidato Cha pili, Juria Kama kawaida yake aliendelea kumsii Sana mwanae afanye kwa bidii zote richa ya kwamba tayari ashaonekana Ni kipanga shuleni. Hata hivyo mda mwingi Wadhati aliutumia kuwa karibu na mama yake kwa sababu Baba yake hakuwa Mtu wa kushinda nyumbani. Hivyo Juria alichukua jukumu kubwa la kumwelezea Mambo mengi hata Yale ambayo alitakiwa kuelezwa na Baba yake. Baada ya mtihani wa taifa kuisha Wadhati akamuomba Mama yake ampatie sehemu alime kijibustani ili aweze kujipatia kipato kwa matumizi yake binafsi.

Kulingana na hali iliyokuwepo nyumbani. Juria hakusita kumpatia mwanae sehemu aliyokuwa anahitaji. Wadhati akaanza kulima mboga mboga ambazo hazikuchukua mda mrefu Sana kukomaa. kwakua alikuwa na Marengo hivyo akaweka bidii ya hali ya juu Sana katika kuhudumia kijibustani chake. " Haloooh, karibu bwana Kapesa, Shikamooo"... Marahaba, asee umeivisha bwana hongera Sana,.." Asanteeeeh..." sasa me nimepata Oda ya kupeleka mjini hizi mboga mboga, Kunahoteli moja hivi wanahitaji,. " Aaah amnashida Wala usiwe na Shaka zote hizi Mali yako hakuna mteja mwingne tena ani hata ningekuwa na uwezo ningekuuzia na udongo wake kabisa,.. " ahahahaaaaaa dah, haya bwana umeamua kunichekesha asubuhi hii hata jogoo bado hajawika, haya basi nipe bei. "ahahahaa usijari bwana kapesa Ni ile ile ya sikuzote, we toa pesa tu mchezo uishe"

Kwa kuwa Wadhati alikuwa Mtoto wa kwanza, kiasi Cha pesa alichokipata akamua kununua Sola kwa ajiri ya Mwanga wakati wa usiku. Juria na Marandola hawakuamini Wala kutegemea suprize aliyowafanyia mtoto wao, walifurahi Sana na kumuombea baraka siku moja aweze kufanikiwa katika Maisha yake. alifaulu kuendelea na masomo ya kidato Cha tatu. "Taratibu tunaanza kuondoka kwenye umasikini mwanangu Mungu akujalie kila lenye kheri na uendelee na moyo huo huo hata uwapo shuleni,... Haya sawa Baba" Wee Cheichei...., Abe..! Mama..., Hebu niletee maji ya kunywa harafu pitia panga hapo kwenye Kona ya mlango twende kwenye kuni Mwanangu." Haya sawa Mama.... Kisha Juria na mwanae wakaelekea msituni kuchanja kuni.