Chereads / MALAIKA WA UPENDO / Chapter 10 - SEHEMU YA KUMI

Chapter 10 - SEHEMU YA KUMI

Wadhati akiwa kambini anamalizia kozi matokeo yakatoka "Oh woow nimefaulu thanks dear God kwa wema wako mkeka wa chuo umetiki. Taarifa za matokeo zikafika nyumbani. Wazazi walifurahi sana. Mke wangu sasa umasikini Basi tena Wadhati atatusaidia kuwasomesha wadogo zake... yalikuwa Ni maneno ya marandola aliyekuwa amekaa chini ya mti anapiga stori mkewe mama cheichei hiyo siku hakwenda kibaruani kwa sababu ya uchovu wa jana.

Wadhati alifanikiwa kutuma maombi ya chuo akiwa huko huko kambini ili kuwa na uhakika aliomba vyuo vitatu MOCUZO, ST PWEZA na BUZUKI. Baada ya mafunzo walitunukiwa vyeti Kisha kila mmoja akarejea kwao kujiandaa na elimu ya chuo kikuu. Wadhati alikuwa na furaha Sana kwanza kwa kuhitimu mafunzo salama na kuikuta familia yake wakiwa wazima na wenye afya tele. Cha kwanza kabula ya yote aliomba simu yake maana alikuwa kamu miss Sana mpenzi wake Lucier . Ghafla furaha yake ilipotea Kama mshumaa uliozimwa na upepo wa kisurisuri baada ya kufungua simu na kukutana na SMS zenye ujumbe mzito.

"salamu wangu my lazizi nasikitika kukwambia kwamba Mimi na wewe ndo basi tena uhusiano wetu uishie hapa. Nilikusubiri sana huonekani nilikuvumilia vya kutosha tena cha zaidi ukimya wako ndo umenitenga nawe, nilijitahidi sana kuvuta subira mwisho nikashindwa, nili lilia sana Kama mtoto mchanga asie na mama nilijuta kwa nini nilimkabidhi ng'ombe anilindie majani fala mkubwa usiejua maana ya upendo wa dhati ni Nini. Yani hata salamu tu miezi mitatu kweli ?. Hapana wadhati, Kama ulikuwa na mpenzi wako huko kwenu si ungeniambia kuliko kuniterekeza kimya kimya ukaona ni bola unikaushie kisa uliona nakupenda eeh, non sense.! Na kwa taarifa yako sasa me nilishapata anipendae na nyumbani nilishaenda kumtambulisha mwakani ni harusi yetuuu UKITAKA njoo uone ninavyo vishwa pete MWANAHARAMU MKUBWA WEWE CHUNGA UTAKUFA KIFO KIBAYA SANA.

Wadhati alibaki ameduwaa kama mtu aliepigwa shoti ya umeme baada ya kumaliza kuisoma Ile SMS alijihisi Kama mtoto yatima alie fiwa na ukoo mzima kwa siku moja hakuamini alichokisoma ili bidi arudie mala mbili mbili. Aliamua kwenda chumbani kwake na kuanza kulia mwisho alipitiwa na usingizi.

Siku iliyofuata likamjia wazo la kumutafta Vero ambae alikuwa ni rafiki yake Lucier.. alichukua kisimu chake kidogo Kisha akaanza kupekua majina"Ehee yesi huyu hapa Veronica... akapiga woow tena vizuri simu yake inaitaa. Vero akapokea simu "Oh woow haloo shem mambooo... Poa shemu za siku... Aisee Ni njemaa kidogo...basi Wadhati akamuelezea ile sms ilivo na chanzo cha kutokuwa hewani hivyo akataka ajue ni nini chanzo cha Ile SMS maana alipo isoma hakuelewa vizuri... Ooh pole shemela wangu ipo hivi baada ya wewe kukaa kimya sijui ndo ulienda jeshini, Lucier yeye aliendelea kukutafta kila siku hupatikani mwisho akachoka akajua ushamblock na huna time nae Tena hadi aliugua kwa sababu yako baada ya mda akawa sawa sasa na me nikawa bize kidogo na Mambo yangu siku moja akawa kanipigia simu akaniambia tayari amepata mchumba anataka kumuoa mkaka flani hivi Kama unakumbuka Kuna njia flan hivi tulikuwa tukiipita wakati wa kwenda kanisani pale kwenye yale makaburi kushoto Kuna saloon pia wanauza na urembo ndo huyo mkaka ambae me aliniambia ndo mchumba wake na tayari alishamtambulisha kwao kwa hiyo ndo hivo shemela wangu we angalia tu ustaarabu mwingine..

Wadhati alibaki akiumia sana moyoni akikumbuka visa na Mikasa yote aliyo ipitia kwenye mahusiano"Mmh naona huku sio ridhiki yangu sijui niende tu upadri maana hata Kama unamoyo wa chuna mwisho ipo siku nao utapata kutu. Basi wadhati akapiga moyo konde akaendelea na Maisha yake. Siku moja jioni katika pita pita zake akapita sehemu moja hivi kulikuwa na mkutano wa injiri kulikuwa na mchungaji Moris aliekuwa akifundisha juu ya upendo jinsi Malaika wa Upendo anavyo fanya kazi ya kuwakutanisha wachumba na ni jinsi Kama kijana ufanye ili kupata mweza alie bora.

Ooh woow wadhati alivutiwa sana na Ile maada iliyokuwa ikitolewa na mchungaji Moris "Hallelujaa.... Jeoni ya leo mbengo zetafunguka namuona mwana wa adamu anakwenda kufunguliwa wewe uliyeteseka kwenye mahusiano nisikilize kwa makini Ooh hallelujah... Leo ninakwenda kuuponya moyo wako sema Amen....

Mmmh huyu mchungaji mbona kama kanilenga Mimi hebu nikae kwa kutulia huenda nikapata chochote kitu. Mchungaji Moris aliendelea... Jeoni ya Leo tutakwenda kujifunza somo linalo husiana na upendo maada yetu kuu ikiwa Ni kazi ya Malaika wa Upendo Hallelujah..... Aimeeeeee.. wote naomba turejee katika kitabu Cha mwanzo. Hapo mwanzo Mungu aliumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo ndani ya siku sita na siku ya saba akapumzika. Aliumba mimea, wanyama, ndege mwisho akamuumba mwanadamu na kuwabariki kwa pamoja zaeni muongezeke mkaujaze ulimwengu na vitu vyote vilivyomo mkavitawale. Hallelujah..... Aimeeeeee. Hapo ndipo upendo ulianzia. Acha nikwambie mpendwa Mungu akamteua Malaika wa Upendo awe ndiye kiongozi na msimamizi wa mahusiano kwa wanadamu na ndiye atakae hakikisha kila mmoja anampata Alie sahihi kwake ambae wataishi katika upendo ili kulitimiza vyema agano nalo Ni kuujaza ulimwengu Hallelujah... Aimeeeeee..... Hivi mnajua kwa nini vijana walio wengi wanapata tabu katika mahusiano?. Haya nisikilize mpendwa.. vijana wengi wa sikuhizi wamekuwa wakiharakia Mambo mtu wanakutana tu barabarani, shuleni then tayari tayari hujamshirikisha huyu malaika ambae ndiye jukumu lake matokeo yake nyie vijana wa sikuhizi mmejipa madaraka wenyewe kwa kuangalia muonekano hasa uzuri wa sura na umbo Kisha unavuta jiko bila kumshirikisha huyu Malaika wa Upendo, haya matokeo yake ni nini baada ya siku kazaa ugomvi unaanza ndani michepuko Kama yote kelele kutwa nzima kazi kupishana studio tu kuimba mapenzi. Siku moja nitoka kwenye mkesha mida ya saa saba hivi usiku nikakatiza mitaa flani hivi nikamsikia kijana wa watu analia huku anaimba 🎢 umeachwa we kubari kubari utampata wako mtapendana kwa zati🎢 niliishia tu kutikisa kichwa na kuona kunahaja ya kuandaa hili somo ili kuwa fungua vijana la sivyo mtakufa kwa stress za mapenzi. Basi ni nini tufanye ili kuepukana na hizi changamoto unapoona umefikia mda ambao unahitaji kupata mweza piga goti chumbani kwako sali muombe huyu malaika wa Upendo ili akuoneshe Alie chaguo lako na ambaye ni sahihi kwako wengi wenu mnateseka kwa sababu mnachukua wachumba wa wenzenu ipo hivi sikuzote Mungu anakupa wa kufanana nae Kama wewe mwizi Kuna dalili kubwa za kupata mwizi mwenzako hivyo vijana tubadilike tuache kujichukulia mamuzi mkononi.

Baada ya mkutano kuisha yapata mida ya saa moja jioni Wadhati alilejea nyumbani akiwa Ni mwenye furaha sana kwani alipokea mafundisho makubwa Sana ambayo hakutegemea... Daah kumbe siku zote nilikuwa nikiumia kwa sababu ya kuharakia mambo. Baada ya machaguo ya chuo kutoka Wadhati alichaguliwa kujiunha na chuo Cha ST. PWEZA kilichopo kusini mwa Thamalia akiwa kachaguliwa kusoma Bachelor of Art with Education (BAED). Ilikuwa Ni furaha isiyo kifani pale nyumbani lakini pia Kijijini Bustania. Mda wa kwenda chuo ulipo wadia Wadhati alikata tiketi ya treni ambayo ilitembea takribani siku mbili njiani, pia kulikuwa na mabasi ambayo yalifika pwani ya kusini siku moja kulingana na hali ya kiuchumi iliopo nyumbani kwao hivyo hakuwaza kukata tiketi ya usafiri wa basi. Baada ya kufika chuo alipokelewa vizuri akaripia ada na kufanyiwa usajiri kwa bahati nzuri hostel za chuo hazikuwa zimejaa hivyo akapata chumba akapumzika.

Wadhati akaendelea Kama kawaida na masomo yake ya chuo kikuu, mala nyingi alikuwa akiyakumbuka sana maonyo ya Juria mama yake hivyo ilimfanya asome kwa bidii sana wakati wa rikizo hakuweza kurudi nyumbani hivyo alikuwa akitafta tempo za kufundisha ambazo zilikua zikumuingizia kipato ambacho kilimusaidia kuendeleza Maisha yake wakati wa rikizo. Mwaka wa pili wa masomo ulipo anza Wadhati tayari alikuwa amshakuwa mkubwa hivyo alianza kipanga mikakati ya kutafta mchumba ambae ataishi nae baada masomo yake ya chuo. Hakukurupuka tena hivyo alijiwekea vigezo vyake alivyokuwa akivihitaji... Natamani mwanamke nitakae muoa awe na hofu ya Mungu. Akaendelea na masomo yake hiki kipindi hakuwa tena mwepesi wa kubabaika ma mademu wa chuo maana alijua ndo wale wale kina Joyce na Lucier. Aliendelea kusoma kwa bidii sana kiasi ambacho ilimpelekea kupata ufaulu mkubwa. Likizo iliyofuata Wadhati alitamani sana kwenda nyumbani kuwaona ndugu zake kipindi hiki alikuwa na pesa ambayo ameikusanya wakati tempo na field hivyo aliweza kukata tiketi ya basi siku ya Safari ilipo wadia Wadhati akabeba begi lake na baazi ya vitu ambavyo alinunua kama zawadi Kisha akapanda Basi kuelekea Kijiji kwao Bustania.