Chereads / MALAIKA WA UPENDO / Chapter 12 - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Chapter 12 - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Palivokucha wadhati akiwa ameshachukua mawasiliano ya mpenzi wake mpya wakaenda kwenye cafe kupata angalau kifungua kinywa. kisha akamsindikiza hadi stend wakaagana vizuri kwa kukumbatiana na mabusu Moto Moto bila kujari kadamnasi ya watu.

Upendo alipofika kwao alipokelewa na mama yake Mariana pamoja na dada yake mkubwa Faima. Mariana alifurahi sana kumuona mwanae akiwa mzima na mwenye afya tele. Pole kwa masomo mwanangu.... Asanteee mama nilikumiss kwelii, mama baba yuko wapi? "yupo dukani kwake. Richard alikuwa na duka kubwa la jumla pale nyakahoja. Upendo baada ya kupata chakula akaenda kumsabahi baba yake.

Usiku upendo akiwa na dada yake kwenye chumba chao akaanza kumuelezea yote aliyokutana nayo tangia mwanzo wa safari hadi mwisho. Dada Faima nimepata mchumba mwenzio anaitwa Wadhati. Mmh haya bhana kwahiyo umeamua kutuletea na mchumba kabisa eeh! Haya niambie anaitwa nani huyo mchumba? Anaitwa Wadhati. Nani?. "wadhati" ahahahaaaa afu we una masihara. Mweee jamani dada sa mi nikuongopee kweli?!. Ety wadhati.. "kweli dada anaitwa wadhati ndio jina lake, yes Wadhati Marandola. Mmh hongera mwaya tuseme mmechagua majina yanayo endana. Kivipi dada. ...mmh si Upendo wa Dhati. Jamani dada mwee. Wote wakacheka. Ok me nawaombea hayo mapendo yenu ya dhati yadumu daima. Amen. Ok mwambie na mama pia, sawa dada usijari nitafanya hivyo. Mmh ok nimepata wazo hebu kabla huja waeleza subiri kwanza umalize chuo maana kwa Sasa si umebakiza mwaka mmoja fanya u wait kidogo now wazee watazingua si unamuelewa mshua hapendi Mambo ya kiwaki malizia huo mwaka kwanza uliobaki hapo Mambo yatakuwa mwake mwake.

Wadhati akiwa nyumbani kwa kua alitoka chuo na vijisenti kidogo akavitumia kujenga pale kwao nyumba ya vyumba vitatu na sebule na choo ya kisasa japo aliimaliza kwa shida ila ilikamilika kwa wakati, aliendelea kuwasiliana na upendo huku wakipanga mikakati mbali mbali ya Maisha yao. Baada ya rikizo kuisha wote walirejea chuoni kuendelea na masomo.

Taratibu nasi tumeanza kuwa watu miongoni mwa watu mke wangu, unakumbuka ulitaka kuitoa mimba ya huyu mtoto kisa wazazi wako hawakutaka nikuoe Leo tungekuwa wapi?."yalikuwa Ni maneno ya Marandola aliekuwa akizungumza na mkewe". Baada ya kuhitimu masomo Wadhati aliwajurisha wazazi wake kuwa tayari amepata jiko. Wazazi wake walifurahi sana kwa taarifa Ile kwani ili kuwa Ni baraka kubwa ndani ya familia, hivyo Kama familia waliandaa taratibu za kutuma mshenga kwao Upendo. Baada ya mwezi mmoja Richard na Mariana nao waligubikwa na wimbi kubwa la furaha kusikia binti yao kapata mchumba. Siku ilipo wadia Wadhati na familia yake walienda kwao Upendo kwa ajiri ya kujitamburisha na kupewa utaratibu wote wa mahari. Tumefurahi kwa kua mmpenda binti yetu, Ni furaha kubwa kwetu sote kuunganisha ukoo na kuwa kitu kimoja, sisi wazazi wake upendo hatuna pingamizi tumekubali kwa moyo wa dhati kuwakabidhini binti yetu mkaishi kwa furaha na amani siku zote, mkachukuliane mapungufu yenu tunawaombea mkaishi vyema kwenye ndoa yenu. Ikatangazwa tarehe ya ndoa wote wakiwa na furaha Sana. Siku ilipo wadia lilifanyika bonge la party haijapata kutokea pale kijijini Bustania haikuwa na kiingilio chochote Ila miguu yako na tumbo lako, watoto walibeba wali kwenye mashati. Familia ya Richard walitoa zawadi ya nyumba na pesa Kama mtaji wa kuanzia maisha.

MWISHO.

Imeandikwa tarehe 10 March 2020, na Salvatory Luciano

Nawasiliano : +255745645716. via WhatsApp