Akiwa ndani ya Basi ni Kama kipofu kaona mwezi alipata bahati ya kukaa na binti mrembo Sana mweupe kiasi halafu mpole. Kwanza kitendo Cha kukaa na binti mrembo siti moja alijiona amekuwa mwepesi ghafla Kama kifaranga aliemponyoka mwewe akafunga vizuri mkanda wake kisha kwa upole akaanza kumuongelesha yule binti.. Hellow Mambo sister... Yule binti akamtizama kwa tabasamu mrua kisha akamjibu poah huku akiona aibu. Uzuri wa binti na madoido aliyokuwa nayo ulimchanganya sana hivyo akajikuta avitukia kutaka kumfahamu zaidi. Samahani unajua si vizuri kuitana wewe vp naweza kukufahamu jina lako?.... ahahahaaaa bila shaka naitwa Upendo Richard. Huku Kama akirembua na kuchezesha midomo na shingo yake. Oh wow nimefrahi kufahamu. Nawe waitwa nani... Wadhati Marandola. Nani?!. Wadhati yule binti akachekaa.. acha utani wako bwana niambie ukweli. Wadhati ili bidi amuonyeshe kitamburisho chake ndo mrembo akaridhika. Upendo alicho kifanya akachukua kalamu na karatasi kwenye kinainai chake. Wadhati akiwa bize kutizama uso mrembo Upendo ulivosoft kwenye upande wa pili wa kioo bila upendo mwenyewe kugundua jamaa alikuwa akimla chabo face yake. Upendo akiwa bize anayaunganisha yale majina mawili jina lake yeye na lile la wadhati. Ooh wooow upendo alicheka kwa furaha huku akimuonesha huku akimuonesha kile kikaratasi. Wooow it's amazing soma UPENDO WA DHATI wote walicheka kwa furaha huku wakiangaliana usoni Kama ishara ya kitu fulani. Daah Upendo we ni mbunifu Sana unajua nilikuwa sijawaza kabisa hichi kitu. Upendo na Wadhati walijikuta wamezoeana ghafla as if walikuwa wakifahamiana tangia hapo awali. Baada ya kufahamiana majina yao wakaendelea na stori Kama kawaida. Wadhati akamuliza Upendo vipi huku pwani ndo nyumbani?... Hapana kwetu ni Ghetania huku nilikuja field me nasoma MOCUZO Mambo ya Library and information technology. Nawe je me nipo ST. PWEZA pale kwetu ni Bustania pale pale Ila lazima uvuke maji ndio ufike kwetu. Wapii kwenu?. Bustania. Hah?!. Upendo alishangaa sana huku akijisemea moyoni au huyu atakuwa ndugu yangu nini. Akamuuliza nyakahoja unapafahamu? Ndio napafahamu kuna bibi angu kule na maranyingi nilkua nikipendelea Sana kwenda wakati wa rikizo. Mmh.! Pendo aliishia kuguna tu nakijiuliza huyu ni nani kwani? Wadhati nae akamuuliza we ni mwenyeji wa mtaa gani? Upendo akatabasamu kisha akamjibu Ghetania mtaa wa Nyakahoja. Haah!.. wadhati nae ndo akashituka Kama mtu aliekuwa usingizini. Kumbe ndo maana ulikuwa ulikuwa ukiniuliza maswali mengi kumbe tumetoka maeneo jirani ahahaaa ulikuwa ukinidadisi dah!. Upendo umenishinda tabia. Wote wakacheka huku wakiangaliana machoni kwa aibu. Wadhati alimtizama tena usoni na kujisemea kimoyo moyo sasa baasi donda limepata mponyaji. Kuna mama flani hivi mcheshi sana harafu huwa anaimba kwaya na kupika vitumbua unamfahamu?. Aah namfahamu si mama Kelvin. Ewala haswaaa ndo huyo ninae msemea. Hadi kwake napafahamu vipi ni ndugu yako? Ndiyo... Wadhati alishangaa Sana hakuamini alichokiona wote waliishia kutizamana tu nakucheka kila mmoja akijitahidi kuionesha furaha yake.
Ilikuwa yapata saa kumi jioni basi likasimama kwenye hoteli moja njiani kwa ajili ya kupata chakula Wadhati ndo akamuona kwa uzuri zaidi wakati upendo akiwa ametangulia kwa mbele kidogo. Alaa! Kumbe huyu mtoto ni fire mamaaa huyu ni zaidi ya stima nanii washa lala huyu lazima niibuke nae kwa namna yoyote Ile she is so beautiful. Sijawahi kupiha stori na binti mrembo hivi na tukacheka kiasi hiki tangu nizaliwe jinsi anavyo nipa ushirikiano Hadi nimedata tangu saa kumi na mbili alufajiri sina hata dalili ya uchovu Wala njaa. Upendo kwake pesa haikuwa tatizo hivyo akaagiza msosi wa gaharama huku wadhati akiwa bado haamini anacho kiona... Kula my mbona wanishangaa sana. Ooh hapana Wadhati alikuwa kapagawishwa na urembo wa Upendo. Baada ya kupata chakula wote wakarejea kwenye gari. Baada ya kurejea kwenye gari ustaarabu ulimshinda hasa akikumbuka ameitwa My ndo alizidi kuchanganyikiwa akajikuta akiropoka. Upendo samahani hivi unaboyfriend?.. ahahahaaaa dah umenichekesha vp mbona umeniuliza hivyo?.. A.a..ah hapana nimeuliza tu. Na hata Kama yupo namsihi akushikirie kabisa asikuache hata Kama hayasikii haya maneno sio kesi yatamjia hata akiwa ndotoni. Upendo aliangua kicheko kikubwa ndani ya basi. Mbona unanifurahisha Sana wadhati kwa maneno yako. No ukweli umenifanya nifarijike Sana siku ya leo hii siku nitaiandika kwenye diary yangu ya matukio ni siku muhimu sana kwangu.. Upendo akatabasamu tu kisha akamjibu sina am single mehn!. Wadhati bila kupoteza mda akaanza kushuka vocal. Upendo wadhati nimetokea kukupenda sana jinsi ulivonionesha ushirikiano na kunijari natamani na ningefurahi Sana Kama hutojari natamani siku moja uwe utimirifu wa ndoto yangu niliyokuwa nikiiota kila siku usiku wa manane a.a.ah I need u to be ma future wife. Upendo alicheka na kuuficha uso wake kwenye bega la kushoto la Wadhati, upendo aliendelea kuchukuria Kama utani. Hebu rudia unathemaa.... Ahahahaaaa Ila upendo hakili yako unaijua mwenyewe nakupenda natamani siku moja uwe mama wa watoto wangu moyo wangu unaniambia nisikuache nahisi malaika wa Upendo kanikutanisha nawe ili litimie lile agano kwanza majina yetu yanasaund vizuri Sana ety UPENDO WA DHATI nimeshangaa sana sikuwahi tegemea ntakutana na muujiza Kama huu nahisi wewe ndiye. Upendo yeye alicheka tu huku akimurembulia macho. Aah okay kwa hiyo ulikuwa unatakaje?.. nimekupenda na nipo tayari kuwa baba na wewe uwe mama wa watoto wangu Kama hutojari. Hapa upendo kidogo akapunguza matani akawa serious. Pole mbona umekuwa hivo ghafla?.. hapana naogopa sijawahi kuingia kwenye mahusiano hivyo naogopa kuumizwa maana nimeshuhudia dada yangu alivokuwa akiteseka. Sure niamini nakupenda, ntakurinda na kamwe ntakufanya kuwa mwenye furaha mda wote Kama leo hivi. Upendo akatabasamu. Kwahiyo unaniahidi hautanisaliti?. Ondoa shaka niamini please haya ninayokwambia namaanisha. Haya sawa me nimekubali.. Ooh woow wadhati alifurahi sana hakuamini alichokisikia. Upendo nae alibaki akishangaa tu imewezekana vipi kumkubalia huyu ni nani alievunja msimamo wake maana alikuwa ashajiwekea msimamo kuingia kwenye mahusiano ni hadi pale atakapo maliza masomo yake.
Mwisho basi lilifika stend mida ya saa saba usiku Wadhati tayari alikuwa kaisha fika kwako. Lakini nawezaje kuiacha hii pisi ilale pekee ake harafu me niende home utakuwa ni ushamba wa hali ya juu sana. Kwa kuwa Wadhati alikuwa mwenyeji maeneo yale akatafuta chumba kizuri wakaenda kipeana malavidavi.....