Wadhati alilejea nae nyumbani kuendelea na ratiba zake. Kama kawaida yao baada ya kutawanyika walibaki wawili darasani wakijisomea na Kisha kufanya yao.
Mtihani ulipo wadia wa kuhitimu kidato Cha tatu Wadhati hakufanya vizuri alikuwa kaporomoka kutoka nafasi ya kwanza Hadi ya kumi huku nafasi ya kwanza na ya pili zikiwa zimeshikwa na marafiki zake Jamari na Malinzi, Wadhati alilia kwa uchungu hakuamini alichokiona pia hata walimu walimuadhibu kwa kuanza kuendekeza uzembe. Wadhati alibaki akiwa Ni Mwenye mawazo, hata nyumbani wazazi wake walimgombeza kwa kuanza kuendekeza uzembe kwenye masomo.
Siri ya mtungi aijuaye kata, Wadhati alijua yote chanzo Cha kushuka kimasomo Ni kuendekeza mapenzi shuleni. "Nilikwambia kuwa makini Kaka, sie wote bado wanafunzi mapenzi yatakupoteza, tena hata shukuru kwa sababu unauwezo binafsi angekuwa mwingine nadhani angetaga kabisa" Yalikuwa maneno ya Malinzi akimunasihi Wadhati, "Dah, nimekuelewa bro! me sifanyi ujinga tena. "Sawa lakini sikio la kufa huwa halisikii dauwa" Wadhati aliyakumbuka maneno ya mama yake "Mwanangu Sasa unaenda kuanza form one, uache mchezo ukatulie kabisa, kaweke bidii pia zingatia yote niliyokueleza Hali ya nyumbani kwenu unaiona sisi Ni masikini.."
wakiwa likizo Wadhati hakuweza kuonana na Joyce hivyo akawa huru akaanza kusoma upya kwa speed ya 4G, japo sikumoja moja alikuwa akimukumbuka Joyce na kutamani amufuate kwao maaana tayari kaisha uonja Utamu wa asali. Joyce nae baada ya kuyajua mapenzi vizuri alitamani kila siku apate dozi, hivyo kulingana na kuwa mbali na Wadhati Joyce alianza kujirahisisha na Machalii wengine wa kitaa. Sikumoja Jamari katika pitapita zake jioni, karibu na nyumba za wageni, alishituka ghafla kumuona Joyce akitoka mle ndani na pande la milaba minne limepanda hewani, "He! Maajabu!" Jamari alijificha kando na kutazama kinachoendelea, maana hakutarajia kumuona Joyce kafikia ile hali. Jitu la Milaba minne, likachomoa waleti na kutoa noti mbili za sh. Elfu kumi na kumpatia Joyce Kisha wakamwagikana kila mmoja akapita njia yake. Jamali aliishia kuguna tu nakutikisa kichwa, "Nilijua tu hamna kitu hapa" Kisha akaendelea na Safari zake.
****
Baada ya rikizo wote walilejea na kuendelea na masomo Kama kawaida, hiki kipindi Joyce hakumchangamkia sana, Tena alikuwa kapendeza zaidi kuliko hata mwanzo, "Joyce sikuhizi hanichangamkii Kama mwanzo na mda mwingi utakuta yupo kwenye ofisi ya mwalimu wa michezo sijui huwa anafata nini". Jamari alikuwa kimya akimsikiliza tu maana tayari alikuwa anaufahamu mchezo unao endelea kwa Joyce na alijua akimweleza rafki yake itakuwa jau "Huyo ni mpenzi wako we tafuta mda tu muite mkae muongee". Joyce tabia yake ilizidi kuchenji siku hadi siku, ilifia hatua akaanza kutoka na maboy wengine wa humo humo darasani hakujari kabisa richa ya uwepo wa Wadhati darasani.
Wadhati aliumia na kukonda sana, baada ya kuona kilichokuwa kikiendelea kwa Joyce alimpenda sana na alitamani sikumoja awe mama wa watoto wake. Jamari alimtuliza na kumweleza Hali halisi tangia siku alipomuona akitoka gesti. Wadhati alijamu "Mbona hukuniambia mapemaa Jamari why rafiki angu unataka nife?". No.no. sio hivo niljua hutoniamini so nilisubiri uje kujionea mwenyewe kwanza. "Dah, inauma sanaa". Huyo achana nae wako utamkuta huko juu amekusubiri. Wadhati alijuta kumpenda Joyce, "Daah, nimemkabidhi ng'ombe anilindie majani".
***************************************
Wadhati, Jamari na Malinzi wote walifaulu na kufanikiwa kuendelea na masomo ya kidato Cha tano na sita. Wadhati alichaguliwa KWAMBI HIGH SCHOOL, Wazazi wake walifurahi Sana kuona mwanao amefanikiwa kuendelea na hatua nyingine ya elimu, walimtayarishia mahitaji yote muhimu na kimkabidhi, akiwa tayari na uwezo wa kujisimamia baada ya mda kuwadia wadhati alienda shule mwenyewe.
*****
Wadhati aliyafurahia sana Maisha ya advance, mazingira yalikuwa Ni mazuri na yenye kuvutia Sana, "woooow kumbe sahivi navaa Shati la mikono mirefu agh" aliendelea na masomo yake vizuri alioneka mpole, msitaarabu na asie na mawaa na mtu wenzake walimpenda Sana, kwa juhudi zake na wepesi katika masomo. Wadhati akapa rafiki aitwae Dominicus ambae walitokea kupatana sana hivyo mda mwingi walikaa pamoja na kushauriana Mambo mbali mbali ya kimasomo na Maisha pia. Kwakua ile shule ilikuwa na chembe chembe za dini Wadhati akaamua kujiunga na Kwaya ili amutumikie Mungu kwa njia ya nyimbo, Wadhati alifanya vizuri pia aliimudu vizuri sauti ya tatu, Shokolo mwalimu wake wa Kwaya aliye kuwa akikaribia kuhitimu kidato Cha sita alimsifia na kumuahidi kumuachia gurudumu pale atakapo maliza.
Wadhati aliendelea kufanya vizuri hata katika uongozi wake, Kwaya yake iliweza kushika namba moja katika mashindano ya kuimba Miongoni mwa shule mbali mbali za ukanda ule, hivyo akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kanda. Sikumoja akiwa kahudhuria kwenye kikao Cha Kanda kujadili kuhusu mahafari mwenyekiti pamoja na viongozi wengine, Kama ulivo utaratibu wa vikao, ilipitishwa karatasi ya Mahudhurio ikiwa na sehemu ya jina, cheo na namba ya simu.
Lucier, Katibu wa kanda, tayari alikuwa kaisha vutiwa na Wadhati siku nyingi kila walipo kutana kwenye vikao, alitamani kumwambia Ila aliona aibu kwa kisingizio yeye ni mtoto wa kike hivyo angeonekana muhuni, Muonekano wa Wadhati uliwatesa mabinti wengi ustaarabu na utanashati aliokuwa nao uliwababaisha sana mabinti, hata wale aliowafundisha kwenye Kwaya walitokea kumpenda mno. Lucier aliendelea kumtazama Wadhati alivokuwa akifafanua hoja mbali mbali zilizokuwa zikitolewa na wajumbe. "Mmh mbona nateseka kiasi hiki na wepesi ninao hapa acha nikopi hii namba yake ya simu nimetokea kumpenda sana Ila naogopa kumwambia sijui Kama atanielewa huyu Kaka jamani anaugalagaza moyo wangu bila kujua ona alivo msafi, afu mpole kweli yani nikimpata ntakuwa nampeti peti naamini huyu atanifaa sio Kama Jack na Semi Mwee, walinichezea tu wakanikimbia dunia hii kweli hadaa walimwengu shujaa, mapenzi konyo hayajawahi kumuacha mtu salama acha nijaribu bahati yangu" Yalikuwa Ni maneno ya Lucier aliyekuwa akijisemea peke yake. Kikao kilipo isha wote wakarejea shuleni.