Chereads / MALAIKA WA UPENDO / Chapter 3 - SEHEMU YA TATU

Chapter 3 - SEHEMU YA TATU

Wadhati alifanikiwa kumaliza elimu ya Musingi na kwa bidii yake ambayo aliiwekeza kwenye Masomo alifauru kwa alama nzuri yeye na marafiki zake Jamari na Malinzi isipokuwa mtoto wa mjomba wake Bulaya yeye alikuwa mtundu Sana asiyependa kuhudhuria shuleni hivyo hakufanikiwa kufikisha alama Mia moja za kumuwezesha kujiunga na elimu ya sekondari hivyo akabaki mtaani na kujiunga na magenge ya vijana watukutu.

Ilikuwa jioni Wadhati anarudi kutoka kwa marafiki zake, Jamari na Malinzi. Akiwa njiani akawa anawaza moyoni,. Mmmh wanasema sekondari hakuna kiswahili lugha ya huko Ni Speak English kila Kona, hata sijui ntaongea nini siku nikienda ".. Wadhati alionekana Ni mwenye wasi wasi Sana huku mapigo ya moyo yakimuenda Kasi Sana, Kila lilipo muijia wazo la sekondari alikuwa akikosa furaha sana. Ntaongea nini Mimi sekondari? naogopa kuvalishwa pembe la ng'ombe Ila ntamwambia mama aninunulie kitabu Cha kujifunza lugha ya kingereza. Wadhati akafika nyumbani na kumusaidia mama yake kupika, wakati huo mama yake Juria akiwa hajarejea kutoka shamabani. "Wadhatii" Naam Baba.. Mama yako kaenda wapi? Ilikuwa Ni sauti ya Marandola baba yake baada ya kurejea kutoka vibaruani. "Bado hajarudi kutoka shamabani" haya njoo ujaribie hizi sale za shule kesho uende kuanza form one, Kisha akampatia madaftari aliyo yanunua pale dukani kwa Lomano, Wadhati akachukua Yale madaftari na zile sale zake na kuvipeleka chumbani mwake Kisha akarudi jikoni kuendelea kupika.

Julia anarejea kutoka shamabani "..Ehfuuu.. akishusha pumzi kwa uchovu huku akiegama pale mlangoni, jamani watu wa hapa mupo? "wakambaa njoo mwanangu niletee maji ya kunywa" Mmh, Wakamba nilishakwambia mie msinipimiege maji wanangu. Hebu nenda kaweke kwenye jagi ulete..

Eh, Wadhati unapika nini leo baba angu. "Napasha moto samaki waliobakia mchana. "Haya ukimaliza weka sufuria ya ugari ntakja nisonge mwenyewe" Marandola tayari alikuwa kashaenda misele Kama kawaida yake.

. Alufajiri na mapema siku ya jumatatu Wadhati tayari ameshaamka akiwa anafagia uwanja, Julia nae akaamka na kumwamsha mwanae Wakamba aoshe vyombo, yeye akachukua ndoo na kuelekea kisimani kuteka maji, "Shikamooo mama,. " Marahaba mwanangu umeamkaje..? Salama mama, Haya fanya upesi ujiandae twende shuleni, Mie naendea maji. Haya sawa Mama.

Wadhati akafagia upesi Kisha akaingia bafuni kuoga, Marandola nae akaamka Kama kawaida yake akaswaki vizuri na kuchukua vifaa vyake vya ujenzi na kuelekea vibaruani. Juria akarejea kutoka kisimani, Kilikuwa na kiporo cha wali kilichobakia Jana usiku akamchemshia mwanae. "Wadhati fanya upesi uje kula tuondoke mda umeenda sana. "Haya mama" Baada ya dakika tano Wadhati anatoka akiwa amevalia sale zake maridadi kabisa Suruali nyeusi na Shati akiwa na begi mgongoni.. Umependeza Mwanangu, Wadhati akatabasamu tu akaingia kupiga kiporo chake Cha wali.

"Sasa unaenda kuanza form one mwanangu, Uache michezo ukatulie kabisa usome nasikia masomo ya sekondari Ni magumu Sana na yameandikwa kwa lugha ya kiingereza, Sasa unatakiwa kuweka bidii ya hali ya juu Sana Mwanangu pia uzingatie Yale nilyokueleza hali yetu ya nyumbani unaiona sisi ni masikini hatuna sehemu yoyote ya kupata msaada tofauti na nyie watoto wetu. Ukasome kwa bidii badae uje utukomboe na sisi tutoke kwenye hii hali ya umasikini". Sawa nitazingatia yote ulionieleza.

Hatimae wakafika shuleni sehemu ya kuingilia pale getini kulikuwa na umbo la pembe tatu palikuwa na motto wa shule ambao unasomeka EDUCATION IS SHELTER zikiwepo na Sheria zingine mbalimbali za shule pamoja na maandishi mengine makubwa yaliyosomeka SPEAK ENGLISH, NO ENGLISH NO SERVICE. "unaona mambo hayo mwanangu.." Wadhati akasisimka kwa hofu hku akijisemea moyoni duuh kumekuchaaa. Kazi imeanza ntayaweza kweli haya Mimi duh,. hku mapigo ya moyo yakimuenda mbio kwa woga. Walipokelewa na mwanafunzi mmoja ambaye aliwapeleka hadi kwenye ofisi ya Head master kwa ajiri ya usajiri. Baada ya usajiri kukamilika Juria akamuaga mwanae na kurejea nyumbani kwa ajiri ya kuendelea na shughuli zake Kama kawaida. Wadhati akaoneshwa darasa lake na mwalimu "This Will be your class eeh".. Yalikuwa Ni maneno ya mwalimu Lucisa, Wadhati akiwa hata hajui ajibu nini kwa mwalimu basi akaelekea darasani kimya kimya alikooneshwa.

Wadhatiiii welikamu mai furendiii..." akipokelewa na marafiki zake ambao walimtangulia kufika shule wakionekana tayari washayazoea mazingira ya shule, wakampatia kiti na meza akakaa, akaja rafiki yake jamari ambaye alimuelezea utaratibu upoje Kisha akampatia notice ambazo wamesha andika nae akopi ili waende sawa. Mda wa break nao ulikuwa umewadia wote wakatoka nje, Wadhati na marafiki zake wakaanza kutembelea mazingira ya shule, Mazingira Yalikuwa Ni mazuri na yenye kuvutia Sana. Kulikuwa na 'round about' Kwenye paredi kila darasa walikuwa na sehemu yao kwa ajiri ya kupanga mistari. Break ilipoisha wote wakarudi darasani kuendelea na vipindi.

Madamu Sarafina, mwalimu wa civics akaingia darasani... "Hawa yuu class...., Guuuuuuud afternuuuuuuun maaaaaadam..! hawayuu....." wiiiii aaaaa faaaaaini senki youuuu maaaadam, "okey sit daun... We as sitingi dauni"ok wea did wi endedi in ze last piriod..? Wote walinyoosha mikono isipokuwa Wadhati aliyekuwa akishangaa shangaa tu haelewi chochote hata English course yenyewe nakuwa amesoma hivyo aliishia tu kuona mapicha picha darasani. Ghafla Madam Sarafina anashangaa kuona Ni mwanafunzi mmoja tu Kati yao ambae hajanyoosha mkono harafu Kama vile haelewi ni nini kinachoendelea wakati ule, Kwa kuwa Madam Sarafina alibobea kwenye mambo ya Saikorojia hivo bila Shaka alijua Kuna tatizo hapa mbona Hawa watoto niliwafundisha vizuri sana. Madam Sarafina akamfuata na kumuuliza, Why are you not responding my question..? Wadhati ameinamisha kichwa akiwa hata haelewi ajibu nini na Wala haelewi kinachoulizwa Ni nini.. Baadhi ya Wanafunzi walimcheka kwa kushindwa kujibu chochote. Pembeni alikuwepo Mwanafunzi mmoja alie kaa nae jirani,.. akamtetea, Exchuze Madam.. he iz a neywu Kama,... Ahahaaa okay, wati iz yua neim..? kimya! am tokin with yu gai, what iz yua neim? Unaitwa Nani? Ndiyo akaelewa Sasa; Wadhati Marandola. Madam Sarafina akaendelea kufundsha huku akiwatafsiria kiswahili ili waelewe zaidi akiwemo na Wadhati ambae ndio ilikuwa siku yake ya kwanza darasani.

Hiyo siku ikapita Wadhati akarejea nyumbani na kumwelzea Mama yake hali aliyokutana nayo, akamuomba amununulie kitabu Cha misamiati ya kingereza kimusaidie kujifunza lugha na hasa alipokumbuka Yale maandishi pale getini NO ENGLISH NO SERVICE hii ikamfanya Wadhati atamani kujifunza lugha ya kiingereza.