Ni hasubuhi na mapema katika Kijiji Cha Bustania kilichopo kasikazini mwa Thamalia, miale ya jua ilikuwa ikichomoza mithili ya pembe za faru zilizo chongoka Kama mshale, watu walikuwa wakiendelea na shughuri zao za Kila siku kwa ajiri ya kujipatia ridhiki na wengine mashambani. Marandola, anafungua mlango huku akipiga miayo...." Oooohuuuuuuuuuuh.. kumekucha. Wacha niswaki haraka haraka hapa halafu nikampitie manogele, twende tukamalizie kibarua chetu Cha ujenzi kwa Nsabi.... Akijisemea moyoni.
Juria, mkewe marandola, yeye huamka alufajiri kila siku kwa ajiri ya kuteka maji. Alionekana akitokea kisimani na ndoo ya maji kichwani, akafika na kuitua chini..efhuuuu.. ee baba angu wa mbinguni kifua hiki kitaniua mimi'... yalikuwa ni maneno ya juria baada ya kuitua ndoo yake kichwani, Kisha akaingia ndani. Baah,.! Mtoto huyu Bado amelala tu.! Mh hapana atakuja kuwa mzito sana ukubwani, baba yake nae Wala hata hajamwamsha jamani,....wadhati..wadhati...wadhatiiii..., Naaa-amh. Akaitika huku akijitafuna tafuna,.. Bado umelala tu Hadi Sasa hivi.?! hebu uamuke huko unawe uende shule utachelewa. Amka.! Wadhati akaamka na kumusalimia mama yake, kisha akachukua kalai na kutoka nalo nje Hadi kwenye ukoka ulopandikizwa na Babu yake Mzee Jombi, akamimina maji kwenye kalai akaosha kichwa, uso, mikono na miguu Kisha akatimua mbio kuingia ndani ili ajipakae mafuta, hakuchelewa akavalia sare zake za shule vizuri kisha akakimbia kwenda shule.
Wadhati alikuwa akisoma darasa la tatu, shule ya msingi Bustania iliyopo kijijini kwao hapo. Shule hii ilijurikana sana kwa jina maarufu ''Bust" kwa sababu ya kuwa na walimu wakali, hasa mwalimu Shunashu, ambae aliogopeka Sana na wanafunzi kwa kutoa adhabu Kali.
Marandola, baada ya kumaliza kuswaki, akaingia ndani na kuchukua vifaa vyake vya ujenzi Kisha akamuaga mkewe na kwenda kumpitia rafiki yake Manogele, wakaelekea kwenye kibarua Chao cha ujenzi kwa Nsabi. Nae Juria baada ya kumaliza kufanya usafi na kuosha vyombo. Akachukua jembe lake na kuelekea shamabani. Juria hupendelea sana kulima viazi kando ya ziwa, alikuwa Ni mama hodari aliemsaidiana Sana mumewe kwa chakula, Juria alikuwa akiivisha viazi vingi msimu Hadi musimu hivyo hawakupata tabu ya chakula, aliuza marando(mbegu za viazi) kwa wakulima wengine, ambao walihitaji mbegu kwa ajiri ya kwenda kupandikiza mashambani mwao.
Ilikuwa ya karibia saa tano na nusu asubuhi Juria akachimba viazi na kurudi navyo nyumbani kwa ajiri ya chakula Cha mchana, Wadhati atakapo rejea akute chakula kipo tayari ale awahi kurudi shule kwenye vipindi vya mchana.
Sakumi jioni Juria akaosha vyombo Kisha akachukua upanga wake na kwenda msituni kuchanja kuni. Wadhati nae alirejea kutoka shule akabadiri nguo zake za shule, Kisha akachukua ndoo na kuendea maji ziwani, akaoga na kwenda kucheza na marafiki zake Jamari na Malinzi waliokuwa wakisoma darasa moja. Saa kumi na mbili jioni, Juria anarejea kutoka msituni na mzigo wake wa kuni. Marandola nae anarejea kutoka kibaruani kwake. Pole mme wangu kwa uchovu..." Yalikuwa Ni maneno ya Juria hku akimpokea mumewe mzigo, Asante ndo wajibu wangu kupambana mke wangu.... huku akishusha pumzi ndefu ya uchovu.
Hebu niwekee Kwanza maji bafuni nioge, harafu ndo ntapa chakula. Basi Juria akampelekea mumewe maji ya kuoga bafuni. Kisha akamukaribisha kwa heshima zote, Ba. Wadhati karibu maji ya kuoga mumewangu.. Malandola akaingia ndani akachukua tauro na kuelekea bafuni,..
Makuti ya hiri bafu yameanza kuliwa na mchwa ngoja nitafte mengine japo sijui Ni lini.., Marandola alikuwa akijisemea moyoni. Wadhati anarejea kutoka kucheza,.
Heee! mbona umechafuka hivo mwanangu..?! Mama nilikua nacheza mpira. "Nilishakuzuia kugaragara kwenye vumbi hausikii kwanini... Unanipa kazi Sana kufua nguo zako we mtoto Ah". Yalikuwa Ni maneno ya Juria akiwa kaketi kwenye kigoda akichambua mchele., Chukua maji unawe hayo mavumbi haraka.
Marandola akatoka bafuni baada ya kumaliza kuoga he,.! Wadhati mbona umechafuka hivyo? "Shikamoo baba". Marahaba, huku akiingia ndani. Mmh,. Ma, Wadhati nilishakwambia huyu mwanao kaanza tabia ya kulanda landa mtaani, ona alivochafuka utazani alikuwa kalala kwenye jivu la tofari za choma... Juria Wala hakuyajari maneno ya mumewe maana alijua Ni kawaida ya watoto. Tayari alikuwa kaisha muandalia mumewe chakula mezani viazi, ufuta na maji baridi ya mtungini aliozawadiwa na Bibi yake Mariatabu kwa ajiri ya kuanzia Maisha siku anaposwa na Malandola.
Marandola baada ya kupata chakula akaenda zake misele Kama kawaida yake, alikuwa akipendelea Sana kwenda kupiga soga na rafiki yake wa karibu Sana Saluma, phamasia muuzaji wa madawa pale Kijijini Bustania. Saluma na Marandola Ni marafiki walioshibana Sana, wamekuwa wakishauriana juu ya maswala mbalimbali kuhusu Maisha hasa zaidi mmoja wapo anapokwama.
Wadhati.... Wadhatii... we wadhatiiii...., akiwa bize anacheza na mbwa. Hivi hunisikii? Naam mama, haya haraka njoo utoe vyombo mezani. "Haya mama nakuja''. Wadhati alijibu kwa furaha Sana alionekana mchangamfu Sana siku hiyo tofauti na siku nyingine akiutazama kwa kuibia ibia mchele uliokuwa ukichambuliwa na Mama yake, Ama kweli Alie uita ubwabwa cheka nawatoto hakukosea.
Juria alipenda Sana kukaa karibu na mwanae ili amfundishe kazi ndogo ndogo za nyumbani, kuosha vyombo, kufagia ndani na kuchanja kuni bila kujali Wadhati Ni Mtoto wa kiume. Aliyakumbuka Sana malezi aliyo lelewa na Bibi yake Mariatabu tangu akiwa na umri wa miaka mitatu tu, umri alionao kwa Sasa Wadhati. Kulikuwepo na watoto nane kwa Bibi yake pale wakiume watano na wakike watatu Ila wote waliokuwa wakifanya kazi sawa bila kujali jinsia, Kama vile kutwanga na kuchekecha unga wa Muhogo. Hii ilimpa nguvu Sana Juria kumfundisha Mwanae kazi aina zote na hata kupika.
Siku zikazidi kwenda Wadhati akazidi kukua akiwa karibu Sana na mama yake. Wadhati alipofika darasa la Saba, tayari alikuwa Kijana hodari na mchapakazi Sana, alikuwa kaisha fahamu kazi zote za nyumbani na shamabani. Juria alimsii Sana mwanae kusoma kwa bidii huku akimwelezea hali nzima ya Maisha yao ya umasikini jinsi wanavyohangaika na kupitia changamoto nyingi kuwa hudumia yeye na mdogo wake Wakamba ambaye alizaliwa Wadhati akiwa darasa la tano.
Hii ilimfanya Wadhati kupata Machungu Sana akabaki akijiuliza Maswali yasiyo na majibu kichwani mwake." Mimi bado Kijana mdogo sana, haya maneno anayoniambia mama yananiumiza sana nitasoma kwa bidii ili nije kuisaidia familia yangu." Wadhati alipata uchungu Sana juu ya yale maneno aliyoambiwa na mama yake hivyo aliweka bidii kubwa sana kwenye kusoma ili badae aje kuikomboa familia yao kwenye umasikini hasa baba yake aliyekuwa akitegemea vibarua vya ujenzi ilikupata kipato kwa ajiri ya mahitaji ya familia yake.