Siku ya Leo imekuwa ya furaha sana,matatizo aliyoyazungumza na Nzagamba yakiwa akili mwake lakini anaamua kuyapotezea kwa muda na kutumia wakati huu kufurahia hatua kumi za ushindi alizopiga kuelekea kugusa moyo wa Nzagamba " Nina uhakika sio mda mrefu atakuwa wangu,kimwili na kiroho pia,vumilia kidogo tu Tulya,ni kidogo sana tofauti na ulikotoka lakini sio sawa na unakoelekea,na safari unakoelekea hutakuwa mwenyewe na huo ndio uzuri wake" anajisemea Tulya akiwa amekaa nje kwenye kitanda akimsubiri Nzagamba arudi.
"itakuwa bado Yuko na marafiki zake" anawaza akiendelea kuangalia uelekeo wa njia atakayotokea Nzagamba akija nyumbani.Kiza kikiwa kimetanda tayari lakini kikiwa sio Cha kutisha sana kutokana na mwanga wa mwezi mchanga uliokuwa unaangaza ukichangiwa na nyota.
" mwanaume nimpendaye aliyeng'ambo ya mto,umbali wetu uliotenganishwa na kina kirefu Cha maji kilichojaa mamba na tope la kunasa nitampateje? yeye hawezi fanya juhudi za Kuja kwangu kwani Mimi ndie nitamfata kwani uzuri wake unaangaza kama mbalamwezi na kunivuta huku niliko ukiniita,na siwezi kujizuia moyo wangu na akili yangu vinazidi kutembea kwenda kwake,na nitavuka mto kwa ajili yake nitapambana na mamba kwa ajili yake,mwanaume nimpendaye aliyeko ng'ambo ya mto ni....."
Anaacha kuimba baada ya kumuona Nzagamba akiwa amesimama akimsikiliza
" umerudi" anaongea Tulya akipiga hatua kuelekea alipo utadhani asipoenda atarudi alikotoka.
" mmmh" Nzagamba anaitikia akimwangalia tabasam lake likiwa linaonekana kwenye mwanga huu hafifu.
" una sauti nzuri" anamsifia na Tulya anaangalia chini kwa aibu.
" Asante"
"Leo tuna lala mlangoni?" anamuuliza kwani Tulya alikuwa bado kasimama Mbele yake akimzuia njia.
" eee?!" anauliza Tulya macho yake makubwa yakimwangalia na inamchukua mda kuelewa anamaanisha nini.
" aaaa,lete nikupokee hiyo" anachukua ndege aliyokuja nao na kuanza kutembea kuelekea iliko nyumba ya Bibi sumbo.
" nikuletee chakula?" anauliza akimwangalia Nzagamba aliyekuwa anaelekea kwenye nyumba Yao, Nzagamba anasimama na kumwangalia." ndio" anaitikia na kumwangalia Tulya akitembea kuelekea nyumbani kwa mama yake lilipo jiko kiuno chake chembamba kilichoyabeba makalio yake vizuri na kuyafanya kujisukuma yenyewe kushoto na kulia.Anatikisa kichwa chake kufuta mawazo yake yalioanza kupita kichwani kwake.Ukweli ni kuwa alikuwa amefika mda mrefu lakini alisimama na kumwangalia Tulya aliyekuwa akiimba pasipo kujali kitu kingine duniani.macho yake yakiwa angani yakiangalia mwezi na uso wake uliojaa upendo kama mtu anayemwimbia anamuona huko juu ya mwezi na kilichomgusa zaidi ni kuwa wimbo ulikuwa unamhusu yeye.
" sijawahi kuisikia" anamuuliza Tulya ambaye kwa wakati huu amepiga magoti akimnawisha mikono yake.
" ehh?!"
" nyimbo,sijawahi kuisikia" Tulya ananyanyuka na kuweka kipeo pembeni.
" karibu chakula" anamkaribisha na kurudi nyuma akienda kukaa mbali kidogo wakiwa wanatazamana.
" asante" Nzagamba anaanza kula.
" ni nyimbo maarufu sana kijijini kwetu,wanapenda kuiimba kwenye ngoma namaanisha harusi"anamjibu akicheza na vidole vyake.
" mmmh" anaitikia akiendelea kula.
" ukweli ni kuwa nilikuwa siipendi,nilikuwa naona ni ujinga,siwezi kuvuka mto wenye mamba kwa sababu ya mwanaume nilikuwa nikisema aliyetunga alikuwa kachanganyikiwa" anatulia kidogo na kumwangalia Nzagamba.
" Sasa naelewa alikuwa anamaanisha nini" anaendelea kuongea na kumfanya Nzagamba ashindwe kumeza chakula chake mdomoni na macho yake makubwa yalikuwa hayasaidii hata kidogo,inakuwaje mwanamke anakuwa Hana aibu namna hii na Leo atakuwa na mpango wa kunifany nisilale kabisa anawaza Nzagamba.
" Niko radhi kuvuka mto kwa ajili yako Nzagamba" anaongea na kurudisha macho yake chini baada ya kuona inakuwa ni vigumu kushindana naye mashindano ya kuangaliana.
Nzagamba anaendelea kula asijue aseme nini,moyo wake ukienda mbio na tumbo lake likijitahidi kuhimili uzito wa chakula linalopokea simu ya Leo ukweli ni kuwa alikuwa ameshiba na alikuwa anajilazimisha tu kula Ili atumie mda kidogo na Tulya.Anamaliza kula Tulya anatoa vyombo na kuvirudisha nyumbani kwa Bibi sumbo anarudi hamuoni Nzagamba nakujua ameenda kuwafungulia mbwa.
Anachukua ngozi na kuanza kumtandikia sehemu ya kulala wakati anamalizia Nzagamba nae anaingia na kumuona akitandika anafunga mlango na kugeuka kumwangalia.
" tayari" anaongea Tulya akisimama na kusogea pembeni na kusimama, Nzagamba anabaki akimwangalia tu.
" usiku mwema" anaaga Tulya na kumkimbilia chumbani kwa mwendo wa haraka Kama katoka kuiba asali ya Babu.
" hiki nini?" anajiuliza Nzagamba akishangaa bado anatandikiwa chini baada ya Yale yote yaliotokea leo.akisahau yeye ndie alisema apewe mda atalala sebeleni.
" kwa nini asiseme tu nalala chumbani leo" analalamika Tulya akijitupa kitandani.
" baada ya kujitoa kote kule bado mgumu tu,mwanaume gani huyu?" anaongea Tulya akijivuta mabuti yake kichwani.Tulya aliyekuwa akitandika ngozi kwa kumtega Nzagamba akitumaini kuwa atasema atalala chumbani hakujua kuwa mwenzake anamsubiri mwaliko.
Baada ya mahangaiko ya mda mrefu atimaye lepe la usingizi linamchukua Tulya uso wake ukiwa na tabasamu akili yake ikirudia matukio ya Leo hasa kumbato ambalo alimpa Nzagamba japokuwa hakulirudisha anashukuru hakumsukuma kama ana ukoma, lakini ndoto yake inabadilika ghafla na kujikuta yupo sehemu nyingine tofauti kabisa.
Tulya anajikuta ndani ya msitu mnene tena Hali ya hewa ikiwa ni ya baridi na miguuni pake akiwa hana kiatu anapiga hatua na miguu yeke inakutana na unyevu " mvua imenyesha?" anajiuliza Tulya akishangaa kwani wakati anaenda kulala ilikuwa ni kiangazi masika haya imekuwaje na inavyoonekana mvua imetoka kuonyesha sio mda.
" hii ndoto tena?" anajiuliza akiendelea kupiga hatua akiuangalia msitu na kuona ni uleule." siipendi hata kidogo kwa nini inanijia?" anajiuliza.
Anapiga hatua na kuona miale ya moto anaanza kutembea kuifuata kwani tayari alishajua ndoto itaishia wapi.
Anafika na kuwaona wanaume walewale wakiwa wamemlaza mwanamke ambaye kwa sasa ameshamjua kama ni Ndesha akiwa amelala juju ya jiwe na kisu kikiwa kifuani kwake.Tulya anapiga hatua karibu walipo safari hii akitaka kujua ni nini hasa kinaendelea pale, akijua hawawezi kumuona na akijua ni ndoto tu anaamua kusogea karibu kabisa.
Anamuona Ndesha akiwa ni mdogo sana umri kama wake na ni mrembo sana lakini Cha ajabu ni kuwa kile kisu kilichopo kifuani kwani hakijamuua bado yupo hai lakini akipumua kwa shida damu ikiwa imetapakaa kwenye mavazi yake na kile kisu kikiwa ni chekundu kama makaa ya moto.Mwili wa Tulya unasisimuka kwa maumivu aliyokuwa akiyapitia Ndesha.
Ndesha anaendelea kutupa kichwa huku na kule asitikise mwili wake,baada ya muda Tulya anaona Moshi mweupe ukiwa unatoka sehemu kilipo kisu.
" tayari" anaongea mwanaume Mmoja ambaye Tulya alishamtambua kama ni kiongozi wa tukio hili ama ni kiongozi wa wale wanaume wawili au aseme ana nguvu kuliko wengine eneo lile.
" lete mkono wako" anamwita mwanaume aliyevalia mavazi kama mtemi naye anasogea na kumpa mwanaume huyo mkono wake kisu kinaletwa,wanakata kiganja Cha mkono kiasi Cha kutoa damu,wanachukua mkono huo unaotoa damu na kuupeleka karibu na kilipo kisu damu inaangukia na kumfanya Ndesha kupiga makelele kwa maumivu.
" oooh mizimu,tambiko la aina gani hii?" anajiuliza Tulya mkono wake ukiwa mdomoni kama kuzuia asipige makelele au asitoe hata pumzi." Ni watu wa aina gani hawa?ni wa katilli hata mnyama huwezi kumfanyia hivi" anawaza Tulya machozi yakimtoka na kumuona huruma Ndesha.
" najua uko hapa nisaidie" anaongea Ndesha kwa maumivu machozi yakimtoka.
Tulya anamwangalia asijue anaongea na nani anaangalia huku na kule asione mtu mwingine wa kutoa msaada kwani walioko pale ni wale wanaume katili tu ambao kwa sasa walikuwa wakiendelea kunuia maneno ambayo Tulya alikuwa hayaelewi.
" anaongea na Mimi au?" anajiuliza Tulya akiangalia huku na kule tena kuhakikisha Kuna mtu mwingine lakini baada ya kurudisha macho yake kwa Ndesha anakutana nae uso kwa uso akimwangalia.
" nisaidiee,inauma sana" anaongea Ndesha kwa shida machozi yakimtoka na macho yake yakiwa kwa Tulya.
" na wewe upo kama Mimi,nakuomba unisaidie"
" ananiona!" anaongea Tulya macho yakimtoka pima kama kadodosha tone la maji baharini na analitafuta.