Chereads / penzi la bahati / Chapter 49 - chapter 48

Chapter 49 - chapter 48

Baada ya Tulya kuondoka pasipokusema kitu chochote, Nzagamba alihisi kuchanganyikiwa akili yake ilikuwa inapiga makelele kitu kimoja tu " Sasa atamuacha" hata wazo tu lilikuwa linamfanya ahisi kufa je,ikitokea kweli atafanyeje.Ikiwa ni ngumu kukubaliana na ukweli lakini alicho kitambuwa kwa wakati ule ni kuwa Tulya akiondoka hawezi kuishi ana uhakika mkubwa kuwa atakuwa Hana kitu Cha kumshika kama hapo awali kwani maumivu aliyokuwa anayahisi kutokana na wazo tu la kuachwa na Tulya yanagawanya moyo wake.

Alijaribu kulala lakini hakufanikiwa hata kidogo aibu iliyokuwa inamsubiri kwa mara nyingine tena ilikuwa haipo akilini mwake kabisa kwa sasa alichokuwa anakitaka kujua kwa sasa ni Tulya anawaza nini,potelea mbali aibu yake kwani itakuwa mara ya kwanza kupitia jambo kama hilo imeshajirudia na kujirudia mara nyingi ingawa haizoeleki lakini siyo sawa kama akimpoteza Tulya.

Hawezi kukuacha anakupenda kumbuka ameolewa na wewe pamoja na shida zako na alisema atakuwepo hapa milele unakumbuka? nafsi yake inampa ushauri na anakubaliana nayo.Hapo alikuwa hajajua nini maana ya aibu ila kwa sasa imeshabisha hodi mlangoni kwake unafikiri ataikaribisha,Nina uhakika atafunga mlango na kuziba nyufa kabisa isipenye hata kidogo. akili yake inamkumbusha na anajikuta katika vita kati ya akili na moyo usiku mzima.

Hawezi kuhesabu ni mara ngapi aliamka na kutamani kuingia chumbani akamuulize anachokifikiria kwani anajua hajalala kutokana na kelele za kitanda mara kwa mara zikionyesha anavyogeuka kitandani.lakini akili yake inamwambia aache kwani ikithibitishwa kuwa kweli anataka kuondoka au anaweza kumpatia wazo hilo je ataweza kuhimili matokeo yake hivyo anarudi.wakati mwingine akiamka moyo wake unamwambia kwani humuamini hukumbuki alichokwambia kuwa atakuwa na wewe mda wote ukienda kumuuliza utavunja moyo wake.Hajui alipigana na vita hii mpaka saa ngapi lakini alilala akatulia mara tu baada ya kutokusikia sauti za kitanda na kujua kuwa Tulya amelala.Lakini hakuweza kulala hata kidogo kulikucha akiwa macho na aliposikia Tulya akitoka chumbani alijifanya amelala.

Baada ya Tulya kutoka alifanya maamuzi ya kubeba silaha zake Kuja kuzifanyia mazoezi kwani ana miaka minne Sasa hajashika upinde,sime,mkuki wala kitu chochote kile kinachoitwa silaha ya kivita.Hata kama hawezi kuwinda mnyama sio vibaya akiwa tayari kwani huwezi jua hatari itafika mda gani akiwa porini,kwani atake asitake kesho lazima aende porini.

Baada ya kufika na kuanza kufanya mazoezi anajikuta akifanya kwa bidii akiwaza kuhakikisha anawinda na kurudi na mnyama hata Mmoja apate ngozi amtengenezee mke wake nguo moja hasa sketi nzuri itakayo mkaa vizuri kwenye kiuno chake hasa akicheza,ukisema kucheza anakumbuka siku aliyomkuta nyumbani kwa Mzee nshana akicheza na kujisemea mkewe anajua kucheza.Aliendelea kulenga mishale na kujisahau kuwa udhaifu wake hautokani na kutokujua kutumia silaha Bali unatokana na yeye mwenyewe.

Na mara akafika mwanamke huyu wa ajabu aliyeingia maishani mwake kama kimbunga na Sasa anasomba vitu vingi,aliposikia sauti yake aligeuka na kumwangalia mapigo ya moyo wake yalitulia kwa mda baada ya kuona tabasamu usoni kwake lakini aliamua kupuuzia na kuendelea na kazi yake akijua mawazo wakati mwingine hudanganya na kukuletea vitu visivyo halisi mpaka aliposikia akipiga makelele na pasipokujua alijikuta akitupa upinde wake na kukimbia alipo uzuri hakuumia,kwani bado alikuwa na nguvu za kugombana na kisiki.

Alichokijua ni kwamba anamjali,amekuja na chakula na anajua kuwa hajala tangu jana,mwanamke kaja na nguvu mpya sura ikiwa na tabasamu utadhani hawako kwenye matatizo tena ni imara Simba jike anayelala na kuamka Kila siku na ari mpya kuliko jana, kupambana na kitakochokuja kwake siku ya leo akiisahau jana mwanamke asiyewaza kesho yake wakati wote anathamini Leo yake akihakikisha watu wanaomzunguka wako salama.

Hajui tu alimpatia furaha ya aina gani alipo mshika mkono na kusema kaja kukamilisha upungufu wake kwani sio Siri kaumiliki upungufu huo mpaka wakati mwingine anajisahau yeye ni nani kama Sasa alipokaa chini ya mti akimwangalia msichana mwenye macho makubwa na ngozi laini,shingo ndefu, nywele...nywele ni mabutu ambayo yameanza kufumuka lakini bado yanampendeza. oooyaa kwendaraa laana na laana yake kwa wakati huu anachokitaka ni kumkumbatia na kunusa ile harufu nzuri kama udongo afanye vitu vingi naye akili yake yote ijue neno Nzagamba tu na yeye mpaka akolee lakini Hana uhakika kama atatosheka Anawaza Nzagamba akiendelea kumwangalia Tulya.

" Nini kimekufanya useme nimekimbia?" anashtuliwa kwenye mrolongo wa mawazo yake na Tulya liyekatisha Hadi wazo lake la kumkumbatia alilotaka kulitekeleza.

" mmmh" anakohoa kidogo kwani anauhakika angeongea hivihivi sauti yake ingetoka kwa mkwaruzo.Sio kama alikuwa anataka kumuuliza swali lile lakini upande wa moyo wake ulitaka kujua Tulya alikuwa anawaza nini jana alipokimbia chumbani hivyo akajikuta anauliza tu na swali lake la awali alimuuliza akitaka kujua msimamo wake katika Hali hii walionayo.

" hukutaka kuongea" anamjibu akiangalia Mbele akiona aibu kwa mawazo yake kwa pembeni anamuona Tulya akitabasamu kidogo.

"ukweli ni kuwa nilikimbia" Tulya anaongea na Nzagamba anamwangalia kwa mshtuko.

" Nilikimbia kwani sikutaka kulia Mbele yako na kingine nilijisikia vibaya kwani wakati unanihitaji sana na Mimi nilikuwa sina Cha kufanya kuzuia maumivu uliyokuwa unayapitia nilitamani niyachukue yawe mabegani mwangu na kuyatupa mbali lakini haikuwezekana ndio maana nikakimbia" anaongea Tulya akiangalia mikono yake iliyokuwa kwenye mapaja.

Mwanamke hashindwi kunishangaza huyu anawaza Nzagamba akimwangalia.

" Niliamua kuwa mbali kwa mda Ili nikipata ujasiri nije kwako na asubuhi ya Leo nimeupata na Sasa niko hapa"

" ulikuwa wapi?" anamuuliza na Tulya ananyanyua uso wake na kumwangalia macho Yao yanakutana kimya kifupi kinapita wakitazamana.

" hapa" anamjibu akinyanyua mkono na kuweka kiganja chake kwenye kifua Cha Nzagamba kilicho wazi kutokana na kuvaa rubega,kiganja chake kinatua sehemu ulipo moyo wake na kufanya moyo wa Nzagamba utake kutoka kwenye jela lake la mbavu na kutoka nje ujitangaze kuwa upo huru.

" ulinipatia ujasiri Nzagamba,baada ya kujua kuwa umeondoka na Kuja mazoezini nikatambua wewe ni jasiri sana,hurudishwi nyuma wala kutishwa na Hali yeyote ile,ni jinsi gani umekuwa imara na wewe hulijui hilo hivyo nikaamua Kuja nikikimbia nipate kukwambia hivyo" anatulia kidogo macho Yao yakiwa bado yamekutana pasipo kupepesa na mkono wake ukiwa bado kifuani.

" wewe ni imara na jasiri sana mtu asikwambie tofauti,na kama mtu akikwambia tofauti na nilivyosema Mimi mwambie kuwa mke wangu kasema ninajiweza"

Anapepesa macho yake anaondoa mkono wake kifuani kwake kwani amemaliza alichokuja kusema lakini Nzagamba alikuwa hajamaliza anamshtukiza kwa kumvuta mkono wake ule uliokuwa kifuani kwake na kumkumbatia kwa nguvu zake zote,kumbato lililokuwa linaeleza mengi kwani moyoni anasema hawezi kumwachia hata iweje,ni mjinga tu angemwacha mwanamke kama huyu aondoke na yeye sio mjinga hata kidogo.

Na Sasa hata yeye mwenyewe Tulya aseme anaondoka hawezi kumwacha aondoke kwani yeye ndiye ameyataka haya yote aliyemwambia avunje ngome yake aliyojenga kwa miaka mingi ni nani? ni mara ngapi ameweka mimpaka kati yao lakini Kila mara alivuka na kujisogeza kwake, Sasa hataondoka atabaki hapa milele kama mke wa Nzagamba atake asitake.

Tulya anahisi mapigo yake ya moyo yakikimbia kama yanakimbizwa na chui,kumbato la Nzagamba limekuwa la kushtukiza kwani hakutarajia kukumbatiwa.Na baada ya muda anaanza kuhisi pumzi zake zikikata anakuja kugundua ni kwa sababu Nzagamba amemkaba sana,anaanza kujitikisa Ili apate ahueni ya kupumua lakini Nzagamba anahisi kama anajaribu kukataa kukumbatiwa na yeye anazidi kukaza mikono yake.

" Nzagam..." anaita kwa shida lakini Nzagamba anakereka kuwa Tulya hataki kukumbatiwa na yeye na kingine maziwa yake yanajigusa kwenye kifua chake na kuamsha hisia nyingine tofauti za mwili wake ambazo amekuwa akifanya kazi kubwa kuzizuia tangu usiku ule walipoanguka sebuleni.

" shiiiiiii" anamwambia akizidi kusogeza uso wake kwenye shingo yake na kunusa ile harufu yake adimu inayopatikana kwa mwaka mara Moja tu inayomfanya atake kumtafuna.Akimwambia mtu kuwa mkewe ananukia kama udongo anajua atamcheka au atamwambia ni kwa sababu ni mfinyazi anashinda mda mwingi na udongo lakini anachokinusa yeye sio hicho na Bora ibaki kuwa Siri yake tu kwani hawezi kuelezea.

" siwe....zi kupu..mua" anaongea Tulya kwa shida.

" mmmh?" Nzagamba anamuuliza

" siwezi..ku.." kabla hajamaliza Nzagamba anamwachia na kumwangalia usoni Kisha anamuona akivuta pumzi kwa pupa.

" vipi uko sawa?" anamuuliza kwa wasiwasi Tulya anaitikia kwa kichwa kukubali lakini Nzagamba hamuamini.

" hauko sawa,mbona una hema namna hiyo?" anamuuliza wasiwasi ukiongezeka.

" ulinikaba sana"

" ehhh?"

" ulinikaba sana" anaongea Tulya akitabasamu

" aaah" anaitikia Nzagamba baada ya kuelewa.Tulya ana angalia chini kwa aibu na Nzagamba anazidi kumwangalia Hali inayomfanya Tulya aone aibu zaidi mapigo yake ya moyo yakienda kasi yakichanganyika na furaha asiamini kuwa Nzagamba amemkumbatia.

Anameza funda la mate kwani anahisi koo lake limekauka na kitendo hiki Nzagamba anakiona vizuri anafuatilia msafara wa mate kwenye shingo yake na macho yake yanaenda kwenye kifua kilichokuwa kina panda na kushuka wakati akipumua anaangalia saa sita yake na kukumbuka namna ilivyokaa vizuri kwenye mkono wake siku amemshika pale sebuleni mkono wake unawasha kutaka kwenda kushika tena na kuyahisi,macho yake yanarudi usoni kwa Tulya na kukutana na mboni kubwa mbili zikimwangalia

Wanatazamana kwa mda Tulya anatoa ulimi wake na kulamba lipsi zake za chini kwani anahisi zinakauka asijue ni kwa upepo unaovuma nje au kwa pumzi zinazotoka ndani.Huyu mwanamke najaribu kujizuia naona ananichezea anawaza Nzagamba na wakati huo huo Tulya anataka kutoa macho yake kwake aangalie kwingine lakini Nzagamba hakumwacha kwani sekunde ile ile mkono wake ulienda shingoni kwake huku dole gumba yake ikifika kwenye taya kumzuia asigeuka macho Yao yanakutana tena na pasipokumwacha Tulya ajue nini kinatokea Nzagamba anakutanisha midomo Yao.