Tulya Hana uwezo wa kuendelea kutazamana machoni na Nzagamba anahisi macho yake yanamwona mpaka maini hivyo anaamua kuangalia pembeni, lakini anashtushwa na mkono wa Nzagamba shingoni macho yake yanarudi kwake na kabla hajajua kinachoendelea mdomo wa Nzagamba unatua mdomoni mwake na kumfanya ahisi roho yake inamuacha. mwili wote unamganda akili yake nayo inazima macho yake yanaanza kuona Giza mazingira aliyeko yakianza kupotea kidogo kidogo.
Taratibu joto la mwili wake linaanza kupanda kama mtu kakoka moto kuanzia vidole vya miguu yake na Sasa umeanza kupanda kuelekea kichwani, huku joto hilo likichanganyika na hisia ambazo hawezi kuzielezea.
Anafumba macho yake nakuendelea kuhisi mabadiliko wakati Nzagamba akiendelea kucheza na mdomo wake macho yake akiwa ameyafumba asiamini kuwa duniani Kuna kitu kilaini tofauti na siagi na kitu hicho ni lipsi za Tulya zinazomtamanisha kuzitafuna, ingekuwa ni chakula anauhakika hata kama Kuna mtu angekuwa anakufa njaa Mbele ya macho yake angemwacha afe tu kwani hataki kuchangia anachokipata Sasa hivi na mtu yeyote hiki ni Cha kwake tu.
Kutokana na mawazo yake yanayopita kichwani kwake anajikuta akimng'ata kidogo lipsi yake ya chini nakumfanya Tulya kutoa sauti mdogo ya maumivu ambayo haikusikika kwani Nzagamba alitumia nafasi hiyo kuingiza ulimi wake mdomoni kwa Tulya,na kukutanisha ndimi zao mkono mwingine wa Nzagamba unaenda kiunoni kwa Tulya anamvuta na kumsogeza mpaka vifua vyao vinakutana.Mkono wa Nzagamba unaendelea kuzunguka mpaka upande wa pili nakuhisi ni jinsi gani kiuno chake kilivyo chembamba kama nyigu.
Anaendekea kumbusu na busu likiwa ni la njaa ya mda mrefu.
Anaacha kumbusu baada ya kuhisi Tulya anakosa pumzi anafumbua macho na kumwangalia Tulya anayevuta pumzi kwa haraka haraka pasipo kufungua macho yake anakutanisha tosi zao mkono wake unaondoka kiunoni na kumshika uso wake kwa mikono yote miwili akipapasa mashavu yake kwa kutumia dole gumba, anafumba macho yake akivuta harufu ile adimu ambayo kwa sasa amekuwa akitamani hewa ingekuwa imetapakaa harufu hiyo kote Ili awe anaivuta mda wote ama angekuwa na uwezo angeiweka hata mfukoni awe anatembea nayo kokote anakoenda hiyo ikiwa ni kwa ajili ya usalama wa afya ya mwili wake.
" ohh Tulya" anaongea kwa sauti ya chini inayotoka kwa shida kinywani mwake kwani maumivu yanatoka katikati ya miguu yake yanamuua na ni zaidi ya Yale aliyoyapata jando, kiumbe chake kikilalamika kuachiwa huru kipate kufanya kazi yake.Baada ya kuona mapafu ya Tulya yamepata hewa ya kustahimili kwa sekunde kadhaa zijazo midomo yake inatua mdomoni mwa Tulya tena na ikiwa na kiu mara tatu ya awali, kwani kwa sasa anahisi kama mtu aliyeachwa jangwani na hatimaye kapata maji.
Tulya anahisi mwili ukikosa nguvu na anauhakika angekuwa amesimama angemomonyoka na kuanguka chini,mwili wake unaendelea kupata hisia mchanganyiko na ukimsukuma kwa mahitaji yake pasipo kujua anajikuta akijisogeza zaidi kwa Nzagamba na kufanya vifua vyao vinavyogusana kusuguana na kufanya sauti za miguno kutoka kwenye midomo Yao wote wawili.Tulya anafumbua mdomo wake na kuchukua lips ya chini ya Nzagamba na kuinyonya akijaribu kurudisha busu lake Hali inayofanya kukatika kwa kamba iliyokuwa inashikilia uvumilivu wa Nzagamba.
Baada ya kuona Tulya anarudisha busu lake Nzagamba anagusa ulimi wake kwenye meno ya Tulya naye anamuelewa kuwa anaomba nafasi anafungua mdomo wake na Nzagamba anatumbukiza ulimi wake mdomoni kwake akikutanisha ndimi zao nakuanza kuzichezesha akifanya miili Yao kuwa katika msukumo mkubwa wa kumhitaji mwingine zaidi.Hata kama Nzagamba hajawahi kuwa kimwili na mwanamke sio kwamba hajawahi hata kumbusu mwanamke, ni anauzoefu mkubwa sana kwani yeye na marafiki zake walikuwa wakienda kwa wanawake mbalimbali kuimarisha uwezo wao kama wanaume lakini Nzagamba hakuwahi kupata ujasiri wa kuendelea zaidi ya busu tu.
Wanawake wengi walikuwa wanataka kuwa kitanda kimoja na yeye hapo zamani kabla Hali yake haijabadilika lakini mara nyingi hata afanye maamuzi kiasi gani akifika chumbani alikuwa anakosa msukumo huo na anajikuta akiishia kumbusu na kutafuta sababu ya kuondoka.Ikija kwa Lindiwe alikuwa akitoroka lindo na marafiki zake anaenda na kuonana nae mara nyingi na mara zote alimbusu tu hakutaka kuendelea zaidi ya hapo nakuamua kusubiri mpaka siku ya ndoa Yao kwani alimpenda na kumfanya wa tofauti. Hakutaka kumuonyesha matamanio ya mwili wake aliona huo sio uanaume haraka ya nini wakati akimuoa atakuwa wake milele hivyo hakutaka kufanya chochote licha ya dalili zote za Lindiwe alizomwonyesha Kila walipokutana kuwa anamuhitaji kimwili alimkwepa na kujifanya hamuelewa.
Na Sasa kinakuja hiki kimbunga Tulya kinachomsukuma kufanya dhambi hata ajizuie namna gani bado uvumilivu wake unatishia kuyeyuka mara nyingi Kila anapokuwa karibu yake na kumfanya ajiulize ile nguvu aliyokuwa akiitumia kuwakatalia wanawake wengine imeenda wapi?na sio kama hao wanawake walikuwa wabaya la hasha kama Lindiwe mwanaume yeyote akimwangalia anatamani kumtupa kitandani na kumaliza haja zake zote lakini aliweza kujizuia pasipo kutoa jasho.Lakini kwa huyu mwanamke ni kama barafu na Tulya ni joto Kila akiganda na kusema hayeyuki lakini akimsogelea tu anayeyuka.
Anakumbuka mwanamke huyu ndiye wa kwanza kumfanya aote ndoto za kumwaga ukubwani baada ya kuvuka kipindi Cha balehe.Siku aliyokutana na Tulya kwa mara ya kwanza mtoni na kumkuta akigombana na Manumbu usiku ule alilala na kuota akiwa naye kitandani kwake na alipoamka hakuamini kwani hata kama alimpenda Lindiwe kiasi gani hajawahi kumuta namna ile na kipindi hicho alipuuzia akijifariji kuwa matamanio ya mwili wake yatakuwa yameeongezeka yalimsukuma na jinsi alivyokuwa anamchukia hakuona haja ya kulifuatilia zaidi.
Lakini Sasa anaona huyu mwanamke anamfanya ajiulize kama yeye ndiye mmiliki wa huu mwili au Tulya namna anavyoupelekesha wakati mwingine anajipa nasaha kuwa mwili unamhitaji kwa sababu ni mke wake na utakuwa umechoka kukaa pasipokutimiziwa mahitaji yake muhimu hivyo unahitaji kitu upate kukata kiu yake lakini Leo amejua kuwa huyu mwanamke ni kama sumaku inayomvuta hata agome kiasi gani Kuna kitu kinachomvuta aende kwake atake asitake na hajui ni kitu gani na kinamfanya achanganyikiwe.
Wanaendelea kubusiana Kila mtu akiwa amepotea katika hamu ya kuwa na mwenzake.Tyulya anampiga Nzagamba kifuani baada ya kuona pumzi zake zikikata lakini Nzagamba hakuwa kwenye Hali ya kumwachia Tulya anaendelea kumguza bega na inamchukua kama Karne Nzagamba kuvunja busu.
Tulya anavuta pumzi haraka haraka mapigo yake ya moyo yakimwenda mbio anafumbua macho yake na kumwangalia Nzagamba na macho Yao yanakutana wanatazamana macho Yao yakiongea mengi zaidi kwani yanaonyesha ni jinsi gani Kila mtu anamuhitaji mwenzake.
Nzagamba anakamata midomo ya Tulya tena na kumbusu kama kesho hatakuwepo tena au atayeyuka sekunde inayofuata na hata muona tena mwili wake ukichemka.Tulya anarudisha busu kadri ya uwezo wake na baada ya muda midomo ya Nzagamba inaondoka mdomoni kwa Tulya na kwenda kwenye shingo yake ukiacha mabusu akielekea kifuani kwake, mkono wake mwingine ukienda mgongoni kwake na kumshika vizuri mwingine anamshika bega ukimsukuma taratibu Tulya naye anatii na kulala chini macho yake akiwa ameyafumba akiendelea kuvuta pumzi haraka haraka wakati mwingine akihisi hewa haifiki kwenye mapafu,haelewi anajisikiaje kwani chochote anachokifanya Nzagamba anakihitaji zaidi anajikuta mkono wake ukienda kichwani kushika nywele zake na kumkandamiza kama kumwambia aongeze kasi.
Nzagamba anakaa juu ya Tulya akiendelea kumbusu shingoni mkono wake Mmoja ukiwa chini kuzuia kuweka uzito wote juu yake,mdomo wake unarudi na kuchukua tena lipsi za Tulya mkono wake mwingine ukienda na kushika ziwa lake Moja na kuanza kulikanda na mguno wa kuridhika na alichokishika unamtoka mdomoni kwake anavunja busu mdomoni na kurudi kumbusu shingoni na Tulya anatupa kichwa chake nyuma kumwachia nafasi zaidi mkono wa Nzagamba unaendelea kucheza na ziwa lake.
"Nzagamba"
Anamwita kwa sauti ndogo inayotoka katikati ya pumzi zake na Nzagamba hasemi chochote kwani sauti hiyo inampa juhudi za kuendelea zaidi na alipofikia hawezi kurudi nyuma tena hata kama mazingira hayaruhusu kwani Leo ameamua kuonja asali hata kidogo tu.Hata kama aseme ajizuie anajua hana jeuri hiyo liwalo na liwe.