"unataka nini Mkita" anamuuliza tena maana jinsi Mkita anavyomwangalia anatamani angekuwa sisimizi Ili amfikiche kwa kidole labda hiyo ingesaidia kutoa tabasamu lake hilo usoni.
Lakini Mkita kama Mkita pasipo kujali anaendelea kumwangalia na tabasamu lake pasipo kufifia.
" niseme tu ukweli Manumbu anajua kutumia mikono yake vizuri,unaweza kuonyesha meno yako nikusaidie kuhesabu unaweza kuwa na pengo halafu wewe hujui" Anaendelea kumchokonoa na kwa sura anayoipata anauhakika kero imemfika moyoni.
" acha na uondoke,unaona raha au?" anabwata Lindiwe akitamani kumpiga na kibuyu kama angekuwa na Cha akiba nyumbani ni uhakika angempiga nacho ni jinsi gani bahati ilivyo upande wake anawaza Lindiwe.
" wewe ndio unatakiwa kuacha" anaongea Mkita tabasamu lote likiwa limefutika ghafla na uso wake ukiwa ni uso wa kazi .
" unajaribu kufanya nini?" anamuuliza Lindiwe anamwangalia asijue anamaanisha nini.
" sikuelewi, unataka niache nini?"
" sijawahi kukutana na mwanamke mbinafsi kama wewe Lindiwe,huna aibu,unajithamini wewe tu,vipi unajutia uamuzi wako eeeh!" anamuuliza hasira zikimpanda Mkita.
" sielewi unazungumzia nini?" anauliza huku akitetemeka akijaribu kujiweka sawa.
" Najua unanielewa vizuri sana Lindiwe,Baada ya kumtelekeza mwenzio wakati anakuhitaji sana,ukageuka hukuona hata haja ya kumsalimia ukawa unampita kama ana ukoma unajua alikuwa na msongo wa mawazo kiasi gani?" anafoka Mkita kama watu wangekuwa wanamezwa na macho Lindiwe angekuwa hata kidole hakionekani lakini hata hivyo kwa jinsi anavyomchukia Kuna uhakika asingekaa tumboni mda mrefu angemtema kwa kichefuchefu .Ukweli ni kuwa baada ya matatizo ya Nzagamba,Lindiwe ndie aloyeacha kumsalimia mwenzake akimpita kwa maringo.Kipindi ndoa yake bado mpya akipendwa na Manumbu alikuwa akitembea na kujitapa kwa madaha yote akiyapatia maisha.
" Mimi ndio Lindiwe bwana Nina staili kilicho bora,nitaolewaje na mtu mwenye mkosi kama yule,unajua hayo maisha oohh! sitaki hata kuyafikiria itakuwa ni ndoto mbaya inayokung'ang'ania huwezi hata kuamka"Anaongea Mkita akimkumbusha maneno yake Lindiwe.Lindiwe anabaki akimwangalia kwa mshangao asijue Mkita kayasikia wapi.
"unashangaa!hivyo ndivyo ulivyosema na Sasa inakuwaje unaanza kurudi kwenye ndoto mbaya au kilicho bora hukitaki tena?" ukweli ni kuwa mwanzo Mkita hakumchukia Lindiwe kwa uamuzi aliufanya akijua alishinikizwa na wazazi wake,na mschana yeyote angekuwa katika nafasi yake angefanya hivyo lakini katika pita zake alimsikia Lindiwe akiongea na marafiki zake akimkejeli Nzagamba tena kwa uso mkavu kitendo kilichomfanya Mkita amchukie kwani aligundua kuwa hakumpenda Nzagamba alimfuata kwa sababu kwa wakati huo alimuona ni Bora na Sasa kuanza kujipitisha kumharibia Nzagamba heshima ambayo Tulya ameteketeza maisha yake kuileta kilimkera sana Mkita.
Lindiwe anaangalia chini kwa aibu machozi yakimtoka " hiyo.. hiyo.." anaanza kujitetea sauti ikitetemeka nyingine ikikwama kooni isitake kutoka." Haina haja ya kujieleza kwangu Lindiwe,ulichagua kilicho bora,ishi na kilicho bora,watu wasiokubali kuishi na majuto ya maamuzi Yao walioyafanya ni wabaya kuliko mchawi na kidogo kidogo hugeuka na kuwa wachawi kwa wivu" anatulaia kidogo akimwangalia Lindiwe.
" ishi hivyohivyo Lindiwe,nadhani mizimu inakuadhibu kwa ulichomfanya Nzagamba,na nisikuone unamsubiria Nzagamba na kujipitisha tena,heshima kaipata kwa shida na sitaiacha ipotee kwa sababu yako kamwe" Anamwambia angeuka na kuondoka.
Lindiwe anakaa chini miguu ikimuisha nguvu machozi yakizidi kutoka,mkono wake wa kulia ukienda kifuani akipiga kifua Chake anachohisi kina bana uchungu una mjaa moyoni,majuto na kujionea huruma mwenyewe.
Mkita anaendelea kutembea,uso wake ukiwa Hauna dalili ya ucheshi anaotembeaga nao Kila siku.Ukweli ni kuwa Mkita ni mcheshi kwa wakati wake ila akiamua kufanya kitu akiweka akili yake ile sura yake ya ucheshi unaikosa kabisa unaweza kujiuliza kuwa labda ni watu wawili tofauti.
Wakati anatembea anakumbuka siku aliyomkuta Tulya amegombana na Nzagamba na baada ya kujua kuwa Lindiwe ndio sababu,jioni ile alikuwa na hasira alienda kumtafuta Manumbu katika vijiwe vyote vya kunywea pombe na hatimaye juhudi zake zilizaa matunda baada ya kumkuta katika danguro Moja akiwa na mwanamke mwingine wakilewa.
" niletee na Mimi pombe" anaagiza Mkita akikaa kwenye gogo karibu na Nzagamba.
" unafanya nini hapa?" anauliza Manumbu akikereka maana kundi lote la Nzagamba humtoa damu puani kwa hasira.
" kwani wewe unafanya nini hapa,unachokifanya wewe ndio ninachokifanya Mimi hapa, asante mrembo" maneno ya mwisho anaongea akimwangalia mschana aliyeleta pombe, mschana anaanza kujipitisha lakini Mkita hakuwa kwenye Hali ya kutongozwa Leo,na hata Kama alikuja kwa starehe msichana hakuwa kipande chake kabisa kwani nyumbani ana mke mrembo mtoto mlaini mwenye miaka kumi na sita tu mwenye nyonyo saa sita hata akinyonyesha watoto Saba litakuwa bado liko palepale aangaike na ngozi ya kenge kisa nini,kwa hiyo wamuache kabisa.Anamkata jicho Kali mschana kumuonyesha atokomee huko na mschana anajua kutii akaamua kuondoka.Jicho lake linarudi kwa Manumbu aliyekuwa anaendelea kucheza na mwanamke ambaye hamfikiii mkewe hata nusu kwa uzuri Mkita anatikisa kichwa lakini hayo yeye hayamuhusu amalize kazi yake aondoke.
" tuondoke" anamsikia Manumbu akiongea baada ya kumpuuzia Mkita kama hakuwepo wote wanasimama Manumbu akinesa kwa pombe." unaweza kwenda kummudu huyo au unaondoka nae tu" Manumbu anamsikia Mkita akiongea baada ya kupiga hatua kuondoka anageuka na kumwangalia " unasemaje?" Manumbu anamuuliza asijue huyu kinyago wa Kijiji anamaanisha nini na anamchezo gani.
" dada anaweza kukuacha nusu huyo,unaweza kuondoka na mimi" anaongea Mkita akisimama na tabasamu mwanana.
" unafanya nini wewe,? kama unataka mwanamke si uchukue wako" Manumbu anaongea kwa hasira kwani anajua Mkita anamdhalilisha kwa kumfanya aonekane hajui mambo kitandani.
" nataka nikusaidie tu,Ili usiaibike" anaongea Mkita sura yake akiiweka Kama vile Manumbu anazama mto na yeye ndio pekee anaweza kumtoa.
"unamaanisha Mimi sijiwezi au,nitakuua" anamsogelea na kumkwida Mkita rubega yake.lakini Mkita anamwangalia tu kwa dharau akijua akiuwasha moto atakayeungua ni yeye hata kama Manumbu angekuwa hajalewa asingeweza kumpiga Mkita kwani uwezo wao unalingana hivyo Kila mtu angeondoka na ngeu ya kukandwa maji nyumbani." sijasema Mimi kasema mkeo" Mkita anamnong'oneza na Manumbu kumwangalia kwa mshtuko.
" hawezi kusema hivyo" Manumbu anamtetea mkewe.
"unajua mwanamke akiwa anahaha kuridhishwa nje inajulikana mumewe hamtoshelezi,anachokifanya mkeo ndio kinathibitisha hilo" Mkita anaongea kwa sauti ya chini asitake kutangaza mambo zaidi kwani anajua atamharibia na rafiki yake na anajua Manumbu hawezi kupiga mdomo wake kwa vile anapenda sifa na nafsi yake isingekubali kudhalilika hivyo anauhakika atakaa kimya.
" mke wangu Hana tabia hizo" anaongea Manumbu kama Mkita alivyotabiria kwa sauti ya chini.
" utakuwa hujui kinachoendelea kijijini" anatulia kidogo akimwangalia Manumbu anachukuliaje.
"fuatilia vizuri utajua,au muulize rafiki yako Nsio atakwambia,naona hata marafiki zako wamekuficha" anaongea Mkita akimwangalia Manumbu uso ukimshuka na tabasamu linatanda mdomoni kwake.Manumbu anamwachia na kuondoka akimsahau hata mwanamke aliyetaka kwenda kulala nae.
kwa sasa Mkita akikumbuka anatabasamu akijua ilikuwa Haina haja ya kutumia jasho jingi wakati Manumbu angefanya kazi nzuri kumuadabisha Lindiwe anajua alichokifanya sio kizuri akiangalia jinsi sura ya Lindiwe ilivyoharibika lakini hiyo ilikuwa inakuja pale tu alipoamua kucheza na shemeji yake Tulya.
" Mbona umechelewa?" Ntula anamuuliza baada ya kumuona Mkita akifika na kukaa karibu yake na kumnyang'anya kipande Cha nyama aliyokuwa anakula na kukitupia mdomoni.
" Kuna kitu nilikuwa nakiweka sawa" anamjibu akimwangalia Nzagamba anayegeuza nyama kwenye moto.
" kitu gani?" anauliza Kilinge
" huhitaji kujua" anamjibu mdomo wake ukiwa umejaa nyama anayoitafuna.
wakati huu marafiki wote wakiwa mtoni wakiwinda ndege na Leo wameamua kuwasha moto na kuchoma wakila na kuongea.
" Kuna nini?" anauliza Lingo anayemuona Zinge akiangalia upande Mmoja kwa mda mrefu na wote wanageuka na kumwangalia Zinge wakiangalia anakoangalia.Nzagamba aliyekuwa na mawazo mengi mwanzoni hakuhisi kitu,lakini kwa sasa anahisi uwepo wa mtu upande ule.macho yake yanarudi na kumwangalia Zinge ambaye alikuwa bado anaangalia kule.
" hamuhisi kama Kuna mtu mwingine zaidi yetu hapa?" anauliza Zinge akiwaangalia marafiki zake Nzagamba anamwangalia kwa kutokuamini inamaana sio yeye tu.
" unamaanisha nini?" anauliza Mkita akiangalia huku na kule.
"itakuwa mawazo yako tu" Kilinge anamjibu lakini bado Zinge haamini au labda ameanza kuchanganyikiwa.
" tangu lini mekuwa ukihisi hivyo?" Nzagamba anamuuliza.
" kwa siku kadhaa hivi," anafikiria vikidogo na kusema " tangu siku tunajenga uwaa nyumbani kwako" anamjibu.
imekuwa ni mda mrefu anawaza Nzagamba akimwangalia Zinge akihisi tatizo haliki kwake tu na kwa Tulya nini kinaendelea.