Nzagamba anahisi kabisa Kuna kitu kinaendelea maana Kuna Hali ya upepo inabadilika, hizi hisia za mtu akimfuatilia mara sungura na Sasa kwa Tulya lazima Kuna kitu kinabadilika.
" kuanzia lini?" anamuuliza.
" sijui,ila nimekuwa nikihisi hivyo tu halafu juzi ile nilikutana na kitu Cha ajabu"
" kitu gani hicho?" anamuuliza.
Kumbukumbu za Tulya zinarudi nyuma siku tatu kabla Bibi sumbo hajamtuma kuleta chakula na kukutana na kisanga.
Akiwa anafinyanga chungu anashtuka kwa kuona mtu akiwa amesimama uani akimwangalia anageuka na kumuona Binti wa miaka kama kumi na nane." karibu" Tulya anamkaribisha akisimama na kumfuata akijua mteja wa vyungu,mdada anaendelea kumwangalia tu." unahitaji kitu?" anamuuliza lakini bado hajibu kitu.Anaangalia mavazi yake na kuona amejifunga kaniki Moja tu iliyoanzia juu ya kifua mpaka chini.
" we bubu au,unataka nini?" bado msichana hajibu " ohh mizimu sijui hata umetokea wapi Mimi sikujui" anaongea akiangalia huku na kule." mama naye katoka labda anakujua"
" maji" mschana anaongea " ohh unaongea umenitisha,haya subiri nakuletea" anaenda ndani na kurudi na kipeo Cha maji anamkuta mschana akiangalia vyungu alivyovianika kwenye kuchanja.
" una mkono mzuri kuliko nilivyofikiria na isitoshe umejifunzia ukubwani" anaongea mschana akiendelea kuangalia vyungu.
" ndio,watu wengi wanasema Nina kichwa rahisi,kwani nilifundishwa mara Moja tu nikaelewa" Tulya anaongea akiendelea kushikilia kipeo Cha maji na mschana asifanye juhudi zozote kuchukua maji kwa mtu aliyekuwa na kiu.
" kama unataka chungu inabidi usubiri siku nne Mbele ndio ninachoma" anaongea Tulya akimwangalia mschana aliyekuwa akiendelea kukagua chungu kimoja baada ya kingine kama mwalimu akimwangalia mwanafunzi wake.
" umefanya vizuri ukiwa mwenyewe Tulya" anageuka na kumwangalia Tulya machoni.
" na umekuwa na kuwa Binti mrembo na shupavu" Tulya anamwangalia asijue afanyeje kwa pongezi anazozipokea kwa mtu asiyemjua subiri lakini mbona anaongea kama mtu mzima na kama vile ananijua anajiuliza Tulya lakini watu wengi wanamjua kutokan na kuolewa na Nzagamba akawa maarufu kwa sababu hii anapuzia na kuendelea kumsikiliza.
" asante" anaongea mschana akipokea kipeo Cha maji anakunywa na kumaliza yote.
"Nina uhakika utafanya vizuri zaidi huko Mbele, unaweza kuniongezea maji"
" ndio,nakuja Sasa hivi" anajibu Tulya akikimbia kuelekea ndani.
" kaenda wapi?" anajiuliza baada ya kurudi asimuone anaweka kipeo Cha maji juu ya kichanja anaanza kuangalia huku na kule asimuone.Anaamua kupuuzia na kuendelea na kazi yake.
Ukirudi walipo Sasa Nzagamba anamwangalia asielewe anaongelea nini.
" mwanzoni niliona ni kitu Cha kawaida labda tu aliondoka lakini Sasa nikifikiria naona sio kitu Cha kawaida,Amna mtu anayevaa kaniki wakati huu hasa mabindi si ndio?" anamuuliza na Nzagamba anaitikia kwa kichwa kukubaliana nae.
" na kingine najiuliza alipita wapi kwani uaani amna njia na angepita huku mlango mkubwa ningemuona ni kama kayeyuka vile" anaongea na kutupia kipande Cha nyama mdomoni.
" kwa nini hukusema?" Nzagamba anamuuliza kwa sauti yenye hasira kidogo akimshtua Tulya.
" kwanza kabisa niliona sio jambo kubwa na pili baaada ya kilichotokea siku ile nilinirukwa akilini kabisa" anajitetea Tulya asijue kilichomtibua tena maana Hali inataka kurudi mwanzo tena.
Nzagamba anasimama akikuna kichwa chake.
" samahani kwa kukupandishja sauti,ni kwamba Mimi mwenyewe nimekuwa nikihisi mtu ananifuatilia kwa mda Sasa lakini Kila nikigeuka simuoni"
" ehh! tangu lini?" Tulya anauliza akisimama nyama zikianza kumuisha hamu.
" nadhani siku mbili baada ya harusi yetu"
" ehee!, na ndio unaniambia Sasa hivi?" anauliza asiamini alikuwa anampigia kelele wakati yeye mwenyewe amefanya yaleyale.
" sikuona umuhimu, na kitu kingine Cha ajabu juzi wakati narudi nyumbani nilikutana na sungura"
" sungura mnyama?"
" ndio"
" kwani hujawahi kumuona?"
" hivi hujui Hali yangu au kwa sababu unaisikia tu,nikimaanishi wanyama wanakimbizwa na harufu yangu namaanisha wanapita miguu elfu kumi mbali na Mimi ndivyo harufu yangu inavyosambaa Sasa sungura alipita hatua Moja na mimi wewe unalionaje hilo,eee?" anaongea Nzagamba akimwangalia Tulya kwenye macho kama hamuelewi lugha.
" labda laana inaisha" Tulya anaongea asijue amwambieje.
" haiwezi kwisha hii Tulya natakiwa kufa nayo weka hiyo akilini na usipate matumaini" anaongea karibu na uso wake kidogo amtemee mate anageuka na kuangalia upande mwingine.
" sikumaanisha hivyo Nzagamba,Mimi nimeongea kutokana na ulivyoniambia wewe,basi usikasirike inabidi tujue nini kinaendelea maana haya ni kama mauzauza au mtu anatufanyia mchezo" anaongea Tulya akijawa wasiwasi.
" nani afanye mchezo huu,tayari sina maisha anataka kitu gani kwangu" anaongea Nzagamba sauti ikijaa majonzi lakini moyoni anajua kuwa kitu kama hiki hakiwezi kufanywa na binadamu kwani,yeye na mama yake baada ya kujua laana yake walienda kwa wataalamu mbalimbali wakijaribu kutafuta njia ya kuivunja lakini waliambiwa ipo kwenye damu Ili laana itoke inapidi aitoe damu yake yote ndio laana iondoke na ni kitu ambacho hakiwezekani, na hiyo ndio ilikuwa mwisho wa matumaini yake na hataki kuyafufua kwa namna yeyote ile.
" usijali Kila kitu kitakuwa sawa,usijali kwa pamoja tutagundua ni nini kinaendelea.Tulya anaenda na kumkumbatia na kumfanya Nzagamba ajione hayuko peke yake.Nzagamba anamwangalia tu asiweze kurudisha kumbato lake lakini alichokifanya Tulya kinamfanya atulie na kufarijika.
" usijali nitakuwa hapa na chochote kile kitakachokuja tutapambana nacho pamoja" Tulya anaongea akiwa bado kifuani kwa Nzagamba na kumfanya Nzagamba avute pumzi ndefu.
" nenda nyumbani na ukiona chochote kile uniambie sawa" Tulya anamwachia na kupiga hatua nyuma na macho yake yakienda juu kumwangalia akinyanyua shingo yake Ili amwangalie vizuri kutokana na Nzagamba kumzidi kimo.
" sawa na wewe ukiona chochote uniambie,tusifichane kitu Mimi ni mkeo natakiwa kujua Kila kitu Ili nijue nitakusaidia kwa mawazo au nikufariji " Anatulia kidogo na kuendelea "Najua kipindi Cha nyuma mama alikuwa na wewe lakini Nina uhakika hukuweza kujionyesha Mbele yake ni jinsi gani ulikuwa unaumia kwa sababu i
ulikuwa unataka kumpunguzia yeye maumivu,kwa sasa niko hapa kuanzia Sasa na kuendelea niambie Kila kitu na Mimi nitasaidiana na wewe kubeba maumivu yako na nakuahidi sitachoka kwa hiyo naomba nijaribu uone,maumivu yako ni yangu kwa hiyo naomba usiyabebe mwenyewe unaweza kufanya hivyo" anmwangalia kwa matumaini na baada ya kuona Nzagamba akitikia tabasamu pana linatoka mdomoni kwake.
" sawa Mimi naondoka,usiache kula na uwe na siku njema mume wangu" anaongea akitabasamu na kufanya mapigo ya moyo wa Nzagamba kuruka na kukosea mahesabu yake anajisikia vizuri kuitwa mume wa mtu.Tulya anapiga hatua akianza kuondoka lakini anasimama.
" marafiki zako wako wapi?" anamuuliza nakumfanya Nzagamba ageuke na kumwangalia alipo.
" wanakuja nadhani watakuwa hapa mda sio mrefu"
" naweza nikakaa mpaka watakapofika" anamuuliza asitake kumwacha peke yake asije akapata mawazo asijue kama Sasa hivi asingewaza kuhusu sungura wala laana atakachokiwaza ni mwanamke Tulya tu mke wake kwani kampatia sababu ya Kila aina ya kubaki kichwani kwake.
" hapana usijali we nenda nitakuwa sawa"
Tulya anampa tabasamu na kuondoka Nzagamba akimwangalia akiondoka.
" kumbe laana haikuchukua vyote Kuna kitu ilisahau" anaongea Nzagamba kwa sauti ya chini akimwangalia akiondoka.
" Tulya,ilisahau mwanamke anayeitwa Tulya"
Upande wa pili wa mto alipo Nzagamba sehemu wanapochota maji wanawake,.Mkita aliyekuwa ameweka lindo toka Jana yake hatimaye nyota ya jaa imemuangazia baada ya mtego wake kunasa,anaruka juu ya mti na kutua chini kama ngedere katika ubora wake anatema kijiti alichokuwa anakitafuna mdomoni kwake na kupiga hatua na kuelekea alipo mwanamke anayejiandaa kuchota maji.
" hatimaye,nilijua nitageuka kichuguu" anaongea Mkita na kusimama karibua na mwanamke anayegeuka na kumwangalia kwa mshangao.
" unataka nini Mkita" anauliza mwanamke akimwangalia Mkita kama hayuko kwenye Hali ya kuongea na Mkita ikiwa ni kweli hakuwa kwenye Hali ya kuongea na mtu yeyote na hasa kucheza kombolela na Mkita.Mwanamke anajaribu kumkazia macho Ili amwangalie kwa ukali Mkita lakini zoezi linaanguka vibaya baada ya jicho lake Moja kutokufunga na lingine likisema usinilazimishe bwana hapa ndio nimefikia mwisho siongezeki tena.
Mwanamke mwenyewe hakuwa mwingine Bali ni Lindiwe aliyekuwa amependeza baada ya Manumbu kumcharaza na kumfanya kuhumuka baadhi ya maeneoa ya mwili wake kibaya zaidi macho yake, Moja likiwa halionekanj kabisa na lingine likionekana kama mwezi mchanga.
" aaah! kama kawaida rafiki yangu Manumbu huwa haachi kunishangaza,kafanya kazi nzuri sana" anaongea Mkita mtu akisikia atajuwa yeye na Manumbu ni maswahiba wa kufa na kuzikana na anachokisifia hapa sio mtu aliyepigwa na kuumia bali ni kinyago chake Cha sanaa alicho kichongesha.