"Njengele! njengele! njengele!" sauti ya njuga alizovaa Tulya mguuni zikiendelea kupiga kelele Kila hatua anayopiga,anajitahidi kukanyaga kwa umakini Ili zisitoe sauti zaidi lakini bado zinamsaliti na kutoa sauti kubwa kuliko ya mwanzo.Tulya aliyechanganyikiwa baada ya kumuona Nzagamba nyumbani kwa mjombaake aliingia ndani na kuaga na kwa sasa wako njiani kuelekea nyumbani.
Nzagamba akiwa Mbele yeye nyuma akifukuzia hatua ndefu anazopiga Ili asimuwache.Kutokana na haraka na kiwewe Tulya alisahau kama mguuni alivaa njuga akatoka hivyohivyo safari ikiwa tayari imeshaanza ndio anazisikia anatamani asimame azitoe lakini kwa muonekano wa Nzagamba sijui kama atamsubiri na yeye sauti hana ya kumwambia asubiri avue njuga alizovaa kwa starehe yake.kimoyoni anajitukana kwa kuwa mjinga na ndio adhabu yake kutembea na njuga zikipiga makelele kama mbuzi mtukukutu aliyefungwa kengele na Sasa anajua kero anayoipata mbuzi kengere ikiwa shingoni pake afadhali yeye Iko mguuni na bado inamkera.
Nzagamba anaendelea kupiga hatua kifua chake kikiwa bado kizito kwa hasira,anazisikia sauti za njuga zinamkera lakini anaamua kuzivumilia akimpatia Tulya adhabu na kumuacha atembee kama mganga wa kienyeji akifanya matambiko kuzunguka Kijiji.Anaongeza mwendo na kuzisikia njuga zikiongeza kasi ya mziki wake na kujua Tulya anajaribu kukimbia Ili asimuache.
Hatimaye safari ya njuga inafikia tamati baada ya kufika nyumbani Nzagamba anafungua mlango anaingia ndani na kushikilia mlango na kumpatia nafasi Tulya aingie.Anaingia huku mapigo yake ya moyo yakipanda mikono yake akiwa ameishikana Mbele akichezea vidole vyake mwanga hafifu wa kibatari sebuleni unafifia kutokana na upepo unaoingia na kutishia kuzimika.
" nataka nifunge mlango"
" ehhh?!" anashtuka Tulya na macho yake haraka yanaenda kukutana na ya Nzagamba ambaye tayari alikuwa anamwangalia.
" unampango wa kulala hapo au?" anamuuliza kwani Tulya alikuwa ameingia ndani lakini sio mbali na mlangoni.taa inatikisika tena kutokana na upepo Tulya anasogea pole pole asijue kinamugopesha nini.
" taa itazi....pumbavu" kabla Nzagamba hajamalizia taa inazima na kufanya mboni za macho Yao kuongezeka saizi wakijaribu kulizoea giza.
Nzagamba anakomelea kizingiti mlangoni,anageuka na kuelekea kwenye mafiga kuchukua kizinga Ili awashe taa.
" aaahh!" anapiga makelele Tulya na hiyo ni baada ya kupamiana na Nzagamba.
"unafanya nini huku?" anauliza Nzagamba akijaribu kuzuia purukushani zao za kuelekea chini lakini pasipo mafanikio na wote wanajikuta chini Nzagamba akiwa juu ya mwenzake.Tulya aliyekuwa anaelekea kwenye mafiga kufanya jambo hilohilo la kuwasha taa alipigana kikumbo na Nzagamba anatetereka miguuni anarudi nyuma kidogo Ili ajiweke sawa lakini anakanyaga Kuni na kuanza kuelekea chini Ili kujizuia asianguke anashika mkono wa Nzagamba ambaye naye hakusimama vizuri na wote kwenda chini matako ya Tulya yakifikia kwenye ukuni na kumfanya apige makelele.Nzagamba aliyesikia njuga za Tulya zikisogea alijua labda anaelekea chumbani na yeye kuamua kwenda kuwasha taa hakujua kama wote walikuwa na wazo Moja na kilichowakuta ndio hicho kwa tatizo lao la kutokuongea.
" kwa nini usiwe makini?" anamuuliza akijaribu kujizoa chini.
" nimekanyaga ku..." maneno yake yanamezwa mdomoni mwake baada ya Nzagamba aliyekuwa anajaribu kunyanyuka kurudi tena chini na juhudi za kuzuia uzito wake usimlalie Tulya zinafanya mkono wake wa kulia kuishia kwenye nyonyo Moja saa sita la Tulya na mwingine chini pembeni ya bega la Tulya uso wake ukiishia kwenye shingo ya Tulya.
Koo la Tulya linakauka ghafla na mwili wake ukimsisimka kwani nywele za Nzagamba zilizojisokota zilikuwa zinamtekenya kwenye shingo na akisikia pumzi zake karibu na mfupa wa shingo yake.
" ooh mizimu nisaidieni" anawaza Tulya akijaribu kuifanya akili yake ifanye kazi lakini inaonekana kuwa kitu kigumu kutokana na ukaribu wao na mwili wake kuganda usifanye juhudi ya kusogeza.
Nzagamba ambaye hakuwa kwenye mpango wa kurudi leo anaendelea kubaki kama alivyo akivuta harufu nzuri ya Tulya " ananukia kama ardhi ambayo haijapata maji mda mrefu"anajisemea akiendelea kumnusa Tulya shingoni. Ardhi ambayo haijapata mvua mda mrefu siku mawingu yakijikusanya isinyeshe mvua kubwa ila ni manyunyu tu ardhi hutoa harufu nzuri sana na ya kipekee ambayo ni adimu sana kuipata na hali hii hutokea mara Moja tu kwa mwaka na ni pindi kiangazi kinapoisha na kuyakaribisha masika kutoa ishara kuwa mvua zinakaribia kuanza.Lakini inakuwaje mwanamke huyu anakuwa na hii harufu mwilini mwake tena ikiwa kama vile huzalishwa hapa anaendelea kusogeza pua zake karibu na shingo ya Tulya na kusahua mahali mkono wake wa kulia ulipo na akiuchezesha kabisa kama kupima ukubwa wa nyonyo.
Tulya anabaki akiwa ameganda pale chini akifumba macho yake mwili wake ukipata msisimko na hisia ambazo hazijui kutokana na Nzagamba anayeendelea kuchezea nyonyo lake huku akimnusa shingo na kupitisha meno yake kwenye ngozi kama anataka kumng'ata na kitendo hicho hakimtishi kwani kwa alivyo hivi Sasa hata kama Nzagamba angeondoka na nyama robo ya mwili wake bado asingeshtuka,mapigo yake ya moyo yakiwa kasi na pumzi zake zikiendelea kupanda Kila baada ya sekende.Baada ya muda anahisi kitu kikicheza kwenye paja lake kikiongezea hisia nzito katika mwili wake.matamanio yanamtuma ajisogeze Ili akihisi vizuri zaidi na hapo ndipo alipoharibu " njingirii!"
Wote wanarudishwa na kelele za njuga alizovaa Tulya zikionyesha uwepo wao baada ya Tulya kuchezesha miguu yake.Nzagamba anatoa kichwa chake kwenye shingo ya Tulya na kusogeza pembeni lakini hakupeleka mbali kwani uso wake unakuja na kuwa karibu na uso wa Tulya aliyekuwa bado amefumba macho pumzi zake zikipanda na kushuka zikiwa sawa na za Nzagamba,hawaonani sura lakini Kila mtu anatambuwa uwepo wa mwenzake kutoka na pumzi zao karibu na nyuso zao." njengele!" njuga zinaita tena baada ya Tulya kusogeza mguu Mmoja.
Nzagamba anatoa mkono wake kwenye ziwa la Tulya haraka kama ameungua baada ya kusikia sauti ya njuga tena.Anaamka taratibu asije akaanguka na kurudi katika Hali Yao ya awali.Tulya anafumbua macho yake taratibu baada ya kuhisi uzito uliokuwa juu yake kupotea.akiwa bado anajizoa pale chini anaona cheche za kizinga zikipiga wakati Nzagamba akipuliza awashe taa na haikuchukua mda mrefu sebule kuangaza mwanga wa kibatari.Nzagamba anageuka akiwa ameshikilia kibatari mkononi na kumuona Tulya bado amekaa chini macho yake ardhini akijaribu kutafuta ujasiri wa kumwangalia Nzagamba usoni.
"chukua taa ukalale" anamsikia akiongea anasimama macho yake yakiangalia kokote isipokuwa nzagamba.anaona mwanga wa taa ukikaribia usoni kwake ananyanyua macho yake na kukutana na ya Nzagamba.Mapigo ya moyo wa Nzagamba yanatulia kwa muda baada ya kuona macho ya Tulya yaliyokuwa bado yamelegea kimahaba kutokana na kitendo kilichotokea kati yao mda mfupi uliopita kwani mwili wake ulikuwa bado unakihisi kilichotokea Kama bado kinaendelea kutokea.Akili na mwili wake vyote vinaunguruma kuonyesha ni jinsi gani vilivyo na njaa na Tulya ndio chakula wanachokihitaji kwa Sasa anameza funda kubwa la mate akihisi maumbile yake ya kiume yakinyanyuka zaidi kuliko pale awali alipokuwa amemlalia Tulya.
" usiku mwema" Tulya anamwambia akishika kibatari na kutimua mbio kuelekea chumbani akimwacha mtoto wa watu gizani tena gizani kweli.Nzagamba anafungua mlango na kutoka nje kwani joto la ndani kwake kwa sasa haliwezi kabisa Tulya amewasha moto na yeye hawezi kuuzima anajua akiusogelea ataungua tena ataungua sana asiweze kutazamika.Anaenda na kujitupa kwenye kitanda chake cha kupumzikia nje analala Chali macho yake yanaenda juu na kuangalia mwezi mchanga ambao tayari ulikuwa unaelekea kuzama.
Anajaribu kuweka akili na mwili wake sawa lakini inakuwa ngumu kwani mambo yalishafika mbali kuyarudisha kiurahisi namna hiii,anaunyanyua mkono wake wa kulia ulikuwa bado unahisi kushikilia ziwa la Tulya lililokuwa limechanganyika kwa ulaini na ugumu anauangalia na akilia yake kumtuma angelishika zaidi kwani kile kilikuwa ni kitu adimu.Anahisi mabadiliko ya mapigo ya moyo wake Kuja juu tena " pumbavu" anatukana akiamka na kukaa kitandani asijue afanye nini kuziondoa hizi hisia.
Mbwa wake wanakuja alipo na kuanza kubweka kidogo wakimwongelesha kama kumuuliza kwa nini asiingie tu ndani afanye anachokitaka kwani yule si mke wake.lakini anaamua kuwapuuzia akifumba macho na kuwaambia Hana muda wa kucheza nao Leo.
Akiwa nje analisikia jogoo la kwanza likiwika asiamini kama kakesha nje na Hali yake ikiwa bado ileile na hapo anagundua kitu kimoja,hajui kama anampenda Tulya ila anamuhitaji kama maji jangwani.ama akae nae mbali maana atamuua.