Chereads / penzi la bahati / Chapter 38 - chapter 37

Chapter 38 - chapter 37

"Amenikuta na Lindiwe" anawajibu Nzagamba akiamka na kukaa vizuri kwenye jiwe na mikono yake akiikusanya magotini pake macho yake yanaenda kwa marafiki zake wanaomwangalia kama kasema marehemu hakufa wakati tayari ameshazikwa.

" unanitania au?" anauliza Mkita aliyeahirisha safari yake ya kuweka mtego kwa sababu anajua familia yake haiwezi kufa kwa kukosa mlo Mmoja ila yeye akikosa kinachoendelea maishani mwa Nzagamba yeye ndio atakuwa marehemu.

" kivipi? wakati wewe na Lindiwe hamuongei tangu avunje uchumba?" anauliza Ntula.

" kwanza kawakuta mnafanya nini mpaka aangue msiba namna ile?" anauliza Mkita akikaa kabisa.

" ndio,inavyoonekana kama Hali ilikuwa mbaya" Lingo anaongezea na Mkita anatikisa kichwa kukubaliana naye sura yake ikimwambia Nzagamba amwage mpunga haraka kwani hana uvumilivu lakini mpunga huo unamwagwa lakini bado unakutana na mabonde na milima mpaka umfikie kwa sababu Nzagamba anatafutiza maneno ya kuwaambia marafiki zake kwa sababu hata yeye mwenyewe haelewi ugomvi wao ulivyo umepindapinda kuanzia suala la Luila gulioni.

" sema bwana" anaamua kumrukia.

" hata sijui" Nzagamba anamjibu ukweli.

" hujui mlikuwa mnafanya nini?" Ntula anamuuliza.

" mambo mengine uko haraka inakuwaje huku uko polepole kama konokono" anaongea Mkita uvumilivu ukikatika na Nzagamba anamkata jicho angekuwa anajua Cha kufanya hata asingekuwa anaongea na ngedere Hawa wanaomkodolea macho hapa anawaza Nzagamba akiwaangalia marafiki zake Mmoja baada ya mwingine na wao wakimwangalia kwa kusubiri aseme.analamba midomo yake na kuvuta pumzi.

" nimekuja nimeweka mitego yangu hapa asubuhi,badae nilikuwa na shida na Mzee Kipile nikaiacha nikaenda nyumbani kwake,nilpokuwa narudi nikakutana na Lindiwe njiani tukawa tunaongea kidogo mara na yeye huyo alikuwa analeta chakula ndio akatukuta hapo,ndio kama hivyo" anamaliza hivyo kifupi tu.

" imekuwaje muongee na Lindiwe mpaka msimame na hamjawahi kuongea kwa miaka mitatu Sasa?" anauliza Mkita akimwangalia mwenzake kwa jicho la kutomwamini.

" unamaanisha nini?" anamuuliza kwa kukereka kabla Mkita hajajibu Lingo anamuuliza.

" hii sio mara ya kwanza kuongea na Lindiwe si ndio?" Ntula na Mkita macho Yao yanenda kwa Lingo Kisha yanarudi kwa Nzagamba.

" ndio,siku nyingi zilizopita nilikuta naye pia tukasalimiana na kujuliana Hali tu,aaaa na kabla ya gulio nilionana naye akanisalimia"

" umefumaniwa" Mkita anasema akimwangalia Nzagamba kwa jicho la kumwambia kalikoroga.

" acha upumbavu nifumaniwe kivipi?" anaongea Nzagamba akikereka zaidi.

" Sasa unamalizia hasira kwangu Mimi ndio nilikutuma ukapige soga na Lindiwe" Mkita analalamika.

" ndio umefumaniwa Nzagamba" Lingo naye anakazia.

" mnanitania au?" Nzagamba anauliza asiamini hawa wajinga wanazungumzia nini.

" Kila kitu kilikuwa sawa kati yenu kabla ya Leo?" Ntula anamuuliza.

Nzagamba anatulia kidogo asijue asemeje.

" hata sielewi kumekuwa na kutokuelewana kidogo ila siwezi kuwaambia kiundani zaidi" anawajibu asitake kusema kuwa Tulya anamwanaume aneyempenda kwani kwa kilichotokea Leo Hana uhakika alizungumzieje tukio la gulioni.

" Mimi nilisikia kwa make wangu kuwa umekuwa ukionekana na Lindiwe mara kwa mara sikutaka kukuuliza kwani chanzo Cha habari hakikiwa Cha kuaminika ila kutoka na Tulya alivyo Leo nadhani mkeo amezipata habari hizo na alipokuona nae zikakata kamba aa kabisa" Lingo anamwambia.

" nani kaongea upumbavu huo,Mimi nimesalimiana nae tu" Nzagamba Kawa mkali.

" mama Nsio " Lingo anaongea na kama angekuwa na ugoro wa akiba sikioni kwake angeuweka mdomoni kusukumizia bahati mbaya alioutapika ulikuwa ni akiba yake ya mwisho.Ntula anapiga mluzi akimwonea huruma Nzagamba kwa msala aliojiingiza.

" mwanamke anamdomo yule,yeye na mkwewe wote jungu Moja" anaongea Mkita akikasirika anageuka na kumwangalia Nzagamba

" na wewe kilichokutuma ukaongee na huyo mwanamke aliyekukimbia wakati wa shida nini? ulitakiwa hata akikusalimia ummpite tu,siku zinavyozidi kwenda nazidi kumchukia yule mwanamke" anaongea Mkita habari zikimkera kuliko Nzagamba mwenyewe,ingekuwa Nzagamba na Tulya wanegombana kwa mambo yao binafsi Mkita asingekereka namna hii,kwani uhalisi anampenda Tulya kama shemeji yake haijalishi kaolewa vipi na Nzagamba lakini kitendo hicho kimempatia rafiki yake heshima kidogo na tangu Nzagamba aoe amekuwa akimwona sio mpweke kama zamani hilo linampa faraja na msichana mzuri kama Tulya kujitoa kafara namna ile akijua maisha ya Nzagamba hayatabadilika kilimfanya ampe heshima kubwa sana Tulya na isitoshe ana roho nzuri na kitendo Cha kumuona akilia pale kilimuumiza sana na alikuwa na mpango wa kumkanya rafiki yake baadae kuwa asimlize Tulya amthamini,Kuja kugundua kuwa kalia kwa sababu ya Lindiwe limemvuruga,limempandisha hasira na kufanya damu kuchemka.

" na mama Nsio na mdomo wake ataongea kama debe la kufukuzia ngedere shamba la mahindi" anaongezea Ntula.

" na ataongezea mengine" Lingo anakazia.Nzagamba anakumbuka tangu siku ya gulio Tulya amekuwa mkimya akajua labda kwa sababu ya mwanaume aliyeonana nae gulionj Sasa anagundua kuwa hili ndio lilikuwa linamsumbua anang'ata meno kwa hasira akijua wote walielewana vibaya.

" utafanyeje?" Ntula anamuuliza.

" afanye nini? akamweleze Tulya ukweli na aache kuonana na yule kinyonga." Mkita anakazia kama vile Nzagamba ni mtoto anayetakiwa kurekebishwa tabia haraka sana.

wanasikia sauti za watu wakiongea wanageuka na kuwaona Kilinge na Zinge wakija.

" Mkita kaweka mtego" Lingo anamwambia akiomba hali ya hewa irudi kawaida." Ntula lete chakula hicho tule maana aniyeletewa kula hamu imekata sidhani kama atakula"

Ntula anachukua kikapu na kutoa chakula na wakati huo wanafika Kilinge na Zinge.

" viazi na maziwa" anasema Kilinge anakaa na kuendelea " mmebeba na vyakula Leo?" anauliza Kilinge akikaa." vya shemeji yenu,yeye kashiba"anasema Ntula akichukua kiazi." Kuna kitu kimetokea au?" anauliza Zinge baada ya kumuona Nzagamba kainamisha kichwa." kitokee nini?" anajibu Ntula akimwangalia Zinge anaona macho yake yakimwangalia Nzagamba" aaaa huyo kachoka tu kaja tangu asubuhi,we nawe kisikupite kitu" maneno ya mwisho anaongea kwa sauti ya chini " Mkita wahi tuje kula" anamwita Mkita kwa sauti ya juu kama alikuwa kwa jirani na uhalisia ni kuwa Mkita alikuwa anarudi baada ya kuweka mitego yake na alishakatibia kufika.

Mbali na walipo Tulya anafanikiwa kufika nyumbani akihema baada ya kukimbia njia nzima,anaingia ndani kwake na kujitupa kitandani " ohh mizimi ya mababu zangu nimefanyeje Mimi, aaaah!" anavuta nywele zake akikaa kitandani.

" imekuwaje nimeruhusu hasira zinitawale kiasi kile,aaaah" anajitupa kitandani tena " vipi akiniona sifai kabisa" anazidi kujilaumu kwa kuacha hasira zimtawale na aongee mengi kuliko aliyotarajia kusema.

Anasikia mlango ukigongwa anatoka akijivuta na kwenda kufungua anamkuta Sinde.

" Sindee!" anaita akimkumbatia

" Kuna nini? maana tumekuona unarudi unakimbia kama umekimbizwa na Ndesha"

" Sasa hivi naona afadhali hata ningekimbizwa na Ndesha maana najua ningekufa na nisingerudi"

" kumetokea nini?,ulikuwa unalia au?" Sinde anamuuliza akiangalia macho yake.

Sinde aliyekuwa amekuja mda mrefu kumsalimia na Bibi sumbo akamwambia amepeleka chakula mtoni alikaa kwenye kivuli pamoja na Bibi sumbo wakimsubiri,ndipo walipomuona akija akikimbia akaamua Kuja kumuona." njoo tukae hapa kwanza" Tulya anamvuta na kukaa kwenye mkeka.

Tulya anamueleza Kila kitu kilichotokea na anamuona Sinde anabaki mdomo wazi.

" nimechanganyikiwa si ndio aaaah"

" hapana rafiki,umefanya vizuri" Sinde anamwambia.

" kweli?"

" ndio,ulichokifanya ni kuweka ngome kwenye himaya yako tu shida Iko wapi?"

" asije akaniona kichaa"

" hapana,Nina uhakika hicho kitamfanya awe karibu na wewe"

" unadhani hivyo?"

" ndio,atakuwa alikuwa anakaa mbali na wewe kwa sababu labda alijua humpendi,Nina uhakika Sasa hivi na yeye atapiga hatua Kuja kwako"

" naomba iwe hivyo maana akikimbia umbali kuliko alipo hapa sijui nitafanyeje?"

" una waza nini wewe,Tulya barubaru kaenda wapi mbona wewe sio mtu wa kutetereka namna hiyo"

" zamani nilikuwa mwenyewe tu Sinde,Sasa Kuna moyo wa mwanaume mgumu kama jiwe na Nina kibarua Cha kuuulainisha"

" Nina uhakika utakiweza,tangu lini ukarudi nyuma wewe, na hamna mwanaume anayeweza kuvumilia kukaa mbali na mwanamke mrembo kama wewe nina uhakika mwamba ulioko moyoni mwake umeanza kuyeyuka tayari"

Nzagamba huyo hanioni hata kama mwanamke kimoyoni Tulya anamjibu.

" asante Sinde,sijui ningefanyeje bila wewe"

wote wanakumbatiana.

" umefuata nini hapa si ulitakiwa kuwa ndani Sasa hivi wewe?" anamuuliza akimwangalia kwa mashaka." usiniambie umetoroka?"

" unadhani mama angeniacha,Leo ndio mwishomwisho nikaamua nije kukuona maana wewe hutaki Kuja kunisalimia" analalamika Sinde.

" olewa uone" Tulya anamjibu akicheka.

" nilijua nitapata umbea wa mambo ya kitandani kumbe mambo yenyewe hata hayajakokewa moto" Sinde anacheka.

" nadhani utasubiri sana" Tulya anamjibu akivuta pumzi ndefu.

Jua likiwa limetanguliza vidole vyake vya miguu yake chini likiashiria machweo yake kukaribia.Nzagamba anaachana na marafiki zake akiamua kurudi nyumbani mapema kumaliza ugomvi wake na mkewe,akiwa njiani mkononi mwake akiwa amebeba ndege aliowatega akiwafunga kwa pamoja anaona kitu cheupe kimepita Mbele yake na kukimbia upande mwingine wa pili kwenye kichaka.

"nini hicho?" anajiuliza na kuanza kupiga hatua kukisogelea kichaka kwa umakini,anazunguka upande wa pili na kuangalia kwa umakini.alichokiona hakuamini macho yake.

"sungura?!"