Chereads / penzi la bahati / Chapter 39 - chapter 38

Chapter 39 - chapter 38

Anaanza kumwangalia sungura kwa kuhakikisha macho yake hayamdanganyi na kabla hajafanya chochote sungura anakurupuka na kukimbia akimshtua.Haelewi inakuwaje sungura apite karibu yake,atakuwa ametokea wapi kwani Sasa hivi wanyama wamekuwa ni adimu na hata kama wangekuwepo kupita karibu yake sio kitu Cha kawaida,nini kimetokea?

Anajiuliza lakini anaamua kupuzia kwani tayari anajambo la muhimu Sasa hivi,mke wake anamsubiri nyumbani asije akawa bado analia na kujaza nyumba nzima mafuriko kwa machozi yake.

Nzagamba anafika nyumbani giza likiwa tayari limeshaingia anamsikia mama yake akiwa anaimba mwanga hafifu wa kibatari ukionekana kwenye matundu madogomadogo ya nyumba ambayo hayajaziba.Anaenda na kufungua mlango na kumuona Bibi sumbo akiwa anapika.

" shikamoo mama" anamsalimia huku akimpatia ndege aliyokuja nao

" Marahaba mwanangu,habari ya kushinda"

" salama tu habari ya hapa" anamuuliza akiangalia huku na kule mle ndani akitegemea kumuona Tulya lakini hamuoni anajiuliza atakuwa wapi wakati mama yake anapika kwani sio kawaida,tangu amuoe Tulya siku zote amekuwa akipika yeye imekuwaje Leo kamwachia mama yake au atakuwa bado amekasirika anajiuliza na kugeuza haraka kuelekea ndani kwake.

" nzuri,mkeo ..."anajibu Bibi sumbo lakini kabla hajamalizia sentensi yake Nzagamba ameshaondoka.

" ohh,sijui anaharaka ya nini?" anajiuliza Bibi sumbo akisimama kwenye kigoda chake na kuweka ndege katika kijiti kilichochomekwa ukutani karibu na mafika anakopikia akiwaning'niniza kichwa chini miguu juu.

Nzagamba anaingia ndani kwake na kukutana na ukimya anaangalia na kuona moto mdogo ukiwa unawaka kwenye mafiga.

" kwa nini hajawasha taaa?" anauliza anaenda kwenye mafiga anachukua kizinga anakitikisa juu kinatoa mwanga mdogo unaomwonyesha sehemu kilipo kibatari anachukua na kupuliza kizinga na baada ya majaribio matatu kinawaka na kuwasha kibatari .Anakirudisha kizinga mahali pake na kukikinga kibatari chake vizuri na mkono wake Mmoja kisizime kutokana na upepo unaoingia anaelekea chumbani akitembea polepole.

" kwa nini hujawasha taa" anaongea na kuingia chumbani akitegemea majibu lakini anakutana na kitanda kitupu mapigo yake ya moyo yanabadili mwendo " Yuko wapi huyu?" anaweka taa kwenye kibao na kutoka upesi anapiga hatua za haraka kuelekea nyumbani kwa mama yake anausukuma mlango na kutanguliza kichwa, Bibi sumbo anageuka na kumwangalia.

" Tulya yuko wapi?" anauliza

" ndio nilitaka nikwambie wewe ukaondoka,ameenda nyumbani kwao" Nzagamba anausukuma mlango na kuingia mzima mzima ndani.

" nyumbani kwao?umbali wote huo ataondokaje mwenyewe kaondoka saa ngapi na wewe kwa nini umemruhusu mama?" Nzagamba anaongea mfululizo, mapigo yake ya moyo yakienda mbio zaidi asijue afanyeje kama kaondoka kweli.Bibi sumbo anamshangaa imekuwa ni siku nyingi tangu kijana wake aongee maneno mengi kiasi hiki kwa wakati Mmoja.

" kwa Mzee nshana Kuna umbali gani? na kama mtu anaenda kusalimia Mimi nitatumia sababu gani kumzuia"

" kwa Mzee nshana?"

" ndio,kwani wewe ulijua kaenda wapi?" Bibi sumbo anamuuliza akimwangalia kwa wasiwasi kijana wake.Nzagamba anavuta pumzi ndefu maana taarifa ilimpa kimuhe muhe akajua Tulya ameenda nyumbani kwa wazazi wake kabisa himaya ya wafugaji.

" mmegombana au?" anamsikia mama yake akimuuliza.

" hapana,nimeshangaa tu kutokumuona" anajibu akijaribu kuweka sura yake sawa.

" Giza limeshaingia ngoja nikamchukue atapata shida kurudi mwenyewe" anageuka na kutaka kuondoka.

" amesema harudi" anaongea Bibi sumbo na kumfanya Nzagamba ageuke haraka.

" unamaanisha nini?"

" unashtuka shtuka nini? Leo Sinde anaanza kukaa mwali ndani alikuja hapa na wakaondoka wote Ili akasaidie kazi kidogo atarudi kesho shida Iko wapi?"

" oooh,si ungesema hivyo,Sasa wewe ulikuwa unatoa maelezo nusu nusu" anaongea Nzagamba akitoka na kufungu mlango.Akiwa nje anapeleka mkono wake usoni akifuta jasho jembamba lililomtoka.

" bado ana hasira" anaongea akienda na kukaa kwenye kitanda kilichopo nje akivuta pumzi ndefu asijue afanyeje,kusalimiana na Lindiwe asingejua kama kungemuweka matatizoni namna hiii.

Nyumbani kwa Mzee nshana familia nzima ikiwa inakula akiwemo Tulya,isipokuwa Sinde aliyepelekewa chakula chake chumbani kwake. macho ya Zinge yakienda kwa Tulya Kila baada ya muda.Baada ya kumaliza kula anaingiza vyomba ndani anawatakia usiku mwema Mzee nshana na Runde na kuelekea iliko nyumba ya Sinde kwa ajili ya kutafuta malazi.

" Tulya" anamsikia mtu akimwita anang'ata mdomo wake akijua ni nani hasa.

" ndio kaka Zinge" anageuka na kumwangalia Zinge anayepiga hatua haraka na Kuja kusimama alipo.

" umegombana na mumeo?" anamuuliza

" hapana,kwa nini umeuliza?"

"una uhakika?"

" ndio"

"kama una..."

" Zinge unafanya nini twende" wanamsikia Kilinge akimwita.

" haya kalale" anaongea Zinge akigeuka na kuondoka.Tulya anavuta pumzi ndefu akimshukuru Kilinge kumtoa kwenye zamaha ya Zinge anaanza kupiga hatua za haraka kuelekea ndani anafungua mlango na kuingia ndani.

" hakimpiti kitu" anaongea akienda kukaa kitandani alipo Sinde.

" Nani?" Sinde anamuuliza akipandisha miguu yake kitandani.

" kaka Zinge,alikuwa anauliza kama nimegombana na Nzagamba"

" yupo kama kakakuona yule,hafichwi kitu"

" hilo jina umempatia kweli" anacheka Tulya akipanda kitandani.

" utamkimbia mpaka lini?" Sinde anamuuliza akimaanisha Nzagamba.

" iwe lini kesho tu,nipate nguvu za kumkabili"

Sinde anavuta pumzi

" usijali mpaka kesho nitakuwa kama zamani,ninaona aibu tu baada ya kusema nampenda kwa nguvu zote zile nikijua nakataliwa,mpaka kesho atakuwa kasahau kidogo"

" sidhani kama atasahau"

" wewe humjui huyo,Nina uhakika hata ningekuwa hapo Sasa hivi angekuwa na uso mkavu" anaongea Tulya pasipokujua kuwa mwenzake anageuka tu kwenye kitanda chake cha ngozi kama kinamiiba usingizi ukiwa umerukia dirishani na kwenda matembezinj na Hauna haraka ya kurudi hivi karibuni.Baada ya mawazo ya mda mrefu Tulya usingizi unakuja na kufanya umiliki mwilini mwake ukimfanya asahau kidogo zamaha la Leo.

Usiku uliyokuwa mrefu kuliko wote maishani mwa Nzagamba hatimaye umekucha anatoka nje na kuelekea uwani,anawaita mbwa wake na kuwafunga anataka kuondoka lakini miguu yake inampeleka mpaka anakotengenezea Tulya vyungu anaangalia udongo na vyungu vingine vilivyokamilika tayari na macho yake yanaenda kwenye udongo uliokuwa chini ukiwa umetengenezwa tayari kwa matumizi,huu ni udongo ambao Tulya alikuwa anautengeneza kabla Bibi sumbo hajaja kumwambia apeleke chakula na baada ya kuvurugwa haukuwa hata akilini mwake na kumkimbilia kwa mjomba aake. Anainama na kuushika." naona na nyie mlitelekezwa" anauambia udongo.

Siku ikawa mchana na ikawa jioni Nzagamba anarudi nyumbani akitegemea atamkuta mkewe lakini hali anaikuta kama ya jana

" mchana nilikuwa huko akaniambia atakuja jioni hata sijui kinamchelewesha nini?" anaongea Bibi sumbo baada ya kumuona kijana wake akizunguka huku na kule akimtafuta mkewe.

Hasira zinaanza kumpanda Nzagamba akijua Sasa Tulya ameanza kufanya makusudi baada ya kuvuruga kichwa chake kaamua kupotea na kujificha.Anafunga mlango wa nyumba yake uliokuwa wazi na kuanza kuondoka.

" unaenda wapi?" anaauliza Bibi sumbo aliyekuwa ametoka na chakula mkononi kumpatia kijana wake

" narudi sio mda mrefu usinisubiri we nenda kalale tu" Nzagamba anamjibu akiondoka.

Nyumbani kwa Mzee nshana vijana mbalimbali wakiwa wamekaa nje wakipiga ngoma na kucheza kuonyesha maandalizi ya sherehe Nzagamba anafika na kabla hajaingia ndani kabisa anawaona mabinti wakiwa wanacheza na pasipokutumia nguvu nyingi anamuona Tulya akiwa ni miongoni mwao akitikisa njuga akiwa Hana habari kabisa na mambo mengine yanayoendelea duniani kwa wakati huu.

" inavyoonekana Hana hata mpango wa kurudi nyumbani" anajisemea aking'ata meno yake kwa hasira na mikono yake inakunja ngumi akiona vijana wanavyomwangalia.

" samahani unaweza kuniitia Tulya mwambie mumeo kasema mundoke" anamwambia Binti aliyekuwa anapita macho yake yakiwa kwa Tulya kama vile akipepesa macho atapotea.

Tulya akiendelea kuyarudi anasimama baada ya msichana aliyetumwa na Nzagamba kumshika mkono.

" unaambiwa na mumeo muondoke" msichana anamwambia karibu na sikio lake na mwili wa Tulya unakufa ganzi.

"Yuko wapi?" anamuuliza akiangaza macho yake makubwa huku na kule.

" yule pale" mschana anamuonyesha kwa kidole na kuondoka akimwachia msala,macho yake yanakutana na ya Nzagamba na Moja kwa Moja akajua amekwisha.