Download Chereads APP
Chereads App StoreGoogle Play
Chereads

Falling in love is a crime:Kupenda ni kosa la jinai

Author_Bahati
5
Completed
--
NOT RATINGS
9.2k
Views
Synopsis
Catherine ni msichana mrembo ambaye alizama kwenye penzi la Markus.Alimpenda na kujitoa kwa kila kitu lakini yatayomkuta yananifanya ajute kwanini alipenda.
VIEW MORE

Chapter 1 - Sehemu ya 1:kupenda ni kosa la jinai

Catherine na Markus ni wapendanao wenye upendo mkubwa.Catherine alimpenda sana Markus licha ya kwamba familia yake hawakuwa na furaha juu ya mahusiano hayo maana Catherine alilewa sana kwa Markus hata kubeba makosa mbali mbali ya Markus.

"Mimi wala sijali na wala usiwasikilize ."

Haya ni maisha yetu na hakuna mwenye haki ya kuingilia"

Catherine akamueleza Markus wakiwa zao pwani wanapinga upepo wa bahari.markus yeye alikuwa daktari wa rais hivyo alikuwa na hela sana.Ukichanganya na utanashati ndo alikuwa balaa.Wanawake wengi walimpenda sana Markus.Jambo walilokuwa wakijadili ni kuhusu kupeana.

"Kama utakuwa tayari kuwaacha hao wazazi wako na kuja kwangu,nitakuowa sina tatizo."

"Niko tayari."Catherine akakubali haraka haraka na kumfanya Markus amkombatie kwa furaha.

Ghafla simu ya mkononi ya Markus ikaingia meseji na hapo Markus akaifungua.

"Umeshafkilia kuifanya kazi yetu?utapewa milioni arobaini kwa kazi hiyo."

Ujumbe ukasomeka hivyo.Punde ikaingia tena meseji ya m pesa kuwa kapokea kiasi cha shilingi milioni ishirini.

"Je,uko tayari?"Ikatumwa meseji nyingine tena.Hapo Markus akitabasamu na kukubali.

Kazi aliyotakiwa kuifanya ni kumuuwa rais wa nchi ya Ghana Dr Sebastian Steve ama double s.Agizo lilitokea kwa waziri wa mambo ya nje wa Msumbiji.

"Nani huyo mpenzi?"Catherine akauliza kwa sauti ya chini.

"Watu wa kawaida tu.kuna kazi ambayo wanataka nifanye."

"Ipi hiyo?"

"Je... unataka kunisaidia?"Markus akauliza akimtazana mrembo huyo kutoka juu hadi chini.Ni mrembo kweli.

"Kama itawezekana."Catherine akakubali bila kujua ni kazi gani.

"Basi sawa,tunaweza kuelekea nyumbani kwa sasa?"

Markus akauliza na kumshika begani mrembo huyo kutoka pale taratibu.Akamuacha Catherine nje ya nyumba yao na kumuaga kwa tabasamu pana.

"Uwe na usiku mwema."Catherine akaaga na kuingia ndani.Markus alikua akimtazana tu hadi alipopotelea ndani.

"Ni mwanamme mrembo kweli kweli na mwenye mapenzi ya dhati.Je, mbona kama nahisi kumtumia kwenye kazi yangu?"Markus akajiuliza .Akaondoa tu gari eneo lile.Moja kwa moja akaelekea maeneo ya club ambapo angekutana na watu waliompa kazi