Chapter 5 - Sehemu ya 5: mwisho

Catherine akafikishwa mbele ya mahakama.Kesi yake haikuwa na utetezi wowote lakini Catherine alikuwa na imani juu ya maneno ya Markus kuwa angekuja kumtetea.Kila shitaka alikuwa kimya.Kaka yake alijitahidi sana kumtetea lakini wapi.

Catherine akahukumiwa khukumu ambayo kila mmoja alishika kichwa chake kwa kumhurumia.Cathe akahukumiwa kunyongwa! Mama yake akadondoka chini na kupoteza maisha.

"Mama!$Cathe akataka kumsogelea lakini akazuiwa na kuvutwa msobe msobe kwenda kwenye gari la polisi.Kwa mbali akamuona Markus akiwa na mwanamke mwingine.Markus akatabasamu na kumpungia mkono Catherine ishara ya kumuaga.

Tayari alishalipwa fedha nyingi mno na hapo ilikuwa safari kwenda Dubai kula Bata.Hapo ndo akili ikaanza kumjia lakini alishachelewa.

Kitanzi hatimaye kikawa mbele yake.Kila alipopepesa macho hakumuona cha Markus wala nani.Alisalitiwa vibaya sana.Mwisho macho yake yakatua kwenye kitanzi ambacho kingekuwa halali yake karibuni.Hapo ndio akaamini kwamba asiye sikia la mkuu huvunjika guu.Angemsikiliza mama yake huenda angekuwa salama.

"Markus nakuchukia mshenzi wewe!"Catherine akalia lakini chozi la mjinga halina thamani.

FUNZO

Usipende kupitiliza.

Sikiliza maneno ya wazazi wako maana asiye sikia la mkuu huvunjika guu.

Kiburi si maungwana.

Fikiria kabla ya kutenda.

Usimwamini mtu kupitiliza.