Chereads / Falling in love is a crime:Kupenda ni kosa la jinai / Chapter 4 - Sehemu ya 4:Ndoto yangu itatimia

Chapter 4 - Sehemu ya 4:Ndoto yangu itatimia

"Kwann usiipeleke mwenyewe."Akauliza Catherine.

"Tafadhali,si unanipenda eeeh..nataka nikuowe lakini kwaz, hebu fanya hili."Markus akabembeleza.Cathe akafikiria kwa muda na kukubali.Markus akatabasamu na kurudi chumbani kwa rais.

"Samahani,nilikuwa napokea simu Mheshimiwa rais."

"Hakuna shida."

Markus akaitoa sindano ya dawa ya kutuliza maumivu na kumchoma kisha akamtumia meseji Catherine aje ndani ambapo Catherine akaja kama nesi mpya.

"Dawa hii hapa Dr Markus."Catherine akasema akimpa sindano.

"Mchome basi.Umebahatika kumtibu rais nesi Catherine."Markus akasema kauli za mafumbo.Cathe akatabasamu na kumshika mkono rais.

"Natumaini baada ya hili ndoto yangu itatimia."

Catherine akasema akimaanisha ndoto ya kuolewa na Markus, mwanaume ampendae.Basi akamchoma sindano rais.

"Narudi sio mda.Akiingia mtu chochote atakacho kuuliza sema ndio.sawa? Kwaajili yangu na nitakuowa."

Markus akasema na kutoka baada ya Catherine kukubali.Maskini Catherine tayari alipofushwa na mapenzi.Baada ya Markus kutoka akawataarifu walinzi wakamtazame rais wajue usalama wake.

Hapo wakamfuma Catherine akiwa anamwagia maji rais.

"We nani?"Walinzi wakamuuliza Catherine ambaye akajitambulisha kama nesi.

"Una kitambulisho cha unesi?"

"Hapana sina."

Mlinzi mmoja akaitazama sindano na kuiokota .

"Muite Dr Markus haraka."Akaagiza mlinzi mkuu na hapo Markus akaletwa.Markus akajifanya kushangaa kama hajui chochote kile.Akampima rais ambapo akagundua kwamba amefariki.

"Umetumwa eeeh..."Mlinzi mkuu akafoka na kumpiga kofi zito Catherine.

Catherine akamtazama Markus asijue cha kujibu.Kabla hajasema chochote.. Markus akamvuta pembeni na kumbananisha ukutani.Walinzi wote walikuwa Bize na raisi.

"Markus nini hii?"Catherine akauliza.markus akamshika Catherine mashavu kwa upendo na kumueleza;

"hiki ndicho kipimo cha upendo wako kwangu Catherine, Tafadhali kubali kila kitu watakacho kuuliza.Nitakuja kukutetea pale mahakamani na ukweli utajulikana."Nitakuja na mawakili wengi kwa ajili yako.Tafadhali."

Markus akamshawishi Catherine ambaye akakubali.Oh ni mpumbavu kiasi gani.Mapenzi na imani kwa Markus ilizidi akili yake.Markus akaachia tabasamu pana.Mpango wake umefanikiwa kirahisi.