Chereads / Falling in love is a crime:Kupenda ni kosa la jinai / Chapter 2 - Sehemu ya 2:kitu kidogo sana

Chapter 2 - Sehemu ya 2:kitu kidogo sana

Kwenye meza moja iliyosheheni vinywaji alikuwa ameketi mwanaume aliyevalia suti nyeusi miwani akipata kinywaji taratibu.Markus akamsogelea na kukaa kando yake.

"Naitwa Dr Markus."

Markus akajitambulisha wakipeana mikono.

"Kwa hiyo umeamua nini kuhusu dili letu?"Akauliza yule mtu kwa sauti ya unyenyekevu.

"Nimekubali ila tu kama mutanihakikishia usalama wangu "

"Usalama tu!Usalama kwangu ni kitu kidogo sana wala usiogope.Unachotakiwa kufanya ni kumchoma sindano ya sumu ambayo nitakupatia na muache.Sawa?"

"Sawa."

"Utalipwa zaidi ya milioni sabini tena kwa kazi hiyo."Yule mwanaume akasema na kumtoa macho Markus kwa uchu.Sindano ikaletwa ikiwa katika sanduku dogo na kumkabidhi Markus.

"Ulishamaliza kazi,utapewa malipo yako.Tutakutana sehemu ya..."Yule mwanaume akasita kutaja eneo.

"Nitakujulisha usijali."Akasema na kutoka . Markus akatabasamu na kutoka pia.

"Unatoka wapi wewe mtoto?Hivi huyo Markus wako ndiye anakupa jeuri na kiburi?"

Mama Catherine akafoka baada ya Catherine kuingia ndani.

"Usinichekeshe mama,mimi sio mtoto.niache na Markus wangu."

"Catherine!!"

"Nini mama?nimekuchoka ujue..."

"Kama umenichoka ondoka nyumbani kwangu.sikuhitaji mtoto wewe kha!"

"Naondoka ujue..."Catherine akakimbia kwenda ndani akiwa na hasira tayari kwa kuondoka.

"Kha!Huyu mtoto mbona anakuwa namna hii jamani.kweli kuzaa kutoa maradhi."Mama Catherine akalalamika .

Punde Catherine akatoka ndani akiwa na begi lake.

"Kwaheri.Naondoka zangu."Catherine akaaga huku akitoka nje.

"Aya si umeamua,nenda "Mama Catherine akasema ingawa roho ilimuuma.Cathe ndo mtoto pekee wa kike mbali na mkubwa ambaye ni mwanasheria, Steve.Steve alikuwa akimtazana tu dada yake akiondoka.

Catherine akafoka nyumbani kwa Markus na kumuita.Akaelekea chumbani na kufungua mlango.Hapo macho yake yakagongana na ya Markus ambaye alilala kitandani.

Kabla hajatoa neno lolote.. mlango wa bafuni ukafunguliwa na kutoka mwanamke akiwa kavalia taulo.