Yule mwanamke akamtazama Markus kisha Catherine kwa dharau kutoka juu hadi chini kwa nyodo na kukaa kando ya Markus.
"Nani huyu mpenzi?"Akauliza Julieth yule mwanamke.Markus akasimama na kumtazama Catherine ambaye tayari michuzi ilianza kumtoka.
"Catherine....."Markus akataka kumsogelea lakini Catherine akaondoka akilia mno.
"Shit!!!"Markus akapiga meza kwa hasira.hakupenda kilichotokea.
Catherine akarudi kwao akilia mno.Steve na mama yake wakabaki tu kumshangaa.
"Tayari yashamsibu huko."Steve akasema na kumpotezea tu Catherine. Catherine Wala hakulala.Alikua akilia mno juu ya kilichotokea.Inamaana Markus kamsaliti sio?
Simu ya Catherine ikaita pale ambapo alikuwa karibu kuikata na kugundua ni Markus.Kwa hasira akaipokea.
"Unataka nini?"Catherine Akauliza kwa sauti ya kutaka kulia.
"Samahani Catherine lakini naomba tu mimi na wewe tukutane.Sijui uko tayari?"
Akauliza Markus.
"Wapi?"
"Mount Meru hotel."Markus akataja.Hiyo siku ndiyo siku ambayo Markus alipaswa amuue rais.
Rais alikuwa na mkewe kwenye hoteli hiyo wakila Bata taratibu.
Nafasi ya kumuua ikaja baada ya rais kwenda kupumzika mwenyewe.
"Mheshimiwa hii dawa itakupa nguvu."Akasema Markus baada ya walinzi kuondolewa chumbani.
"Saw,bora tu inaponyesha." Rais akasema.
"Samahani kidogo..."Markus akatoka nje baada ya kupokea ujumbe wa sms ya Catherine kua amefika. Markus akamvuta pembeni.
"Catherine tafadhali.. naomba unisaidie tu kubeba hii dawa na uilete kwenye chumba cha rais.sawa? utasema wewe ni msaidizi wangu."Markus akaomba akimpa ile sindano ya sumu.