"Nimekuuliza ulikuwa unafanya nini na Lindiwe?" Tulya anauliza machozi yakitaka kuonyesha kazi Yao.
" wewe unadhani nilikuwa nafanya nini?"Nzagamba anamuuliza naye hasira zikianza kumpanda.Tulya anamwangalia kwa mshangao ni Moja kati ya majibu aliyekuwa anayatarajia lakini hakujua kama lingemchoma kiasi hiki.Ukweli ni kuwa Tulya alikuwa hataki kuzungumzia hili kwani hakuwa na nguvu za kukabiliana na ukweli,lakini pia hakutaka hali iendelee na isitoshe yule mbwa mwitu anaziti kujisogeza hivyo akaamua kurudi na Kuja kulimaliza hili Moja kwa moja.Lakini Sasa ameanza kujutia uamuzi wake wa kurudi kwani Hali inakoelekea ni mbaya kuliko alivyodhani.
Anainamisha macho yake chini na chozi linamdondoka kwenye jicho lake Moja anafuta haraka kwa kiganja chake cha mkono anainua macho yake na kumwangalia tena.Nzagamba anashangaa kuona maumivu machoni mwake lakini anaamua kuyapotezea macho yake yanenda kwenye mtego wake na kuona ndege wakiwa bado wamenasa pale wakitafuta jitihada za kujiokoa.
Tulya anafuata macho ya Nzagamba na kuwaona wale ndege wakiangaika kwenye mtego.kwa haraka haraka anajiona yeye ni sawa na wale ndege kwani wote wamenasa kwenye mtego na mtu pekee anayeweza kuamua hatima Yao ni Nzagamba peke yake ama awachie huru au awafanye vitoweo.kwake yeye hakuna ahueni kwa njia zote mbili kuwa huru ni kuwa mbali na Nzagamba na kwa hatua hii aliyofikia sidhani kama lingekuwa ni chaguo jema kwani ana uhakika hawezi kukaa mbali na Nzagamba na kuwa kitoweo ni kubaki akimwangalia Nzagamba akiwa na Lindiwe asiseme chochote kwani wakati anaolewa alijua wazi kuwa Nzagamba anampenda Lindiwe hilo halitauma si eti, ukweli ulikuwepo kuanzia mwanzo si ndio.alijua baada ya muda Nzagamba atamsahau Lindiwe lakini kwa upepo unakovuma ni dira nyingine kabisa.
" sema kilichokuleta Nina kazi mimi" anashtuliwa na sauti yake Nene anatoa macho yake kwenye mtego na kumwangalia tena nzagamba.anashika vidole vyake vilivyokuwa vimelowa jasho na kuvifikicha asijue aseme nini na baada ya muda anaongea kile kilichokuja mdomoni mwake kuliko akae kama bubu.
" unarudiana nae?"
" mhhh?!"
" unarudiana na Lindiwe?" anauliza safari hii akimwangalia usoni akitarajia kuona mabadiliko yoyote. 'anawaza nini huyu mwanamke?" anajiuliza Nzagamba.
" wewe unaonaje?" na yeye anamuuliza swali tena.
Tulya anang'ata mdomo wake akizuia asije akapiga ukunga mwili wake ukimtetemeka.
' anamaanisha nini? ndio anarudiana naye au vipi?' anajiuliza.
" kama huna Cha kuongea rudi nyumbani" anaongea akijitahidi kuzuia hasira yake inamaana haoni hata shida yeye kuwa na mwanamke mwingine na kwanza anamchukuliaje,yeye wakutembea na wake za watu anajiuliza Nzagamba na kuanza kupiga hatua kuelekea mtoni.
" ulisema nikupe mda" anasikia sauti ya Tulya na kusimama anageuka na kumwangalia.
" ulisema nikupe mda Nzagamba,na nimefanya hivyo,nimekuachia nafasi uliokuwa unaitaka,lakini...lakini bado tu unataka kurudi kwa huyo mwanamke" anaongea maneno yake ya mwisho yakififia kwani machozi tayari yalikuwa yanamdondoka.
" kwa nini hutaki kuupatia uhusiano wetu nafasi,sababu tu ya mwanamke aliyekuacha na ameshaolewa na wewe umeshaoa kwani ni lazima mfanye uchafu wenu kwa nini msituheshimu wenza wenu,kumbuka alikuacha Nzagamba na..na..na kwa nini usimsahau tu" Anaongea yeye mwenyewe asijue anaongea ujinga gani kwani pointi zote alizozipanga Kuja kuongea zimeshamtelekeza baada ya kufika hapa Hana hata Moja.
" wewe umeshasahau?" Nzagamba anamuuliza asijue swali linatoka wapi?
" ehhe?!"
" niambie Tulya kwa nini uliolewa na mimi?" anapiga hatua kubwa mbili tu na miguu yake mirefu na tayari alikuwa karibu kabisa akili ya Tulya inamtuma apige hatua nyuma lakini miguu yake inamsaliti na kuganda pale chini.
" ehhe?!"
" niambie kwa nini uliolewa na mimi?" safari hii kamba zote zilizofunga hasira ya Nzagamba zikianza kukatika Moja baada ya nyingine,amechoshwa na huyu mwanamke kwanza ameolewa naye kwa michezo yake ya kijinga,pili akaamua kukaa na kujifanya mke mwema na kujifanya hajali chochote,kumbe akiwa na mengi ya kuficha na pia mwanaume anayempenda na hajui waliachana kwa sababu gani itakuwa aliona ukichaa wake lakini anakumbuka alimsikia sinde akisema yule mwanaume bado anampenda Sasa kiliwasibu nini anaamua kupotezea kwani hataki kujua yeye anachotaka ni huyu mwanamke kuacha kucheza na akili yake.
" nili...hiyo..kwa sababu..."
" acha Tulya" anashtuliwa na sauti yake Kali na ya juu anafumbua macho kwa mshtuko na mikono yake inakimbilia kifuani kushikilia roho yake isimtoke.
" nimechoshwa na michezo yako ya ajabuajabu katafute mtu mwingine wa kucheza naye"
" unamaanisha nini michezo yangu" anaongea akishukuru tu sauti yake kuwa bado ipo kwa hali hii asingeshangaa kama nayo ingemtelekeza.
" unajua nini,Mimi nimeshazoea kuishi mwenyewe na ninauwezo wa kuishi mwenyewe mpaka kifo changu,unaweza kuondoka na ukaishi maisha yako,kwa sababu sihitaji huruma zako wala za mtu yeyote yule"
" unasemaje?" Tulya anauliza asimini kuwa huyu mwanaume anatafuta njia ya kumtoa Ili arudiane na mwanamke wake anawaza Tulya pasipokujua kuwa wote wawili wanatembea njia Moja lakini bado wanajiona wako njia tofauti.kwani Kila Mmoja anafikiria mwenzake anataka kumuacha.
" unaona ndoa ni mchezo au,unaamua tu kuwa niondoke na Mimi nitakutii,kama unataka kufanya uzinzi na huyo Lindiwe wako fanyeni tu lakini Mimi siondoki" Tulya naye anakuja juu.
" kwa nini ubaki na Mimi?Nina uhakika Kuna wanaume wengi sana wanaotaka kukuoa na bado wanakupenda" anaongea Nzagamba maneno ya mwisho akikazia kwani hataki hata kumkumbuka huyo mwanaume aliyemuona mnadani anayeoneka tajiri pia,sio kama yeye mwenye kuandamwa na mikosi na afadhali mikosi hiyo vitu vingekuwa vinamfata angebahatisha kukamata hata kimoja tu lakini yeye vinamkimbia,ukiwaza vizuri nadhani hawakuelelezea mkosi wake vizuri au hawakujua tu ila kwa hivi Sasa amegundua kuwa mkosi wake unahusisha wanawake kumkimbua pia.
Lakini yeye ahusike vipi na Kuja kwa Tulya aliyesema anataka mwenyewe kuolewa naye na Sasa anataka kumkimbia tena labda kachoka na kachoka kabla hata msimu haujapinduka umesahau kuwa aliolewa na wewe kwa kukwepa ndoa yake na Manumbu alijua akiolewa na Manumbu asingemuacha aondoke kiurahisi tofauti na wewe ambaye angepata sababu kiurahisi ya kukukimbia.
Akili yake inaendelea kuzunguka na kuzunguka pasipo kujua kua anajiumiza mwenyewe kwa kujipeleka mbele kimawazo.
Woga wa kuachwa umekuwa ni sehemu kubwa kwenye maisha yake akijua Kila mtu atakuja kwake na kupita kwani hawawezi kustahimili maisha yake akasahau kumuona mwanamke aliyekuwa pembeni yake akifanya juhudi za kupata moyo wake sio kama hajamuona bali hajataka kumkubali na alichokuwa anakifanya ni kuupunguzia moyo wake maumivu kwani anajua safari hii ukidhurika kiungo hicho Cha mwili wake hakitakuwa na nguvu ya kuinuka tena hata kuwa na nguvu za kuuguza kidonda kwani anajua safari hii atakuwa amepigwa na mshale wenye sumu na sumu hiyo itaenea mwili mzima.
" acha kuigiza kama unajali Tulya,kwani ninajua haujali hata kidogo,hiyo michezo yako usinihusishe Mimi,uliolewa na mimi kukwepa kuolewa na Manumbu na kama unataka kuondoka nenda Mimi sitakuzuia,kwa hiyo acha kupindisha maneno na kutafuta sababu za kuondoka Mimi nitakurahisishia usitoke jasho"
Tulya anang'ata midomo yake akizuia kulia zaidi hasira ikimpanda,anajua nimeolewa nae kwa mchezo hivi haoni ninavyomvumilia ananifukuzaje utadhani Mimi sio mkewe.
" nenda nyumbani,sitaki kualika umati huku mtoni watushuhudie tukigombana isitoshe hiyo itakuwa sifa mbaya kwako itakuharibia usiolewe tena" anapiga hatua na kurudi nyuma akiacha nafasi kati yao.
" hivi unajua kwa nini niliolewa na wewe?"
" acha maigizo ni mtoni huku Tulya"anamkanya.
" nimeolewa na wewe sababu nakupenda" anaongea kwa nguvu kidogo sauti yake ikiwa na hasira.Lakini Nzagamba anamwangalia kama kakutana na mzima wa Kijiji.mapigi ya moyo wake yanapanda juu ghafla na mwili wake unahisi kufa ganzi akili yake inashindwa kufanya kazi kwa mda.
" ndio,nilikupenda tangu siku ya kwanza nilipokuona kwenye siku ya tambiko,hapana..hapana..nilikupenda hata kabla sijawahi kukuona" anaongea machozi yakimtoka asijue ameishiaje na mwanaume huyu ambaye anadhani hatakuja ampende kamwe.tumaini lake lilikuwa linafifia lakini anaona ni bora azitoe hisia zake liwalo na liwe.
Nzagamba anabaki akimshangaa tu,habari hakujua aipokeeje.
" nakupenda"