Anageuka na kumwangalia aliyepamiana nae na kukutana na vijana wawili wenye umri mkubwa kuliko yeye kama miaka mitano hivi.
" angalia unakoenda kijana" anaongea Mmoja wao.
" samahani" anaomba radhi akiwaangalia,hajawahi kuwaona Hawa watu Kijijini hapa.
" kama umekuja kucheza ngoma na kukesha Haina shida karibu" anaongea mwingine akimwangalia nzagamba kwa makini.
" hapana niliku..." kabla hajamalizia anasikia mtu mwingine akiita nyuma yake.
" kaka lengi mmerudi"
ilikuwa ni sauti ya sinde na nzagamba anaijua vizuri sana na hakutaka mtu yeyote amuone hapa anafanya haraka na kuondoka kabla sinde hajafika walipo.
" ndio sinde,habari ya jioni" anaongea Mmoja aliyejulikana kwa jina la lengi.
" salama tu shikamoni" sinde anasalimia kwa heshima macho yake yakimwangalia mtu aliyekuwa akipotea maeneo yale.
" Marahaba" wote wanaitikia na wakifuatiza uelekeo wa macho ya sinde alikopotelea nzagamba.
" unamjua yule?"
" kama nimemfananisha vile lakini sina uhakika kama ni yeye, kaka wengine wako wapi?" anauliza sinde baada ya kuona idadi Yao pungufu na walivyoondoka.
" tumewaacha huko bado Wanaongea si unajua vijana" anaongea mwingine wakianza kutembea kuelekea ilipo nyumba na walipokaa watu wengine.
sinde anacheka kidogo na kusema " kwani wewe kaka kiila ni Mzee?"
" ndio,wewe hunioni?" anajibu kiila akimwangalia sinde usoni na lengi aliyekuwa akiwasikiliza anaongezea.
" kiila ana Binti umri kama wewe Yuko mwali anatoka mwaka ukigeuka"
sinde anamwangalia kwa mshangao na wote wawili wanacheka.
" mmerudi?" ilikuwa ni sauti ya zunde aliyewaona wakiingia uani.
" ndio mama mdogo" anaitikia lengi
" mnahitaji chakula?" anauliza akimtupia jicho sinde aliyesimama pembeni kama kumuuliza anafanya nini pale.
" hapana,tumekunywa pombe na nyama choma tulipokuwa kwa hiyo Haina haja ya chakula Leo jioni" anajibu lengi.
" haya Mimi nawaacha naenda ndani kwa tulya" anaaga sinde.
" ndio,nenda mdogo wangu atakuwa kapozewa kukaa peke yake sisi tutakuwa sawa" anajibu kiila akimwangalia sinde.
wote wanamwangalia sinde akiondoka na macho yao kuyarudisha kwa mama Yao mdogo zunde.
" baba Yuko wapi?" anauliza kiila.
" yupo huko nyuma na wazee wenzie zungukeni mtamkuta na mkihitaji kitu chochote mtanijulisha sitakuwa mbali"
wanaitikia kwa kichwa na kuanza kuondoka kuelekea upande wa pili wa nyumba.
Sinde anafika aliko tulya na kumkuta amejilaza kitandani.
" naona Leo utalala vizuri" anaongea na kumfanya tulya amwangalie.
" siwezi Leo naona mawazo yamezidi zaidi,msishangae kesho mkikutana na bibi harusi ana macho mekundu kama kapaliwa mate ya ugolo" anajibu tulya akijigeuza pale kitandani na kufanya ngozi ya mnyama iliyotandikwa pale kitandani kupiga ukelele kidogo,Sasa mgogo wake ukiwa kitandani na uso wake kuangalia dari.
Sinde anacheka kidogo akienda kukaa kitandani hapo.
" Haina haja ya kuficha Mimi na wewe tena hamna Siri kati yetu acha kujifanya"
Tulya anatoa macho yake darini na kumwangalia sinde aliyekuwa akitabasamu jino kwa jino akionyesha mwanya aliourithi kwa mama yake.
" unamaanisha nini?mbona sikuelewi?"
"nzagamba" anamjibu kwa sauti ya chini.
" kafanyeje?" tulya anamuuliza kwani hajui sinde anazungumzia nini.
sinde anamwangalia tulya na kuona kuwa atakuwa hajui chochote
" kwani hajafika hapa?hujaonana nae?" anajikuta akiuliza maswali tena.
" sinde,hapa tayari kichwa kinanipasuka usinioongezee zaidi, hembu ongea vizuri nikuelewe" anautoa mgongo wake juu ya ngozi na kukaa akimwangalia sinde vizuri.
kutokana na kumsubiri kwa mda mrefu tulya alishakata tamaa kabisa kuwa nzagamba atakuja kumuona hivyo alishalifuta kabisa wazo hilo ukizingatia Leo ni siku ya mwisho na watu ni wengi hakuwa na tumaini kabisa.
" nimemuona nzagamba njee nikajua katokea hapa?"
" nini?mda gani? na wapi?"
tulya anamtupia maswali huku miguu yake ikitua chini tayari kwa kusimama atoke lakini sinde anamkata maini.
" nje na ameshaondoka imekuwa mda kidogo"
Tulya anakaa akifumba macho yake kwa viganja vya mikono yake.
" kwa nini unaniambia Sasa hivi" anaongea tulya akijilaumu siku zote hukaa nje akimsubiri na haji Leo tu hajatoka kutokana na watu wengi waliopo nje na amekuja,angejua kama angekuja angekaa hivyo hivyo hata kama watu wangemuona wa ajabu.
" Mimi nilijua katoka hapa ndio maana sikuwa na haraka ya kufikisha ujumbe"
" una uhakika alikuwa ni yeye?"
" nilimuona akiongea na kaka zako nilipofika akaondoka sikumuona uso ila ule mgongo ulikuwa wake kabisa"
Tulya anavuta pumzi ndefu akimwangalia sinde " kwa hiyo umeona mgongo ukajua ni yeye?"
" na mwendo wake,si unajua nzagamba ni watofauti kama mbuzi mweusi katikati ya weupe au mweupe katikati ya weusi"
tulya anapanda kitandani akimpuuzia sinde
" ndio ni watofauti ndio maana hawezi Kuja hapa"
" nina uhakika ni yeye"
" sinde,unaweza kuniacha nipumzike tafadhali"
" mmh! sawa" anaitikia sinde akijisikia vibaya kufikisha taarifa zisizo kamili na kumuumiza moyo tulya,yeye alikuwa na uhakika kuwa nzagamba ameonana na tulya ndio maana akapata shauku ya udaku angejuaje kama hajafika hapa lakini ana uhakika alikuwa ni yeye aliyemuona,macho yake hayawezi kumdanganya
" nilimwambia kabisa aje,mwanaume asiye na shukrani" anatema cheche sinde.
" nani ulimwambia aje?"
" mmh!"
Anashtuka sinde asijue kama kaongea kwa nguvu.tulya anakaa tena kitandani
" sinde,usiniambie ulionana na nzagamba na ukamwambia aje kuniona?"
sinde anabaki akimwangalia tu.
" niambie ukweli" tulya anaongea kwa ukali na kumfanya sinde ashtuke alipokuwa amekaa.
" nilitaka tu kukusaidia sababu ulikuwa unamsubiri Kila siku"
" kwa sababu nilikuwa nataka aje mwenyewe pasipo kulazimishwa sinde,tayari nimeshamlazimisha anioe sitaki kufanya Mambo yatakayo mfanya anichukie zaidi na wewe ukaenda kumwambia aje kuniona.Nina uhakika alijua Mimi ndio nimekutuma"
" nilimwambia nimekuja mwenyewe wewe hujui"
" atakuamini Sasa"
" samahani,Mimi nilitaka tu kukusaidia"
" nahitaji kupumzika kesho Nina safari ndefu"
anaongea na kulala kitandani akimpatia sinde mgongo na kufumba macho yake.
Mbali na nyumbani kwa Mzee Shana kwenye kianda Cha vijana nzagamba anarudi na kuwakuta wenzake bado wakinywa pombe.
Anajisogeza na kukaa Mahali alipokuwa amekaa awali.
" msalani gani huko masaa,kidogo tuanze kupiga mbiu ya kupotea kwa bwana harusi usiku kabla ya ndoa" anatania mkita pombe ikianza kumkolea.
" mnajua nilikoenda" anawajibu nzagamba akichukua kipeo Cha pombe kilichokuwa chini na kukipeleka mdomoni.
"sisi tutajuaje ulikoenda" anauliza ntula aliyekuwa akitengeneza Kiko yake vizuri tayari kuipeleka mdomoni kuvuta.
" si mliongea makusudi Ili niende" anaongea nzagamba akijua mpango wa marafiki zake na kumfanya lingo acheke.
" huyo ndio nzagamba bwana"
" vipi umeonana nae?" anauliza kilinge na nzagamba anaitikia kwa kutikisa kichwa kwa ishara ya kukataa na kuendelea
" watu ni wengi sana,sikufanikiwa"
" mmh,angalau umejaribu" anaongea kilinge na kuendelea
" mwangalie vizuri tulya ukimuoa,ni mwanamke mzuri sana ukimjua vizuri, ukimpiga kama manumbu ujue sitakuchukulia kirahisi"
nzagamba hatii neno macho yake yakiwa kwenye moto uliokuwa ukiwaka katikati Yao akijua kuanzia kesho Mambo yatabadilika.
Baada ya kurudi nyumbani nzagamba anajitupa kitandani kwake akiliangalia Dari mkono wake mmoja ukiwa chini ya kichwa chake na mwingine akiutumia kigasha Cha mkono kufunika uso wake akijaribu kupata usingizi asijue kama itawezekana kutokana na makelele ya ngoma na nyimbo zilizokuwa zikipigwa nje na watu waliokuja kukesha nyumbani kwake kusubiria siku ya harusi yake.kwa mtu asiyependa makelele angewambia waondoke lakini Hana jinsi kutoka na Mila na desturi itambidi avumilie kwa siku ya Leo na kesho kwani siku hizo mbili hazitakuwa na utulivu kwake.
Hayawi hayawi yamekuwa siku ilikuwa ikitarajiwa imewadia,rangi ya dhahabu ya jua la asubuhi inawaangazia watu wa Kijiji Cha rumo na himaya ya mpuli kwa ujumla,ndege wa angani wakipiga kelele na kuchangamsha mbawa zao kuikaribisha asubuhi.
Zunde na runde Wanaingia chumbani kwa tulya na kukuta akiwa bado amelala,tulya ambaye hakupata usingizi vizuri usiku kutokana na mawazo pamoja na makelele ya ngoma za usiku usingizi ndio unamjia Sasa.
wakati zunde na runde wakimwangalia anaingia sinde akiwa na kifurushi mkononi.
" ulienda wapi asubuhi hii na kumwacha mwenzio?" runde anamuuliza Binti yake.
" nilienda kuchukua nguo yangu" anaangalia na kumwona tulya akiwa amelala.
" mwacheni msimwamshe alale kidogo,usiku hajalala" sinde anawaambia mama na shangazi yake.
" maskini mwanangu atakuwa na mengi kichwani" anaongea zunde macho yake yakiwa kwa tulya,runde anamshika bega kumfariji.
" usijali tulya ni shupavu sana Nina uhakika atakuwa sawa."
Zunde anaitikia kwa kichwa akifuta machozi yake yaliokuwa yanatishia kudondoka chini.
" sinde mwangalie akiamka umpe chakula na utamsaidia kujiandaa shangazi zake watakuja kukusaidia,mfanye haraka tusije tukachelewa sawa" runde anatoa maelezo kwa Binti yake.
" sawa mama,lakini mbona bado mapema si tunaondoka baada ya jua la mchana"
" haraka haraka haina baraka sinde,Bora tujiandae pole pole kuliko tuharakishe tuharibu" runde anamkazia Binti yake.
" twende wifi" anamwambia zunde na wote wanatoka chumbani wakimwacha sinde.
" ngoja kwanza nijaribu nguo yangu" anajisemea sinde nakuanza kufungua kifurushi chake.
mchana unapofika tayari tulya alikwisha kuoga akiwa chumbani kwake na shangazi zake wawili pamoja na sinde wakimsaidia kuvaa.
"nkeli avae kwanza nguo ndio tutamalizia na nywele" anaongea shangazi yake tulya aliyemuona mdogo wake akianza kumchana nywele na kuendelea
" sinde lete hiyo sketi yake hapo"
Sinde anachukua sketi iliyotengenezwa kwa ngozi na kuchanwa chanwa kwa chini na kufanya vimikanda vidogo vidogo vikining'inia pamoja na shanga za aina mbalimbali zilizoshonewa kwenye sketi hiyo liyokuwa juu ya kiti Cha miti na kumpatia tulya.
Tulya anachukua na kuivaa anajiangalia na kuona imemkaa vizuri kabisa,sinde anampa na ya juu avae.tulya anachukua na kuivaa brauzi yake ikiwa ni ya ngozi vilevile lakini isiwe ya kufunga kama zingine na isifike kiunoni kuacha kitovu Chake nje na iliyofanya maziwa yake saa sita kifuani yaoneka vizuri kwani yalikuwa hayajakabwa kwa kufungwa.
" mama mkwe wako amekutengenezea nguo nzuri sana,ona tyale" anaongea shangazi yake nkeli huku akimwita mwenzake aone aliyekuwa akitengeneza shanga na alikuwa hajamuona tulya.
" kweli, kapendeza sana" shangazi yake tyale anamsifia na tulya anatoa tabasamu.
" na ni mrembo pia" anaongezea sinde asiyepitwa.
" ndio, mpwa wangu ni mrembo sana" tyale anaongezea akicheka.
" nashangaa tu kuolewa na huyo mwanaume asiye na chochote asiweze hata kumlisha vizuri" anaongea nkeli ambaye hajafurahishwa na tulya kuolewa na nzagamba.
" shangazi tulishaongea kuhusu hilo lakini"
" najua,ila Mimi ni shangazi yako huwezi kunizuia kuwa na wasiwasi juu yako sawa,Nina hofia tu utaishije"
" usiwe na wasiwasi shangazi nitakuwa sawa"
lakini licha ya tulya kumwakikishia kuwa atakuwa sawa shangazi nkeli alikuwa hajapendezwa na nzagamba na alitaka mpwa wake aolewe na mwanaume mwenye uwezo angalau kwa familia Yao kuongeza utajiri na nkeli alikuwa Yuko kipaumbele sana huko nyuma kumtafutia wachumba tulya na kuwaambia wazazi wake.
Na sio kama tulya alikuwa hajui kama shangazi yake alikuwa akimnadi kwa faida yake ya kutaka Mali na uhusiano Mpana na watu wenye Mali nyingi akimtumia yeye.hivyo tulya kuolewa na nzagamba ni kama kamfanya akabwe na mfupa wa samaki kooni asijue namna ya kuutoa.
" atakulisha nini huyo na uzuri wako wote umejihari..." kabla hajaendelea mdogo wake anamkatisha akijua watagombana na kuharibu siku bure kwani wote ni wabishi.
" tunachekewa dada,aanze kuvaa hizo shanga" anaongea tyale
" ndio na bangili" sinde nae anadakia aliyeanza kuona Hali ya hewa nzito mle chumbani.tulya anawapatia tabasamu kwa msaada wao kwani hakuwa kwenye Hali ya kugombana na mtu siku ya Leo.
Anavaa bangili mikono yote miwili,wanamsaidia kuvaa shanga za shingoni na kiunoni.
" Kaa hapo tuchane nywele" anamsikia shngazi yake tylae akimwambia naye anaenda kukaa kwenye kiti kilichokuwa karibu hapo.
Wanamchana na kubana katikati ya kichwa na kuchukua shanga zingine na kumvalisha kichwani zilizozunguka kichwa na zingine zikining'inia pembeni.
" umependeza sana mwanangu" anasema nkeli na wengine kuitikia kwa vichwa.
" Sasa uvae viatu" anaongea sinde akiinama kumvalisha viatu vyake vya ngozi vya kufunga na kamba mpaka karibia na magoti baada ya kumaliza kufunga viatu anachukua vikuku na kumvalisha miguuni.
" tayari" anaongea sinde akisimama na kumwangalia tulya aliyependeza.
" hembu simama tukuone" anaongea tyale na tulya anasimama akitoa tabasamu na mara hiyo mlango unafunguliwa anaingia zunde.
" bado tu tuna..." maneno yanamuisha mdomoni baada ya kumuona Binti yake.
" umependeza mwanangu" anaongea akienda kumkumbatia.
" asante mama" tulya nae anamkumbatia machozi yakimtoka.
" sio mda wa kulia huu tuondokeni tunachekewa" anaongea nkeli na sinde kwamwangalia huyu nae mpenda kuharibu Hali ya hewa anajiwazia sinde.
" ndio wifi tunachlewa" anaongezea tyale.
" haya tuondokeni tusiwafanye watu watusubiri" anaongea zunde akimwachia Binti yake huku akimwangalia kuhakiki Yuko sawa na kumpatia tabasamu tulya nae analirudisha kwa kumhakikishia kuwa Kila kitu Kiko sawa.
zunde na wifi zake wanatangulia kutoka wakimwacha tulya na sinde nyuma
" umependeza sana sijaina bibi harusi mrembo kama wewe" sinde anazidi kumsifia ndugu yake na rafiki yake.
" asante" anatulia kidogo na kuendelea " "samahani sinde kuhusu Jana,sikutakiwa kumalizia hasira zangu kwako"
" usijali najua unavyojisikia,na hayo sio makosa yako ni ya huyo nzagamba kukufanya umsubirie" tulya Anacheka kumsikia sinde akimsema nzagamba na wakati huo wanasikia shangazi nkeli akiwaita.
" twende kabla hajabadili mawazo shangazi yako" anaongea sinde anayeonekana kutokupatana na shangazi yake tulya na wote wanacheka.
sinde anachukua kaniki na kumfunika Ili watu wasimuone na safari ya kuelekea kwenye mti mkubwa wa matambiko ilikokuwa inafungiwa ndoa kuanza.
Wanafika maeneo yale na kukuta watu wakiwa tayari wamefika akiwemo nzagamba na mama yake na ndugu zake wengine na wanakijiji waliokuja na matumbo ya njaa ya chakula na umbea wa kutotaka kusimuliwa harusi ya nzagamba wakiwa wamekuja na lengo la kujua ni msichana gani aliyejipiga mshale wa mguu.vigelegele na ndirimo vikiendelea kupigwa pamoja na nyimbo zikiimbwa.
Tulya aliyekuwa na uhakika ya kuwa macho yote yalikuwa kwake jasho jembamba lilikuwa likimtoka akiona viganja vya mikono yake vikiloa zaidi. shauku yake ilikuwa ni kumuona nzagamba kwani ni wiki tatu Sasa zimepita tangu waonane au amtie machoni pake.
Shangazi yake anasogea karibu yake kwa ajili ya kutoa kaniki iliyokuwa imefunikwa kichwani pake Hali iliyomfanya tulya atetemeke zaidi.lakini hakuweza kuzuia kitendo hicho kwani sekunde chache shangazi yake aliitoa kaniki hiyo kichwani pake,macho yake yakiwa bado yapo chini anasikia watu wakipiga vigelegele na waliokuwa wakiendelea kucheza wakicheza zaidi na kutimua vumbi.
Anajaribu na kunyanyua uso wake akiangaza kati ya watu kama atamuona anayemtafuta na macho yake yalipovuka upande wa pili yakitua kwa nzagamba ambaye hakuwa mbali na pale alipo na mapigo ya moyo wake yakipoteza mahesabu kwa sekunde.
Hali haikuwa kwa tulya tu hata kwa nzangamba ilikuwa vilevile alimwangalia tulya kwa kutokuamini kuwa ndio yeye msichana ambaye ameonana nae mara mbili tu na Leo ikiwa ni mara ya tatu lakini akimuona ni watofauti sana.
" mrembo sana"
" umekwisha nzagamba"