Chereads / penzi la bahati / Chapter 25 - chapter 24

Chapter 25 - chapter 24

" Acha kulia lia kama mtoto Sasa hivi umeolewa utakuwa mama sio mda" zunde anamwambia Tulya aliyekuwa amemkumbatia mama yake.Hii ni baada ya ndugu kukaa kikao na kujuana,na wazazi wake walikuwa wanaondoka Sasa." kwani Mimi sio mtoto wako tena?" anamuuliza mama yake angali kichwa chake bado amekifukia begani kwa mama yake." ni mtoto anayeweza kujitegemea,sisi tunaenda kuwa mwema kwa mumeo na mama mkwe wako sawa?"

Tulya anaitikia kwa kutikisa kichwa huku akijitoa kwenye kifua Cha mama yake " Tutakuja kuwatembelea mambo yakikaa sawa" Nzagamba ndie aliyeongea na kumfanya Tulya amwangalie kwa jicho la kumuuliza kweli " ndio unatakiwa uje upajue nyumbani" Mzee Kijoola anamkaribisha na kuongezea " Sasa wewe ni kijana wangu unakaribishwa nyumbani muda wowote ule"

" asante sana" Nzagamba anaitikia.

"Tuache sisi tuondoke tunachelewa" watu wote waliokuwa hapa wanaanza kuondoka na Tulya,Bibi Sumbo na Nzagamba wakiwasindikiza.

" unaenda lini kuchukua udongo mama?" Tulya anamuuliza Runde aliyekuja na kuanza kutembea karibu yake.

"vipi unataka uende?" Tulya anamjibu kwa kutikisa kichwa kukubaliana nae " hupumziki?"

"nipumzike nimechoka na nini? baada ya kukaa ndani muda wote huu pasipo kufanya chochote,sina hata hamu ya kukaa nyumbani tena,vilevile kukaa nyumbani panachosha"

" kweli,kukaa tu nako kama umezoea kuchakarika unaweza kuhisi unaumwa,ndani ya siku hizi ninaweza nikaenda,nikikamilisha siku nitamtuma sinde akuletee taarifa"

"itakuwa vizuri zaidi"

Wageni wote wanaondoka Tulya na Nzagamba wanarudi nyumbani kwao.

"unaondoka?" anauliza baada ya kumuona Nzagamba akibeba mitego yake.

" ndio,naenda mtoni"

" mbona bado mapema sana,ungesubiri hata upate chakula Cha mchana"

" sijazoea kushinda nyumbani,na kuhusu chakula usijali mchana huwa sina kawaida ya kula nyumbani,naondoka" baada ya kusema hivyo anatoka na kumwacha Tulya akimwangalia mgongo wake.

" unaenda wapi?" anamsikia Bibi Sumbo akimuuliza nje.

"mtoni"

" kwanini usikae na mkeo nyumbani Leo nyie bado ni wanandoa wapya"

" unajua mama sijazoea kushinda nyumbani,tutaonana badae" na hiyo ndo ikawa kwa heri yake.

Ndani Tulya anapita chumbani na kukaa kitandani, ngozi iliyotandikwa kitandani hapo ikitoa sauti,anavuta pumzi ndefu macho yake yakipepesa huku na kule mle chumbani na mwisho kutua kwenye furushi lililokuwa pale kitandani.

Anaangalia zile nguo alizovaa na kuamua kubadilisha kwani sketi aliyovaa ilikuwa ni nzito sana kutokana na shanga zilizoshonewa kwenye sketi.Anafungua furushi na kutafuta nguo nyingine ya kuvaa.Baada ya kubadilisha nguo na kupanga vitu chumbani kwake anajilaza kitandani macho yake yakiangalia dari la miti likifunikwa na majani " kweli nyumbani panachosha,ndio maana Nzagamba kakimbia" anajisemea akiendelea kujigeuza pale kitandani.

Mchana ulipofika Tulya anaamka na kwenda kuandaa chakula Cha mchana na mama mkwe wake chakula walichokula wao tu na baada ya kumaliza alirudi ndani kwake tena nakujilaza kitandani asijue usingizi umemchukua mda gani.anakuja kushtuliwa na sauti ya mtu akiimba anaamka na kuisikiliza na Moja kwa Moja anajua kuwa Bibi Sumbo ndiye aliyekuwa anaimba.

Ananyanyuka na kujitoa kitandani anaivuta miguu yake iliyoupeleka mwili wake mpaka nje na kumuona mama mkwe wake akianika ukindu kwenye kichanja kilichopo pale nje.

" unajua kushona ukili mama?" anamuuliza na kumfanya Bibi Sumbo ageuke na kumwangalia Kisha anaendelea na kazi yake.

" umeamka?" anamuuliza sura yake ikiwa na tabasamu ambalo Tulya hakuliona kwani alikuwa nyuma yake.

" ndio" anaitikia akienda pale alipo mama mkwe wake na kuanza kumsaidia kutandika ukindu aliyokuwa ametoka kuuchanganya katika rangi mbalimbali muda sio mrefu.

" ni mzuri na unapendeza sana,unashona mikeka?"

"na vikapu" anamjibu nakuendelea " itabidi nikushonee kapu Moja nimeona nguo zako zimefungwa katika furushi utakuwa unapata tabu ya funga fungua Kila mara unapotaka kubadili nguo"

"Nitashukuru sana" anaitikia mkono wake akiuleleka kukuna nywele za kichwa chake huku akitoa tabasamu la aibu ndogo na bibi sumbo analitambua hilo.

" Haina haja ya kuona aibu watu wengi wanafunga nguo zao kwenye mafurushi na sisi hapa ni familia,kachukue mkeka mwingine uko chumbani kwangu kauweke pale kwenye mti tukakae"

" sawa" anaitikia na kuondoka mara moja akimwacha Bibi Sumbo akimsindikiza kwa macho yaliyojaa furaha.

Baada ya kuweka mkeka chini ya mti wote wanakaa na bibi sumbo akiwa anashona ukili kwa ajili ya kutengeneza mkeka aliokuwa anauchanganya rangi mbalimbali,Tulya anamwangalia kwa mshangao na shauku jinsi mikono yake ulivyokuwa myepesi katika kushona ikionyesha ni jinsi gani alivyomzoefu katika kazi hii.

" umeanza kushona tangu lini?" anamuuliza

" tangu niko binti mdogo" ndio maana anamkono mwepesi anawaza Tulya lakini subiri amejifunza kwa nani anavyokumbuka alisema bibi yake alikuwa ni mfinyanzi au mama yake,bila kujizui anamuuliza." nani alikufundusha kushona au ni mama yako?"

" Mama yangu alikuwa anajua kupika tu" anaongea Bibi Sumbo akicheka kidogo macho yake yakiwa kwenye ukili na kuendelea " nilikuwa na rafiki yangu mama yake alikuwa ni fundi mzuri wa kushona ukili nilikuwa naenda nyumbani kwao na mama yake anatufundisha" Tulya anakubaliana nae kwa kichwa na inavyoonekana rafiki yake alikufa kwani anazungumza kwa mda mrefu uliopita na kwa mtu ambaye hakuwepo.

" na uzee huu nimemkumbuka sana,alikuwa ni mtu pekee wa karibu niliyezoeana nae wa kufichiana Siri" anaongea akivuta pumzi ndefu.

Bibi Sumbo hana marafiki wengi wakuongea nae Mambo mengi sio kama amejitenga au ametengwa kama mwanae Nzagamba isipokuwa yeye ni mtu wa kushinda nyumbani kwake tu na watu wengine aliozoeana nao nizaidi ya kusalimiana kwa mda mfupi na Kila mtu anaendelea na Mambo yake na watu wengi wanamheshumu sana kutokana na busara zake nyingi na ukarimu wake sema wakati mwingine upweke unamzidi kwani Hana mtu wa kuzungumzia nae Mambo mengi hivyo kwa wakati mwingi humkumbuka sana rafiki yake.

" watoto wake si wapo ukiwatembelea,utapata faraja kidogo" Tulya anaongea na kumfanya bibi sumbo atoe tabasamu ambalo halikufika machoni pake " hilo ndio tatizo,alikufa mdogo sana rafiki yangu hata hakuolewa sembuse mtoto"

" pole sana" Tulya anampa pole akiwaza kuwa huyu rafiki atakuwa alikuwa ni mtu wa karibu sana mpaka Bibi Sumbo bado anamkumbuka sana.

" miaka imetembea lakini Kila nikifikiria naona kama ni jana tu tulikuwa tunacheza na kukusanya Kuni na kujifunza kushona ukili pamoja"

Ndio maana anashona ukili kwani unamfanya ajisikie kama Yuko na rafiki yake anawaza Tulya " msamehe bibi kizee huyu,anakuongelesha habari za kizee " anaongea akicheka kidogo.

" hapana Haina shida,ni vizuri ukiwa na mtu wa kukusikiliza, unaweza kuongea na mimi chochote kile" anaongea huku mikono yake ikikusanya masalia ya ukindu aliyotupa Bibi Sumbo.

" hivyo vyema,nikajua utamchoka mama mkwe wako sio mda"

" umesema alikufa mdogo kabla hajaolewa aliunwa au" Tulya anamrudusha bibi sumbo kwenye maada ya rafiki yake naye anaitikia kwa kichwa akiashiria kukataa na mikono yake iliyokuwa inachakata ukindu ikisimama.

" alishambuliwa na Simba" Tulya anamwangalia kwa mshtuko kwani katika taarifa zote za vifo hakuitegemea hii.

" miaka iliyopita kulikuwa na wanyama wengi sana tofauti na Sasa ila huwezi kulinganisha na kipindi Cha mababu zetu" anatulia kidogo kama anarudi katika miaka hiyo iliyopita.

" wanyama walikuwa wakizunguka kwenye makazi ya watu kama ndio nyumbani kwao,tofauti na Sasa usiku unakutana na fisi tu na mchana unakutana na nyani na ngedere tu"

" nawaogopa fisi" anaongea Tulya na kumfanya Bibi Sumbo acheke " ungezaliwa miaka ile usingetoka nje"

" Sasa ilikuwaje mpaka rafiki yako akashambuliwa na Simba?"

" alikuwa tu nyumbani,inavyoonekana Simba naye alipotea njia matembezini, watu wakaanza kumkimbiza na akaishia karibu na nyumbani kwao yeye alikuwa ndani akasikia makelele kutoka nje hakujua kama Simba alikuwa ndani ya boma lao akamrarua kupiga makelele mpaka watu walipofika alikuwa amejeruhiwa vibaya sana na akafariki Dunia kutokana na kuvuja damu nyingi"

kumbe hata nyumbani hapakuwa salama anawaza Tulya baada ya kuisikiliza hadithi ya bibi sumbo kuhusu rafiki yake kwani anauhakika angezaliwa kipindi hicho angekuwa hatoki ndani kabisa kwa kuogopa kuwa kitoweo Cha wanyama wakali.

" pole,itakuwa ilikuwa ni mshtuko mkubwa sana kwa watu wote"

" mmh, sio kama ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mtu kushambuliwa na wanyama lakini inauma sana akiwa ni ndugu yako au mtu wako wa karibu"

" najua,ni vizuri tu wanyama wamepungua"

"hapana sio vizuri,tena ni vibaya sana" anaongea bibi sumbo akikazia maneno yake na kumfanya Tulya amwangalie kwa mshangao.