Chereads / penzi la bahati / Chapter 29 - chapter 28

Chapter 29 - chapter 28

" Yule mwanamke anamatatizo gani na Mimi?" anauliza Tulya akiwaangalia Lindiwe na marafiki zake wakiondoka mwili ukichemka hasira.Asijue Lindiwe anamatatizo gani kwani kila akikutana naye mambo hayaishii kwa amani.

" Mvumilie tu maisha yake yanasikitisha " Sinde anaongea akimshika bega " kwa hiyo kama yanasikitisha kwangu ndio sehemu ya kupunguzia mawazo,mwanzoni nilijua ni kwa sababu ya mumewe labda anajikinga nisiolewe nae na nikampatia alichokitaka Sasa anazidi kunichokonoa tu,na wake wanawake wawili wako kama manyumbu.

Sinde anacheka " kinachokuchekesha nini?" anamuuliza akimkazia jicho lakini Sinde anazidi kucheka.

" pumua Tulya,nasikia Manumbu anampiga karibia kila siku ndio maana uso wake umevimba kama kang'atwa na nyuki au nyigu"

" namwonea huruma sana" anaongea akijitahidi kutokumchukia zaidi Lindiwe kwani ana yake yaliyojaa kwenye kikapu na Tulya sio mtu wa kuufurahia majanga ya watu.

" chota maji tuondoke" anamwambia Sinde naye anaingia mtoni na kibuyu.

Nzagamba akiwa na shoka na panga lake anaingia katikati ya pori,anatembea huku na kule akiangalia miti mizuri kwa ajili ya ujenzi wake.anafika mahali nakuona miti mizuri iliyonyooka nakuona itamfaa.Anatua panga lake chini na kubaki na shoka mkoni nakuanza kukata miti .

Wakati anaendelea na kazi yake anahisi Kuna mtu anamwangalia lakini kila akigeuka haoni chochote,atakuwa anawaza vibaya au lakini siyo hivyo hata kama Nzagamba siyo muwindaji tena anajulikana kwa kuwa na hisia kali na kama anahisi Kuna mtu anamwangalia basi ni kweli na sio kaanza kumwangalia Sasa hivi anajua mtu huyo amekuwa akimfuatilia tangu ametoka nyumbani kwake lakini tatizo linakuja kila akigeuka haoni chochote

Kuamua kupuuzia jambo la mtu kumwangalia anaamua kuendelea na kazi yake iliyomleta hapa porini,na kama mtu huyo angekuwa anataka kumdhuru basi angejitokeza na kama kaamua kumfanyia mazingaombwe basi atakuwa hana cha kufanya itakuwaje kama akija kumsaidia kukata miti hapa anajiwazia Nzagamba.

Baada ya muda anasikia watu wakiongea wakija mahali alipo kabla watu hao hawajafika anawaona mbwa wawili waliokuja kusimama alipo na anawajua mbwa hawa."bwana harusi kulikoni porini mapema hii" anauliza mwanaume mmoja " atakuwa anataka kuongezea nyumba kwani sio mda atapata watoto anataka kukuza ukoo haraka" anaongezea mwingine.

" mnafanya nini hapa na pinde zenu migongoni?" anaongea Nzagamba akiacha kukata miti na kuwaangalia marafiki zake wawili waliosimama pale.

"kuwinda,kwani huoni?" anaongea Mkita akionyesha sungura mkononi aliyemuwinda

" sio mwindaji lakini najua eneo hili huwezi kupata chochote ilihali niko hapa,na hata nisingekuwepo sidhani kama mngepata kitu" anaongea akimwangalia Lingo aliyekuwa hana chochote kabisa. " wanyama siku hizi ni shida sana" anaongea Lingo akitema mate ya ugoro aliokuwa anatafuna.

" hapa tumetembea tangu alfajiri na ndio tumepata hiki" anaongea Mkita akimuonyesha sungura wake asiyetosha hata kwa kitoweo cha mchana tu.

" kwa nini msizunguke milima ya nkyala?" Nzagamba anawashauri

" ungekuwa wewe ungeenda?huko ni mbali sana na ni hatari mkienda wachache, mnatakiwa muende kikundi.Mpaka rombo ipigwe sio leo" mkita anazungumza akitafuta kivuli cha mti na kukaa akimweka sungura wake pembeni kama ndio thamani ya leo " na nasikia kuna mizimu huko inazuia kuwinda" anaongezea mwili ukimsisimka kwa kuwaza tu kuonana na mizimu.

" Hali inazidi kuwa mbaya kila kukichwa" anaongezea Lingo akienda kukaa alipokaa Mkita "Mimi nachoka hata sijui nitalisha nini familia leo" anaongea Mkita akimkazia macho Nzagamba aliyekuwa anawaangalia pale walipo.

" na wewe unakata miti ya nini?" anauliza Lingo " naenda kutengeneza uwaa" anawajibu akiangalia ile miti aliyokwisha kukata " uwaa wa nini wakati hauna hata mbwa" anaongezea Lingo na mkita kudakia " kama unataka mbwa njoo uchukue kwangu mbwa wangu alizaa mwezi uliopita na watoto wake ni visu hatari,nitakugawia wawili mmoja atapozewa"

" sio kwa ajili ya mbwa,namtengenezea Tulya sehemu ya kufanyia kazi yake" anawajibu akipuzia mgao wa mbwa.

" kazi gani?" Lingo anauliza " anafinyanga vyungu" Mkita ndie aliyemjibu "mkeo ni mchakarikaji" Lingo anaongea.

" Nzagamba kwa nini tusiende kuwinda wote huko mtoni mimi sina cha kulisha familia leo" Mkita anaongea akiwa na mawazo yakulaza familia yake njaa." niliwinda jana kwa hiyo bado nina akiba ya siku mbili mbele mpaka nitakapomaliza kazi yangu ya kujenga uwaa" anawajibu

" acha hizo Nzagamba kwa nini usifanye hivi kwa marafiki zako wa kufa na kuzikana,kuzikana kwenyewe ndio huku" anabembeleza Mkita akisimama na kumfuata pale aliposimama Nzagamba." kweli tena tusaidie" anaongezea Lingo aliyeafikiana na wazo la Mkita." hamuoni nina kazi mimi?" anawaambia akiwaonyesha miti.

" usijali kuhusu hilo tunalishughulikia haraka tunaondoka" anaongea Lingo akisimama.

" kama mnasema hivyo mimi sina tatizo,na mfanye haraka kabla jua halijawa kali si mnajua" anawaambia, Mkita anachukua panga aliloacha Nzagamba pale chini na Lingo kutoa sime yake anayotembea nayo kiunoni pake yenye ukubwa sawa na panga nakuanza kusaidia.

" ndio maana nilikuwa nashangaa kukosa wanyanyama kumbe wewe uko hapa" wanamsikia mtu akiongea na wote wanageuka kuangalia nani anaongea na macho yao kukutana na Manumbu akiwa na rafiki yake Nsio.

" Bora uondoke tu,siko kwenye hali ya ugomvi leo" anaongea Mkita ambaye kweli hakuwa kwenye hali nzuri leo njaa ya familia yake ilikuwa inamtesa akili na mwili.

" naona wengi tunalala njaa leo" Lingo anaongea akicheka baada ya kuwaona Manumbu na Nsio na silaha zao mikono ikiwa patupu.

" unacheka nini? wakati eneo lote halina wanyama kwa sababu ya huyo" anabwata Manumbu akimnyoshea kidole Nzagamba.

" umekosa wanyama kwa sababu umekuja kuwindia miguuni pangu hapa" Nzagamba anamjibu uso ukiwa kawaida pasipo kuonyesha hisia zozote zile licha ya Manumbu kumpa maneno makali " kwa nini usizunguke milima nkyala huko unaweza kubahatika" Anatoa ushauri Nzagamba.

" aende huko anaubavu huo" anatania Mkita na Lingo kucheka tena kuona siku yake sio mbaya kivile.

" Tutajuaje pengine laana yako inaenea kote unakopita,ndio maana kila kitu kinakimbia"

" vinakimbia vingine lakini wewe bado upo hapa,fanya uondoke kabla haijakufikia,kama ulivyosema pengine laana yangu bado inatembea itakuwa vibaya kama ikikufikia wewe na ukapoteza sifa yako,maisha yako yatakuwa mabaya zaidi kwani sifa yenyewe unayo hiyo tu"Nzagamba anamtwisha mzigo wa maneno Manumbu sauti yake ikiwa vilevile pasipo mkwaruzo.

" kumbe unajijua kama wewe ni kama ugonjwa wa mlipuko" anazidi kudhihaki Manumbu akijua itamkera Nzagamba lakini hasira inampanda zaidi anapomwona yuko tulivu vilevile." unajua ukijijua vitu vingi havikusumbui" anamjibu huku akitoa tabasamu." Angalia usije ukamwambukiza na mkeo" Manumbu anaamua kumwingiza na Tulya apate kumkera Nzagamba na ilifanya kazi kidogo kwani mkono wa Nzagamba ulioshika shoka unalikamata kwa nguvu kama anaenda kuangusha mbuyu lakini hakulionyesha hilo usoni.Nsio akiwa amesimama na mkono wake kiunoni na mwingine ukishikilia fimbo yake ndefu anaangalia tu jinsi rafiki yake anavyotaka kujikomba hawezi hata kushauri kwani anamjua rafiki yake vizuri mdudu akipanda kichwani.

" Inavyoonekana bado hujamsahau tu mke wangu Manumbu,usijali kuhusu yeye kwani ugonjwa huo ulimpata siku tu alipoamua kuolewa na mimi,nakuhakikishia kuwa umeenea mbali kiasi kwamba hawezi kupona na kingine usimuingize kwenye masihara yako siku nyingine akikusikia yeye sijui mtamalizia wapi nadhani unamjua vizuri" Nzagamba naye anajibu kwa dhihaka ileile.

" Inavyoonekana Manumbu hajui kuwa mwanaume rijali haangalii cha mwenzake hutunza chake" Mkita anaamua kuingilia na Manumbu kumwangalia kwa hasira na Mkita kuangalia juu kama mtu aliyekuwa anaongea nae alikuwa juu ya mti.

Kama mbili au nne ilikuwa haitoshi inaongezaka na kuwa sita "Kuna nini hapa?" anauliza Kilinge aliyefika akiwa na ndugu yake Zinge wakiwa na mishale na pinde na mbwa wao.inavyoonekana hapa ndio Kambi ya mawindo leo anawaza Nzagamba "Tulikuwa tunamsikiliza Manumbu anavyoelezea ni jinsi gani hajamsahau Tulya" Lingo anajibu swali la Kilinge uso ukiwa na tabasamamu la kuwa mshindi wa mwaka.itakuwa nimepitwa na uhondo anawaza Zinge macho yake yakipita kwa Kila mtu aliyeko pale kama mtoto aliyetumwa kibarua cha kuhesabu wageni walioko sebuleni ili mama apate idadi ya kugawa nyama jikoni " Manumbu hujamsahau tu binamu yangu,lakini haiwezi kuwa rahisi namna hii,ukizingatia jinsi alivyo mrembo" Kilinge nae anaunga tera kumtania Manumbu ataachaje nafasi nzuri kama hii inayokuja mara moja moja.

"Nani kasema anamfuata mke wake,au mnashindwa kumuuliza shemeji yenu ambaye hajamsahau mke wangu" Manumbu anajibu mashambulizi na macho yote kwenda kwa Nzagamba kwa sababu ukweli uliopo hapa ni kwamba wote wako kwenye mapenzi na mke wa mwenzake isipokuwa Nzagamba ambaye hajui kuwa hisia zake zimeanza kubadilika.

" umeniona lini mimi nikiwa nyuma ya sketi ya mkeo" anajibu Nzagamba asipende mazungumzo yanakoelekea.

" tutajuaje pengine hufanya kwa siri,na ulivyo mzuri kwenye kipengele hicho" anajibu Manumbu akiona amempatia lakini Kila mtu aliyeko hapa anajua ukweli kuwa Nzagamba alikata mawasiliano na Lindiwe pindi tu alipovunja uchumba licha ya hisia zaku kubaki moyoni mwake lakini hiyo ilikuwa ni siri yake na Manumbu analijua hilo sema anathibitisha usemi unaosema asiye na silaha wakati wa vuta anakuua hata kwa mate.

" kwa hiyo unatuthibitishia kuwa mkeo anakusaliti na Nzagamba au" anahoji Kilinge

" aaaah! ndio maana nilikutana nae yupo kama nyuki wamefanya uso wake mzinga wa kutengeneza asali kasoro sikuona asali tu au wamehama na kubeba kila kilicho chao " anatania Mkita na wengine kucheka akiwemo Zinge na Manumbu kumwangalia kwa hasira." hizo dalili mbaya Manumbu,zinakuonyesha dhahiri hujiwezi kitandani" Lingo anatia chumvi kwenye kidonda na Manumbu kutoka mbio pale alipo akielekea kwenda kumvaa Lingo lakini Nsio na Zinge wanamzuia.

" Huo mwisho wa salamu jamani sisi tunaenda" Nsio anaongea akimvuta Manumbu waondoke " niachie,niachie" anajitupa Manumbu akitaka aachiwe lakini Nsio anamvuta kwa nguvu mpaka anafanikiwa kumtoa." hao mbwa wako bado wako kwenye mgao" Anaongea Nzagamba macho yake yakiwa bado yapo kule alikoelekea Manumbu akiwaza kupigana na mtu kama yule ni hasara tu siku nyingine anawaacha mbwa wamshughulikie endapo akiwa nao na wazo la kuwafuga linamjia.

" ndio,ni wewe tu" anajibu Mkita akitabasamu kama anaelewa kinachoendekea kichwani kwa Nzagamba.

" nakuja kuwachukua jioni" anatangaza maamuzi yake.