Chereads / penzi la bahati / Chapter 16 - chapter 15

Chapter 16 - chapter 15

Bibi sumbo anarudi nyumbani na kumkuta nzagamba akitengeneza kamba za katani uani akiwa amempa mgongo " una mpango wa kunidhalilisha mama yako si ndio" nzagamba anaendelea na kazi yake pasipo kumjibu mama yake.

" ulienda wapi asubuhi hii na ulikuwa unajua tunaenda wapi"

" sitaki kuoa,tena sio huyo msichana mama mara ngapi nikwambie achana na mawazo hayo" anaongea macho yake yakiwa kwenye jembe akitengeneza nyuzi kutoka kwenye katani Ili badae aje ashone kamba.

"kwa nini mwanangu,Binti ni mzuri wa tabia na ni mrembo pia wewe unachotaka ni nini, kama mizimu imeamua kukupa nafasi wewe ni kama nani mpaka uitupe" bibi sumbo anajua mwanae alikotoka baada ya lindiwe kuvunja uchumba ilimuuma zaidi hategemei mwanae kubadili mawazo kirahisi lakini anajua kuwa endapo akioa mkewe atakaye kuwa upande wake atabadilika,na hakuna mwanamke mwingine anayeweza kufanya kazi hiyo zaidi ya tulya.

" nilidhani Jana ulinielewa tukakubaliana imekuwaje leo upotee asubuhi na kumfanya mama yako aongee uongo kukutetea" bibi sumbo alipoamka asubuhi hakumuona nzagamba hivyo na kuamua kwenda mwenyewe kumuona tulya na kuongea uongo kumtetea kwa sababu wangejua kama hataki kuoa wangebadili mawazo na bibi sumbo hakutaka hilo litokee.

" hatukukubaliana chochote mama, wewe ulinipa taarifa tu,na Mimi ndio nakwambia sitaki kuoa kubaliane na hilo, mapema utakavyokubali ndivyo Mambo yatakavyoisha" anaongea na kusimama kumwangalia mama yake.

" umefanyeje hapo mdomoni" anauliza bibi sumbo baada ya kumuona akiwa ameivilia pembeni ya mdomo kutokana na ngumi aliyopigwa Jana na manumbu.

" Amna kitu chochote,kwa hiyo mama huo uchumba utauvunja" anapapasa mdomo Wake alipoumia.

" nini? ni vunje uchumba?" anashangaa bibi sumbo hasira ikimjaa kutokana na kijana wake asiyejali tena "unatafuta kumharibia heshima Binti wa watu au, huo uchumba hauvunjiki kama ulikuwa hautaki usingepotea Leo asubuhi tungeenda wote na ukakata Mbele Yao kilichokufanya usiende nini na kitu kingine wewe Sasa ni mchumba wa tulya utake usitake utaoa na usije ukafanya kitu Cha kipumbavu nakuapia hutaniona tena" anaonya bibi sumbo na kuingia ndani.

Nzagamba anatupa katani na nyuzi zake alizotengeneza pale chini na kusambaratika

" haya yote makosa ya yule mwanamke chizi,nisimtie machoni kabisa" nzagamba anazidi kumchukia tulya kwa kumtumia yeye katika mchezo wake na kumfanya yeye kuwa kivutio zaidi Kijijini na anaahidi kumshikisha adabu.

Tulya Leo ameshinda ndani akimwangalia runde akifinyanga vyungu na yeye akichukua udongo na kujaribisha lakini mikono yake ni mizito mno na udongo ukimteleza mara kwa mara " usijali sana mwanzo huwa ni mgumu hivyo hivyo tena naona unafanya vizuri,pumzika tutaendelea kesho"

" hapana shangazi tuendelee hata sijachoka" anakataa tulya akiwa na shauku ya kujua Kila kitu Leo.

" Mimi ndio nimechoka,humuonei huruma mama yako nimezeeka ujue,na tunatakiwa kuandaa chakula Cha jioni" runde anasimama na kunawa mikono yake tulya nae akienda kunawa " porini tunaenda lini" anauliza akinawa.

" mbona una haraka hivyo" runde anamshangaa

" si unajua sina mda mrefu nikikaa ndani hamtaniruhusu nifanye chochote hasa mama akija"

"upo sahihi,tutaenda kesho lakini usiwe na pupa kiasi hicho kuwa mfinyanzi mzuri kunahitaji uvumilivu pia Ili vyungu vyako visipasuke,unatakiwa ufinyange kutoka moyoni kwanza ndipo ufikie kwenye mikono iliyoshika udongo ukiliipua lipua tu hutaweza kupatana na udongo kwani hata udongo huchagua mtu wa kuunga nao urafiki,kwa hiyo chukua muda unaotaka kwani hata ukiolewa utakuwa unakuja na kujifunza taratibu,ujaribu kupumzika mapema kesho tutaenda porini.

Tulya anaelewa mafundisho ya runde kuwa ukihitaji kitu usiwe na haraka na kwa sababu uvumilivu ni jadi yake.hilo Halina shida atahakikisha yeye na udongo wamekuwa ni marafiki wasiotengana maisha Yao yote na kwa kutumia ufundi wake atailisha familia yake.

Siku tatu zimepita tangu aanze kujifunza kufinyanga na runde kumpongeza kuwa anapiga hatua nzuri.

" kwa nini usingepumzika tu ningeenda mtoni mwenyewe" anaongea sinde akimwangalia tulya aliyekuwa akikanda Kanda vidole vyake vilivyokuwa vikiuma kutokana na kushika udongo mda mwingi mikono yake ilikuwa ikiimuuma pia kwani ilikuwa haijazoea hasa kutengeneza udongo mkubwa.

" usijali nipo sawa nataka nipate upepo kidogo kukaa ndani panachosha hapa nimekaa siku mbili tu naona kama mwaka hapo bado hawajanifungia kabisa Bora nitumie nafasi hii kidogo"

" kweli ndani panachosha Mimi sitaki hata kukumbuka kipindi Cha mafunzo ya mwali siku za mwanzo nilikuwa nalia"

" hata Mimi,lakini hiyo afadhali kuliko hii ya kukaa peke yako nawapa hongera waliotoka tu mwali wakaolewa hawakukutana na hii adha"

Wanafika sinde anaanza kuchota maji tulya anasimama akiangalia huku na kule akijiuliza kwa nini hasikii kalimba ya nzagamba.

" nipokee kibuyu unawaza nini" sinde anamshitua aliyekuwa akimpa kibuyu akipokee na yeye alikuwa hamsikiii,anakipokea na kumpa kingine achote.

"unayemtafuta hayupo Leo" sinde anamwambia akitoka mtoni na kusimama ukingoni.

" namtafuta nani" anauliza akiona aibu sinde kumkamata

" najua kilichokufanya uje mtoni,atakuwa anajiandaa na harusi itakuwa ni vigumu kuonana nae"

wanajitwisha na kuondoka tulya akiwaza kwa nini nzagamba hajaja kumuona hata mara Moja na wakati hamjui inamaana Hana shida ya kumuona mwanamke anayemuoa,vijana wengine wako radhi kukimbia hata kambini Kuja kuwaona wachumba zao wakiwakumbuka,kama Tinde alivyofanya.kwa nini yeye hajaja kumuona roho yake inakuwa nzito na anahisi kuumizwa lakini anajipa moyo na kujua ni bado mapema kwani harusi ni ya kushtukiza sio kama wamechumbiana mda mrefu.

" usiwe na wasi wasi atakuja tu kukuona"

" mmh!" anaitikia wakiendelea kutembea

" sinde"

sauti ya kiume inamwita sinde wote wanageuka na kumuona nzagamba akitokea vichakani akiwafuata " uliyekuwa unamuwaza huyo amekuja"

mapigo ya moyo wa tulya yanapoteza mahesabu asijue afanye nini na kuanza kujialaumu kwa nini hakujipendezesha.

" nzagamba" anaita sinde baada ya nzagamba kuwafikia tulya ananyamaza kimya macho yake yakimshangaa nzagamba kwani kwa karibu ni mzuri zaidi kuliko alivyomwona siku ile ya sherehe ya matambiko nywele zake ndefu za kusokota kichwani zikimpendeza na mkono wake kumuwasha ukitaka kuzishika .

" habari yako sinde" anamsalimia sinde tulya akibaki hoi kwani hata sauti yake ilikuwa nzuri na tulivu kama maji ya mto usiotembea.

"nzuri tu za kwako"

" nzuri" na macho yake yakigeukia kwa tulya "nadhani wewe ndio tulya"

" eheee!ndio" tulya anaitikia sauti yake ikimgomea kutoka na kumfanya sinde acheke tulya anamfinya kwa chini asimcheke huku akiangalia chini kwa aibu akiilaumu sauti yake kukimbia wakati kama huu na kumuaibisha huu kama sio usaliti nini.

" unaweza kutuacha kidogo sinde" anaongea macho yake yakiwa bado yametua kwa tulya,tulya nae ananyanyua uso wake na macho yao yanakutana.

'hiki nini' anawaza tulya baada ya kuona macho ya nzagamba yaliyokuwa yakimwangalia sio kama anataka kumjua au mtu aliyetaka kumjua na hakuweza kugundua Yana maanisha nini kwani siku ya tambiko licha ya kumuona kwa mbali macho yake yalikuwa angavu yenye ujasiri licha ya matatizo aliyokuwa nayo,lakini Leo yanaonekana tofauti kwa nini.

" tulya mimi natangulia "

"sawa"

sinde anaondoka tulya anakaa kwa muda na kuona nzagamba haongei anataka kutua kibuyu chake lakini nzagamba anamkataza.

" Haina haja usitue kibuyu chako sitachukua mda mrefu"

tulya anamwangalia kwa kujihami kwani hata sauti yake imebadilika tofauti na alivyokuwa anaongea na sinde.

" nitaenda Moja kwa Moja kwenye lengo,huo mchezo uliouanzisha nataka uumalize wewe mwenyewe sina muda wakucheza mchezo huo na hata kama ningekuwa nao nisingecheza na wewe" anaongea na tulya kubaki akimtazama asijue anamaanisha nini.

" sikuelewi"

" hunielewi vipi,kwa matendo yako na unavyooneka unakili au nimekosea" anaongea lakini anaona tulya bado anamwangalia kwa kutokuelewa.

" nataka uuvunje uchumba huu wewe mwenyewe"

moyo, mwili,akili na Kila kitu Cha tulya kinatetemeka haamini anachokisikia, sasa anajua kwa nini anamwangalia namna ile ' ananichukia,hanitaki' anawaza tulya na midomo yake inataka kusema kitu lakini anashangaa inatetemeka tu hakuna neno linalotoka.

" unasikia, Mimi sihitaji huruma zako,haya ni maisha yangu na Mimi nimeshakubaliana nayo na Nina uhakika mama yangu angekubaliana nayo sio muda mrefu,wewe nani uje kuyavuruga na kunifanya kuwa zaidi ya kituko,Ninachokitaka uvunje huu uchumba mwenyewe kabla Mambo hayajawa magumu zaidi kwanza hii itakusaidia wewe pia,na hii itakuwa mara yangu ya mwisho kukuona sitaki kuonana na wewe tena, na usiumize kichwa kuhusu sababu ya kuvunja uchumba sababu inajulikana Kijiji kizima Mimi nitachukua lawama na hiyo itakusaidia wewe kuolewa tena,nadhani umenielewa" anamaliza na kuanza kuondoka akimwacha tulya akiuangalia mgongo wake,anajikaza asianguke chini kwani akimtoa mama yake runde hasara ya kibuyu kingine lazima atabeba mtungi.

Anasimama na kumwangalia nzagamba mpaka anapotea na yeye kukusanya nguvu na kuelekea nyumbani akijikaza asilie .

Anafika nyumbani anamkuta sinde akimsubiri nje kwa shauku ya kupata habari lakini baada ya kuona sura ya tulya anajua Kuna jambo.

" vipi imekuwaje mbona uko hivyo" anaongea sinde akienda kumsaidia kutua kibuyu baada ya kuona mikono ya tulya ikiteteneka.Tulya anaweka kibuyu na kukimbia kuelekea nyumba ndogo wanayoitumia yeye na sinde.anaingia ndani nguvu zote alizozikusanya Kuja ndani zikamuisha na kukaa chini machozi yakimbubujika sinde aliyekuwa anamfuata nyuma anafika na kufunga mlango.

" tulya mbona unalia Kuna nini,kasemaje nzagamba" anaenda kukaa pale alipo akimbembeleza tulya anazidi kulia

" sema basi unanitisha ujue,ongea nikusaidie"

" hanitaki sinde" anaongea kwa sauti ya kigugumuzi iliyojaa maumivu.

" nini?,hakutaki?" anauliza sinde kama hajamsikia

" hanitaki,kasema nivunje uchumba mwenyewe,hataki hata kuniona"

" usilie nyamaza,atakuwa kapata tu mshtuko sababu Mambo yamekuwa ghafla ndio maana, Nina uhakika atabadili mawazo" sinde anamfariji akimshika bega.

" hapana ananichukia sinde,ananichukia Mimi" anazidi kulia akishika kifua chake

" usiseme hivyo atakuchukiaje wakati ndio kwanza mmeonana Leo na hujamkosea chochote na alitakiwa kuwa na shukrani mwanamke kama wewe umekubali kuolewa nae"

" wewe hujamuona sinde,macho yake yote yanaonyesha chuki juu yangu,ananiangalia utadhani nimemnyang'anya tonge mdomoni yaani siwezi kuelezea aaa kama Mimi ndio chanzo Cha matatizo yake yote,nitafanyaje Mimi sinde"

Anazidi kulia tulya hakujua mtu akikuchukia unajisikiaje Sasa ameona na mtu anayemchukia ni mume wake mtarajiwa atakayeeenda kuishi naye nyumba Moja kitanda kimoja asijue atafanyaje roho yake inamuuma na kuona nzagamba kachukua sime na kuuchoma moyo wake hivyo haitoshi na kuanza kukizungusha, asijue afanye nini kuyakabili maumivu hayo asione dawa.

" shhshhh,nyamaza Kila kitu kitakuwa sawa shhhh" sinde anamnyamazisha akimlaza kifuani kwake tulya aliyekuwa analia kwa uchungu usioelezeka.