Chereads / penzi la bahati / Chapter 15 - chapter 14

Chapter 15 - chapter 14

nzagamba anaanza kukohoa kwa nguvu huku akipenga pua yake kutoa pombe iliyoingua puani"uko sawa" mkita anamuuliza akimpigapiga mgongoni " nani huyo" anauliza mkita na kugeuka, uso kwa uso anakutana na manumbu aliyekuwa amelewa " manumbu!" anauliza kwa mshtuko.

" nani Leo amekuja,aaa ni nzagamba mwenyewe mtu maarufu" anaongea manumbu kwa sauti ya kilevi.

"unafanya nini,ungemuua mwenzio je?" anauliza mkita hasira zikimchemka

Nzagamba anayeendelea kukohoa chini anajikongoja na kusimama akisaidiwa na vijana "shida yako nini manumbu" nzagamba anamuuliza kwa sauti yake ya kukwaruza akiendelea kukohoa.

" unauliza shida yangu ninj?" manumbu anaongea akiendelea kupepesuka kama anashindana na upepo " shida yangu ni wewe,wewe nzagamba"

" kama umelewa si uende nyumbani huko kwa nini ulete fujo hapa" anang'aka mkita kwa ghadhabu lakini nzagamba anamshika mkono kumzuia asilete fujo zaidi.

"haya sema nimekukosea nini" anaongea nzagamba sauti yake ikianza kuwa sawa na kikohozu kikipungua.

"khaaa! hicho ndio kinachonikera zaidi muda wote kujifanya unabusara,naona utakuwa na furaha sana sababu unaenda kuoa mpaka nzagamba wewe mwenye kuwinda ndege na panzi Leo umeamua Kuja kwenye ukara kuongea"

Vijana wote walikuwa wanajua kilichotokea kwani taarifa zilikuwa zimeenea Kijiji kizima na wanajua kwa nini manumbu Yuko hivo,kwake yeye anayependa kupata Kila kitu na wanawake wengi wakijipendekeza kwake alijua tulya nae atakuwa Moja kati ya wale wanawake ukilinganisha matukio ya kukutana kwao alijua ni lazima atakubali tu kuolewa nae hivyo alipeleka posa pasipo hata kujua msimamo wake na Moshi wote kuishia kwake baada ya tulya kuikataa posa na kinachomuuma zaidi ni posa yake kukataliwa na kuchaguliwa nzagamba.

"hata uoe uanze Kuja kwenye ukara na mawaidha utabaki kuwa yule yule nzagamba usiye na bahati huwezi kubadili hilo na huwezi kujichanganya na sisi" manumbu anaendelea kumnanga mwenzake.

"Sasa kama unajua maisha yangu tayari hauwezi kulinganishwa hata kidogo na yako kwanini usiniache nilivyo kwani lazima unikumbushe Kila ukiniona" nzagamba anamjibu na kuendelea " na usijali kuhusu hilo Mimi nimeridhika na Hali yangu na Kila mtu anajua Haina haja ya kunikumbusha, vipi kuhusu wewe kinakusumbua nini tusichokijua kwa ninavyoona maisha yako Yana shida zaidi mpaka pombe haunywi kwa raha Bali kwa kutaka kupunguza masaibu yako"

kusikia maneno ya nzagamba, manumbu mwenye hasira za karibu anashindwa kujizuia akijuwa wazi kuwa nzagamba alikuwa anamtukana makusudi asionyeshe dhamira yake wazi.

"unasemaje?" manumbu anampiga ngumu ya shavu nzagamba ambayo haikumtikisa sana kutokana na mpigaji aliyelewa.Nzagamba nauzungusha ulimi wake mdomoni na anakakutana na Radha chachu kidogo anayakusanya mate na kutema pembeni.

" unafanya nini wewe" mkita aliyetoka kwa ghadhabu na kutaka kwenda kumvaa manumbu anazuiliwa na nzagamba " mtu asiingilie" anatoa amri nzagamba na vijana wote kutulia.

" inavyoonekana Kuna kitu umekisahau manumbu" anaongea huku akimsogelea na kusimama karibu kabisa na manumbu aliyekuwa akinesa, nzagamba aliyemzidi manumbu urefu kidogo kama inchi nne ilimbidi manumbu kunyanyua uso wake kidogo kumtazama machoni.

" wewe kuwa kiongozi wa wawindaji hapa Kijijini kumekufanya usahau kama Kuna mtu Mmoja anayekuzidi madaraka hapa"

Manumbu Anacheka kidogo " nani huyo"

"Mimi" anajibu nzagamba na vijana wote kumwangalia kwa kutokumuelewa akiwemo manumbu anayeendelea kucheka " pombe ninywe Mimi ulewe wewe" anadhihaki manumbu

" subiri nikukumbushe kidogo" nzagamba anaendelea " nani aliyeshinda kurusha visu kabla hatujaenda jando?" anauliza swali na kutulia kidogo " Mimi " anajibu swali mwenyewe nzagamba " nani aliyeenda jando na kutahiriwa pasipo kulia?" anauliza " kwa ninavyomkumbuka uvumilivu ulikushinda dakika za mwisho ukalia mpaka kamasi" nzagamba anaendelea kumzalilisha manumbu na vijana kucheka.

Licha ya vijana wengi kulia wakiwa jando kutokana na maumivu waliokuwa wakipitia baada ya kutahiriwa nzagamba hakutoa chozi hata kidogo kwani ilikuwa ni wiki mbili tu tangu baba yake afariki na alimwahidi kuwa imara maumivu ya jando yote aliyaweka nyuma Ili kutimiza ahadi yake kwa baba yake. Hiyo ilimfanya kuwa kiongozi wa vijana wote na aliendelea na uongozi wake hadi walipoingia Kambi ya mafunzo na uongozi wake ulikuja kupotea baada ya majaribio ya mwisho.Vijana wote wanakubaliana na hilo kwani kutoka na Mila na desturi nzagamba ndio kiongozi hata kama asinge faulu mtihani wa mafunzo ya mwisho.

" kwa hiyo Mimi bado ni kiongozi wako manumbu kwani katika mitihani yote tuliofanya Mimi nilifeli mmoja kati ya minne na wewe ukafaulu Mmoja,subiri kidogo hata huo hukufaulu peke yako kwa ninavyojua mmegawana uongozi pasu na kilinge,kwa hiyo nakuonya hiii itakuwa mara yangu ya mwisho kukuvumilia siku nyingine sitakuacha" anaonya nzagamba na kutaka kuondoka lakini manumbu hakukubali kushindwa anamvuta bega " naona Sasa unataka kuoa unaanza kutafuta vyeo,mtu mwenyewe umeonewa huruma tu"

Nzagamba anageuka na kumpiga ngumi ya uso, manumbu nae hakuwa nyuma licha ya kuwa amelwa. kukawa vurugu ya piga ni kupige hakuisha dakika manumbu alikuwa chini wakaja vijana waliokuwa upande wake na kumsaidia wakiondoka nae akiendelea kuvurumusha matusi.Nzagamba anasimama akifura kwa hasira " usijali nzagamba unajua hawezi kuvumilia aibu huyo kukataliwa posa sio kitu Cha mchezo" anaongea kijana Mmoja aliyekuwa karibu na nzagamba na wengine kukubaliana nae.

"kakataliwa posa?kwani alikuwa anaoa tena" anauliza nzagamba akijifuta Kona ya mdomo Wake kwa kiganja chake Cha mkono

"kwani ulikuwa hujui sisi tunadhani unajua" anaongeza mkita.

"Mimi nitajuaje ndio nasikia hapa"

" kwani wewe si unaoa?" mkita anamuuliza

" nimepokea hiyo taarifa Leo jioni kutoka kwa mama hata sijafanya maamuzi bado,haya hiyo inahusiana nini na posa ya manumbu?" nzagamba anaendelea kushangaa

" kweli utakuwa hujui" inambidi mkita kumwelezea Kila kitu.

" ndio maana manumbu kasema umeonewa huruma tu,lakini usijali anaona wivu tu umechaguliwa wewe sio yeye" anaongezea mkita akimwangalia nzagamba anayechemka hasira na kuhakiki hisia zake zilikuwa sahihi.

Asubuhi tulya anaamka mapema na kuwashangaza watu walioamka na kumkuta kamaliza kazi zote akiwa na Ari mpya ya kujiandaa na maisha ya ndoa "uko sawa" sinde anamuuliza na tulya anampa tabasamu pana kabisa.

" Niko sawa kuliko siku zote,kama ulivyosema nilichokuwa nakitafuta nimeshakipata na sitaki kukipoteza kizembe" wakati sinde anamshangaa anatoka mama Yao runde " nilijua utakuwa bado unalia" runde anamtania tulya " kaamka mapema leo na ameshamaliza kazi zote za asubuhi" sinde anamwambia mama yake

" ndio vizuri anaenda kuwa mke wa mtu,na kuanzia Leo Amna kutoka" runde anatoa amri " hapana shangazi unaonaje nikianza kukaa ndani wiki ijayo wiki hii unifundishe kufinyanga vyungu"

runde anamwangalia kwa mshangao" unataka kujifunza kufinyanga?"

" ndio,sitaki kuilaza familia yangu njaa"

" hivi ni wewe tulya au umemwacha usingizini"sinde anatania

" mwache mwenzio kaamua kukua,hata hivyo utakaa ndani nitakufundisha ukiwa ndani sitaki bibi harusi wa watu adhurike isitoshe ulimsikia mjombaako jana"

" hapana mama unaweza kunisaidia kuongea na mjomba tafadhali sitafanya fujo mpaka siku ya harusi naahidi,nataka nijifunze Hadi namna ya kuchagua udongo mzuri nitajifunzaje nikiwa ndani na udongo porini" anabembeleza tulya "wewe mwenyewe unasema mfinyanzi mzuri ni yule anayechagua udongo mzuri kwanza,nisaidie mama" anabembeleza tulya na kumfanya runde asiwe na njia nyingine ila kukubali na anavyojua tulya akiamua kitu haachi mpaka akipate kwa hiyo kumkatalia ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

" sawa,punguza kuongea una maneno mazuri Nina uhakika mumeo atakuwa hajui kukukatalia kitu" anaongea runde na kumfanya tulya kuona aibu kidogo kwani tayari nzagamba ameanza kuonekana kama mumewe na hajui ni kwa nini anajisikia furaha kwa hilo.

" haya kajiandae upesi Nina uhakika bibi sumbo na nzagamba watakuwa hapa kukuona ninavyojua bibi sumbo huenda na muda" runde anakumbusha na kuingia ndani.

" twende nikakusaidie upendeze Hadi nzagamba akikuona ashindwe kunywa maji" sinde anatania na wote wanaelekea nyumba waliokuwa wakilala " kwa nini ashindwe kunywa maji"

" kwa sababu Kila akishika kipeo Cha maji anakuona wewe hawezi kukumeza hujui hiyo"

" naona unaona raha kunitania si ndio" wote wanacheka.

Wanaingia ndani sinde anamsaidia kuvaa na kumfunga nywele zake ndefu kwa mabutu matano yaliyokaa vizuri kichwani.

" umependeza,Nina uhakika atasema akuoe Leo hii" sinde anazidi kumtania akipita Mbele na kumwangalia vizuri lakini tulya anaonekana mwenye mawazo " vipi unawaza nini tena si tulishayamaliza hayo" tulya anavuta pumzi ndefu na kusema " itakuwaje asiponipenda"

" kwa nini asikupende acha ujinga huo"

" ninasema tu asiporidhia kuwa na Mimi je" anaongea tulya akiwa na wasiwasi endapo na yeye atakataliwa kama alivyokuwa anawakataa wengine kwani wahenga waliosema kinachoenda siku zote hurudi isipokuwa kifo walikuwa Wana maana yake.

sinde anaenda kukaa pembeni yake " kwa nini asiridhie Nina uhakika atakupenda wewe ni mrembo sana tulya kuliko hata huyo lindiwe wake" sinde kumtaja lindiwe kunafanya moyo wa tulya kutulia kwa sekunde kwani alishasahau kama nzagamba tayari aliwahi kuwa na mchumba na simulizi inasema kuwa alimpenda sana.

" vipi Kama bado anampenda lindiwe" anauliza sauti ikikwaruza na moyo ukiwa mzito.

" mbona una vipi nyingi hivyo, yule tulya aliyeamka na Ari ya kuokoa himaya yote ya mpuli kutoka utumwa wa mtemi mbilu Yuko wapi hata hivyo wewe mwenyewe uliwahi kuwa na mchumba kwani bado unampenda"

tulya anatikisa kichwa kukataa " unaona,hayo yote ya zamani nzagamba ni mwanaume mzuri Nina uhakika atakujali unabahati ujue na umepata mama mkwe mzuri asiye na kelele kama bibi sumbo,kwa hiyo Rudi katika Hali yako ile ya mwanzo Leo siku yako ya kuchumbiwa utaikumbuka" sinde anampa moyo na tulya anarudi katika Hali ya mapambano " sawa hapa mwendo Mbele hakuna kurudi nyuma" anajikakamua tulya.

Runde anakuja kuwaita kwani tayari wageni wamewasili licha ya kujitoa wasiwasi tulya bado alikuwa anatetemeka,anatoka akiwa na sinde pembeni yake.wanafika nyumba kubwa sebuleni na kumuona Mzee Shana,kaka yake kilinge hajamuona zinge akijua atakuwa ameondoka mapema kwenda kutoa taarifa nyumbani kwao.walikuwepi wazee wengine wawili na mama wa makamo Moja kwa Moja anajua atakuwa mama yake nzagamba macho yake yanaangaza na kutokumuona anayemtafuta na macho yake unarudi kwa bibi sumbo anayempa tabasamu pana kabisa.anasalimia kwa heshima na kuambiwa akae na anakaa karibu na shangazi yake runde.

Kikao kinaendelea na wazee kufikia muafaka atatolewa mahari ya mbuzi wa nne na hiyo kumfanya tulya kuwa mchumba halali wa nzagamba.

" Nzagamba Yuko wapi mama" anauliza kilinge na tulya kumwangalia bibi sumbo kwani hata yeye pia alikuwa anataka kujua.

" usijali kuhusu yeye karidhia na ameenda kuwataarifu kaka zake ndio maana hajaja" bibi sumbo anatoa ufafanuzi na tulya anapata nafuu kidogo " si angeenda hata kesho tu,nimetumia nguvu nyingi hivyo kukupendezesha" ananong'ona sinde aliyekuja na kukaa pembeni yake, tulya anampiga kumwashiria anyamze.

Kikao kinaisha wazee wanaondoka bibi sumbo anakaa kuongea na runde kuhusu kumtunza mwali na maandalizi ya harusi baada ya kumaliza anaenda kuonana na tulya ambaye alisharudi nyumbani kwao " tulya njoo mara Moja" runde anaita.

tulya anatoka na kumuona bibi sumbo akiwa na runde anainamisha kichwa chini kukwepa kumwangalia usoni kama heshima kwa mkwewe " usifanye hivyo Binti yangu niangalie usoni Mimi ni mama yako Sasa sio mama mkwe sawa" anaongea bibi sumbo kwa sauti iliyojaa upendo na kumfanya tulya ajione Yuko karibu nae na kumpenda bibi huyu kwa sauti tu.

"karibu kwenye familia yetu Mimi ndio mama yake nzagamba,asante sana kwa kumkubalibali mwanangu jinsi alivyo Nina uhakika mizimu itakuachia baraka nyingi maishani mwako kwa kuwa na moyo mkubwa kiasi hiki" anaongea bibi sumbo machozi yakimtoka na moyo wa tulya na kujaa simanzi kwa bibi huyu aliyepitia mengi kuchelewa kuzaa,kufiwa na mumewe na kumwacha na kijana mdogo aliyekuwa bado anahitaji malezi ya baba yake hiyo haikutosha matatizo ya mtoto wake kukosa bahati,uchumba kuvunjika na maneno mengi waliongea watu lakini bado kasimama imara pasipo kukata tamaa,tulya anajikuta akijiapia moyoni kumfanya uzee wake apumzike apate faraja kidogo na atamtunza vizuri.

" haya ni machozi ya furaha Binti yangu" anaongea bibi sumbo akifuta machozi na kumfanya tulya nae arudishe machozi yake yaliyokuwa yakimzi uwezo machoni.