Chereads / penzi la bahati / Chapter 12 - chapter 11

Chapter 12 - chapter 11

"amesemaje huyu" anauliza kuhakiki masikio yake.sinde anaruka kwa furaha " hongera tulya inaonekana utaolewa kabla yangu" lakini tulya hakuwa na furaha hata kidogo akawa kama kamwagiwa maji ya mtungi,sinde anazima furaha yake baada ya kumuona tulya aliyekuwa amezubaa"vipi mbona uko hivyo" anauliza akimwangalia " usiwe na wasiwasi baba atakuwa ametafuta mwanaume mzuri tu" anamfariji " una uhakika asije akawa Mzee kama mama alivyosema" anaongea moyo wake ukijawa na hofu kuhusu mchumba anayekuja.

Wakiendelea kujadiliana anafika runde " vizuri nimewakuta" anaongea akiwafuata walipo anafika na kumwangalia tulya aliyekuwa akitetemeka " nenda ukajiandae Kuna wageni wanakuja sinde msaidie kutengeneza na hizo nywele Hana muda wa kusuka mfumue uzifunge vizuri" anatoa maelezo na kuelekea ndani anageuka na kuwaona bado wamesimama " bado mnafanya nini hapo,upesi we tulya kaoge,wakati huo sinde njoo huku unisaidie kuandaa vinywaji vya wageni" wanashtuka na wote wanaitikia "sawa" runde anaingia ndani " fanya kaoge,ngoja nikamsaidie mama,ukimaliza nakuja kukutengeneza nywele" tulya anaitikia kwa kichwa sinde anamshika bega " usiwe na wasiwasi Kila kitu kitakuwa sawa haya nenda ndani" sinde anakimbia kuelekea nyumba kubwa na tulya anaelekea nyumba nyingine ndogo.

Anafika ndani na kukaa kitandani akili yake ikiwa imevurugika kabisa,ghafla anajikuta anamuwaza nzagamba na moyo wake unaanza kumwenda mbio "utakuwa umechanganyikiwa tulya wakati kama huu sio wa kumuwaza nzagamba" anaamka na kuchukua kaniki anajiandaa na kuelekea bafuni kuoga baada ya muda anarudi anachukua mafuta yake yaliyotengenezwa kutokana na maziwa ya Ng'ombe na kujipaka anavaa sketi yake fupi iliyomfika magotini,kinafuata kitambaa Cha kufunga kifua chake anakiangalia vizuri na kukifunga kifuani pake akiacha tumbo wazi kama ilivyo mavazi ya kiasili anatafuta viatu vyake vya kamba uvunguni na kuvivaa akizungusha kamba zake kufikia usawa wa magoti na kufunga alikuwa tayari.

kwa Binti ambaye hajaolewa hakuwa na vitu vingi vya kuvaa kama mwanamke aliyeolewa.

Anasogea kwenye ubao uliokuwa umegongelewa miti ukutani mwa chumba Chao anatoa kikapu kilichokuwa juu ya ubao huo anakishusha na kutoa chana Cha miti na kurudisha kikapu juu anakaa kitandani na kuanza kufumua nywele zake za mstari kichwani.Wakati akifumua ya pili anafika sinde " lete" tulya bila kubisha anampa chana sinde na kuanza kumfumua "una uhakika uko tayari kwa hili,kama hauko tayari niambie naweza kukusaidia kufanya vimbwanga" tulya Anacheka kumsikia sinde anataka kumsaidia kuharibu uchumba " usifanye hivyo,unataka Tinde avunje uchumba ubaki kama Mimi" anamwambia sinde aliyekuwa anafumua nywele anaacha kidogo "ndio itakuwa vizuri Ili tuwe tunazunguka wote ngomani Kila siku" anajibu na kuendelea kufumua "asante sana sinde kwa kujaribu kunitia moyo lakini usijali, Mimi kweli Niko sawa,na kingine kama mchumba kamchagua mjomba ninauhakika atakuwa ni mzuri sitaki kumwaibisha mjomba" anaongea sauti ya chini akijiona Hana njia ya kutokea katika pori lililojaa miti yenye miiba " umesikia chochote kuhusiana na mchumba" anauliza baada ya kimya kifupi "sijasikia nimejaribu kumuuliza mama lakini hajasema chochote nadhani wanahofia ukijua utafanya fujo" sinde anamaliza kufumua anampa Chana tulya Ili achane.

"Vipi kuhusu malengo yako?" sinde anauliza na kumfanya tulya aliyekuwa anachana nywele aache kwa muda na kuendelea "Haina haja tena nimevumilia na kufanya vitu vyote kwa mda mrefu sana na bado sijafanikiwa wanaume wote wanaokuja wanataka kunioa mke wa pili tu,siwezi kuendelea kukataa tu pengine mizimu ndivyo ilivyonipangia na Mimi napingana nayo,Leo hii hata wakisema niwe mke wa tano naolewa tu" sinde anamwangalia ndugu yake na rafiki yake anayeonekana kukata tamaa hajawahi kumuona tulya akiwa amekufa moyo namna hii mda wote huonyesha nguvu na hari ya kupambana hata na Simba lakini Leo hii alikuwa kama ndege aliyekatwa mabawa na kuambiwa apae.

Sinde anavuta pumzi ndefu na kuanza kumbana nywele" usiwe hivyo kuwa na matumaini kuwa mchumba atakuwa yule unayemtaka sawa,na Mimi naomba kwa mizimu ikutimizie lengo na haja yako" tulya anajisikia faraja kidogo kusikia maneno ya sinde na kujipa moyo.

"umependeza" anaongea sinde baada ya kumaliza kumbana nywele tulya na hapo wanasikia watu wakiongea nje "watakuwa wamefika" sinde anaongea na kuelekea mlangoni kuchungulia "kaniletee maji ya kunywa uone nani amekuja" tulya anamtuma sinde nje na sinde anaelewa anamaanisha nini anatoa tabasamu pana na kusema "usijali kazi yako imepata mtu wa kuifanya" anatoka njee haraka haraka akifunga mlango taratibu usijibamize.

Tulya anabaki mle chumbani akizunguka huku na kule kijasho kikimtoka licha ya kuwa anajipa moyo kuwa ataolewa na mwanaume yeyote yule upande mwingine wa moyo wake bado ulikuwa unamtuma amjue huyo mwanaume anayetaka kumuoa kabla ya kutoka njee kwa wazee na anamatumaini kuwa sinde atamjua vizuri, sekunde kwake ilikuwa kama mwezi na dakika kama mwaka akijiuliza sinde ameanza kufanya nini mda huo wote na wazo likimtuma kuchungulia nje anageuka na kuelekea mlangoni kabla hajafika mlango unafunguliwa na sinde anaingia akiwa na maji kwenye kipeo.

"umeanza kufanya nini mda wote huo" anauliza tulya baada tu ya kumuona "vipi umemuona?ni nani?,unamjua?ni mzuri? hapana uzuri sio tatizo ni kijana?,ameoa?" anamtupia maswali mfululizo sinde akishindwa ajibu lipi " sijui,nimewakuta wazee watupu huko nje hata sijui nini kinaendelea" anajibu sinde akionekana kama kakata tamaa na hiyo inamchanganya tulya "unanitania si ndio,haiwezekani mjomba anichagulie Mzee hata kama mama alisema hivyo" sinde anamwangalia kwa kutokujua afanye nini

" Mimi mwenyewe sielewi waliokuja ni wazee na wote Wana watoto umri kama Mimi au zaidi" anaeleza sinde na kumfanya tulya ajitupe kitandani mwili ukimuisha nguvu na macho yake yakianza kuona Dunia inazunguka.Sinde ananyanyuka na kumpa maji aliyokuja nayo,tulya anakataa na sinde anaweka chini,kwa Hali aliyokuwa nayo anaona hayatapita kooni kabisa "tusijipeleke Mbele sana labda kachelewa anakuja" anamtia moyo na tulya anamwangalia kwa matumaini kidogo.

Mlango unafunguliwa anaingia runde na wote wanasimama kwa pamoja kama askari aliyemuona mkuu wake wote wakijua mda umewadia " umependeza Binti yangu mama yako angekuona angefurahi sana" anaongea runde akimshika bega tulya akimkagua kuanzia kichwa mpaka mguu,tulya analazimisha tabasamu ambalo halikufika machoni "haya twende wanakusubiri na ukumbuke usifanye fujo kabisa au mjombaako atatuua wote humu ndani" anaonya runde akimshika mkono tulya na kuanza kuelekea nje,sinde nae akiwafuata nyuma lakini mama yake anamzuia "unaenda wapi? nenda kawaangalie kaka zako kule kwa zinge wambie waje huku upesi" anaagiza runde na kumfanya sinde akunje sura, mama yake kumbania kwenda kushuhudia uchumba wa tulya na kumjua mwanaume anaemuoa.

Wanatoka nje na sinde anaelekea nyumbani kwa kaka yake zinge kuwaita kabla hajafika anakutana nao njiani wakija "wageni wamewasili" anauliza kilinge akimpita sinde na kutangulia Mbele " ndio,mama kasema muwahi" na wote wanaendelea kutembea "hivi kaka mnajua nani anayemchumbia tulya?" anauliza sinde akili ya kutaka kujua ikimzidi uvumilivu kilinge anasimama na kumfanya zinge nae asimame " kwani umeambiwa uende kwenye kikao" anauliza kilinge sauti yake ikiwa ya ukali na sinde anajibu kwa kutikisa kichwa kilinge anaendelea " Sasa huku unaelekea wapi?" hapo sinde ndio anagundua kuwa alikuwa anawafuata kaka zake kuelekea nyumba kubwa akipita nyumba aliokuwa analala yeye na tulya " haya urudi huko,ungejua haya yote ni makosa yako ya kutokutulia kwako nyumbani" kilinge anamtupia sinde lawama lakini kabla hajaendelea zinge anamzuia " acha usisababishe varangati na unajua Kuna wageni baba akijua hatapenda kabisa twende tunasubiriwa" kilinge anafumba macho kuzuia hasira zake na kuanza kutembea " nenda ndani" zinge anamwambia na kumfuata kilinge,sinde aliyekuwa ameduwaa kutokana na lawama za kaka yake asijue yeye kahusikaje na uchumba wa tulya anarudi ndani ubongo ukikaribia kumtoka kwa msongo wa mawazo akiwaza inawezekana yeye ndo Kasababisha tulya kuolewa na Mzee lakini vipi.

"ni mrembo kweli na anaonekana ana heshima" anaongea Mzee Mmoja kati ya wazee waliokuwa kwenye kikao na wengine wakiitikia kwa "mmh" "kinachofuata ni kupanga kiasi cha mahari " anaongezea Mzee mwingine akishika ndevu zake.Tulya aliyekuwa akipoteza uvumilivu wa kutaka kujua anaemuoa nani kwani waliokuwepo hapa wote walikuwa ni wazee mda wote akiangalia njia kuona kama Kuna kijana yeyote atajitokeza kufika akiwa amechelewa kama sinde alivyosema lakini mpaka Sasa hajafika na amejuwa wazi kuwa kati ya wale wazee pale ni mume wake mtarajiwa, kifua kinabana anatamani kulia anaangalia juu kuzuia machozi yake.

Anashtuliwa na mkono wa runde uliomshina begani anamwangalia runde na runde anaachia tabasamu na kumnong'oneza " nenda ndani" tulya anasimama ile anataka kupiga hatua anataka kuanguka kilinge anawahi na kumdaka anamsaidia kusimama mwili wake ulikuwa umekosa nguvu kabisa anamwangalia kilinge " Niko sawa kaka" kilinge anamwachia na tulya anaanza kupiga hatua kumtoa eneo lile " mnaweza sema Mahali yeyote ile kwani manumbu amesema Yuko radhi kuitoa" anasikika Mzee Mmoja na kumfanya tulya kuganda alipokuwa, akijaribu kutafakari kama masikio yake yamesikia vizuri "Haina shida kwa kuwa wazazi wake waliniachia jukumu hili nitakuwa Mimi wa kuitaja mahari hiyo na nili...." kabla Mzee Shana hajaendelea anakatishwa na sauti ya tulya aliyerudi na kusimama karibu na Mzee Mmoja " umesema nani anatoa mahari babu?" anauliza sinde akimwangalia Mzee aliyeshtuka kutokana na sauti ya tulya aliyozungumzia karibu na sikio lake na wengine wote kumwangalia tulya kwa maswali " manumbu" anamjibu Mzee mwingine " kwa nini manumbu atoe mahari" anazidi kuuliza tulya akisahau kuwauluza wazee hasa wakati wakifanya maamuzi huwa Kunahesabika kama ukosefu wa nidhamu " kwa sababu ndiyo anayekuoa" anajibu Mzee aliyeulizwa swali awali na tulya "wewe ulitaka atoe nani kama sio mumeo mtarajiwa" maumivu makali ya kichwa yanamjia tulya na kuona Dunia yake imefika mwisho akili yake ikichanganua na kujua mwanaume anayetaka kumuoa ni manumbu " mama kilinga mpeleke ndani huyo" mzee Shana anamuamuru mke wake na runde bila kuchelewa ananyanyuka na kwenda alipo tulya na kumshika akimnong'oneza " twende ndani tulya usifanye fujo hapa" tulya anarudi katika uhalisia na kuanza kuondoka huku runde akimshika mkono.

Tulya anaanza kukumbuka Mambo mengi yaliyotokea kati yake na manumbu tangu afike hapa Kijijini na tabia zake manumbu za ulevi na kumpiga mke wake alipofika hapo pa kupiga akajiona akipigwa na manumbu mwili wake ukimvimba na akilia mwili unamsisimka anarudi katika uhalisia "haiwezekani,siwezi kabisa" anaongea kwa sauti ya chini ambayo runde hamsikii vizuri,wakati runde akijaribu kufikiria kasema nini tulya anamponyoka na kurudi walipo wazee "hapana sitaki kuolewa" anaongea kwa sauti ya juu na wazee wote kumwangalia.

"nilikwambia usiwe na shaka tulya hawezi kukubali kuolewa na manumbu" zinge anaongea kwa sauti ya chini akimwambia kilinge " anaweza kufanya fujo hapa na baba asifurahishwe nayo unajua hapendi kuaibishwa" kilinge anaongea kwa sauti ya wasiwasi upande wa moyo wake ukifurahi tulya kukataa uchumba upande ukiwa na wasiwasi nini kitatokea endapo tulya akifanya fujo zaidi " usijali, ninavyojua mjomba ni mkali na alifua dafu Nina uhakika baba nae hatafanya chochote" zinge anamtoa wasiwasi kaka yake huku akiwa na tabasamu pana usoni linalosema acha kombolela ianze kwani alikuwa anaufurahia mchezo.

"kwa nini?" anauliza Mzee aliyekuwa na mvi nyingi kichwani na macho mekundu akionekana kama kalewa ugolo " runde mpeleke ndani huyu haraka" anatoa amri Mzee Shana uso ukimghadhabika " sitaki kuolewa Mimi mjomba" anaongea tulya na wazee kubaki midomo wazi,wakati huo runde anafika na kuanza kumvuta " mwacheni aseme kwa nini, hatuwezi kumlazimisha ndoa sisi" anaongea Mzee Mmoja aliyekuwa akionekana kama kiongozi wa msafara huuu runde anamwachia na Mzee anaendelea " haya sema Binti kwa nini hutaki kuolewa?"

Tulya anazubaa kwani hakujiandaa kujibu swali kama hili anaanza kufikiria asemeje na kumsikia mzee Shana akiongea " Hana tatizo lolote huyu wazee ni msumbufu tu,aende ndani tuendelee na kikao" anaongea huku akimwangalia jicho la onyo tulya, lakini hakuwa kwenye wakati wa kukabiliana na onyo lolote kwani anajua akilaza damu ataingia kuzimu na hakuwa tayari kwenda huko hivyo inambidi kujikwamua kwa Hali yoyote ile " Kuna mtu tayari nampenda na nataka kuolewa nae" analopoka na watu wote kumwangalia.Mzee Shana anasimama alipokuwa amekaa na kwenda aliposimama tulya "sema ninani unaempenda kama ukikosa jibu utanijua Mimi ni nani" anaamrisha Mzee Shana kilinge na zinge wanaamka upesi na kwenda upande walipo kutoa msaada endapo Hali yoyote ikijitokeza.

Tulya anakosa jibu kwani hakuwa hata na mtu wa kumtaja " mpelekeni ndani atake asitake ataolewa" Mzee Shana anazidi kuunguruma kutoa amri,Amna mtu aliyejitokea kumtoa tulya wote wakiwa wamesimama tu na hii inamkera zaidi Mzee shana " kilinge mtoe huyu nimesema" kilinge anasogea alipo tulya na kumshika mkono akimvuta aondoke " nzagamba" analopoka tena tulya kujiokoa kuolewa na manumbu " nzagamba ndio nanaempenda nataka kuolewa nae."